Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

kwa maelezo fikirishi tu Majimbo yapo ndani ya wilaya na wilaya hipo ndani ya mkoa. Mkuu wa mkoa na wilaya miaka ya sasa ndio wamekuwa kama wanafanya kazi zisizo zao sijui mfano hapa Dar.
Tindo,
Huenda nami niko kwenye kundi la mkuu 'chizcom', hasa katika mstari huu, kwa maana sijui kazi za mbunge jimboni siku hizi.

Itasaidia sana kama kuna elimu tusiyokuwa nayo sisi juu ya hilo tukaelimishwa.
Huenda kuna jambo ambalo hukulielewa katika bandiko aliloweka mkuu 'chizcom' na kukusababishia hisia za kumjibu kama ulivyomjibu.
Au pengine kuna nisichokijua mimi kilichopo kati yenu?
 
Eeenh, kana kwamba huu ndio ukweli wenyewe na hakuna ukweli zaidi ya huu.

Inahitaji mtu awe katokea kwenye sayari nyingine ambayo haina mawasiliano yoyote na hii yetu kuanza kuaminishwa kwamba mambo ndivyo yalivyo kama ulivyoyaelezea.

Uzuri wenyewe ni kwamba hata wewe unayeyaandika haya unakaa chini na kuanza kujiuliza inakuwaje wawepo watu wa kuamini porojo zisizokuwa na chembe yoyote ya ukweli?

Lakini inajulikana, kwako wewe hilo halina mashiko, lenye maana ni kufurahisha na kuwa na mategemeo ya kesho na keshokutwa, kama hii leo kazi bado haijarasimishwa.
 
Hipo = Ipo
Hawe = Awe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekosa kazi ya kufanya? Umekosa story ya kuandika? Ongelea hata Simba na Yanga tu. Kuliko KUONGELEA USICHOKIJUA.
 

Nimemshukuru kwa bandiko lake, lakini uandishi wake una matatizo ya msingi.
 
Paschal Mayalla kwa nini unapenda sana kurudia huu uongo mara kwa Mara ?!! Mwigulu Nchemba hana 1st Class ya Economics toka UDSM! alipata Upper Second na Form Six pale Mazengo alipata Division II ya point 10 akiwa na E ya Economics.
Hivyo Mwigulu ni wa kawaida tu tatizo ni umbumbumbu wako tu Paschal pale uliposikia Mwigulu alikuwa Mchumi daraja la Kwanza pale BOT!
Mchumi Daraja la Kwanza haimaanishi GPA aliyopata UDSM ni rank ya nafasi aliyofikia kama Mchumi pale BOT au tuseme alikuwa Mchumi Mwandamizi.Paschal Mayalla Mwana Ilboru unakuwaje Kila.za hivyo kwa vitu vidogo kama hivyo?
 
Umekosa kazi ya kufanya? Umekosa story ya kuandika? Ongelea hata Simba na Yanga tu. Kuliko KUONGELEA USICHOKIJUA.
Muheshimiwa kumbe umo humu sasa ombi langu moja tu kwako:
TUNAOMBA UFUTE MAANDISHI YAKO YALIYOTAPAKAA NCHI NZIMA "mwigulu rais 2015".......Ahsante!
 
Pascal umeamua kujitoa ufaham mchana kweupe, kama magufuli ameagiza mpaka wagombea wenyeviti wa mtaa wakatwe atashindwaje kumzuia mbunge kama mbunge huyo n threat kwake? Pascal rejea kwa maada ya presenter!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe rudi shule kwanza, kwa sababu hii ndo shule kubwa zaidi kuliko hiyo ya makaratasi .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekosa kazi ya kufanya? Umekosa story ya kuandika? Ongelea hata Simba na Yanga tu. Kuliko KUONGELEA USICHOKIJUA.
Mheshimiwa hivi kuongelea Simba na Yanga ni kwa wale wasiojua? Nafikiri issue ni kueleweshana tu unachokijua ambacho mimi sikijui. Kama kuna mambo umefanyia Iramba yaseme Mheshimiwa - hicho tu!
 
Mheshimiwa hivi kuongelea Simba na Yanga ni kwa wale wasiojua? Nafikiri issue ni kueleweshana tu unachokijua ambacho mimi sikijui. Kama kuna mambo umefanyia Iramba yaseme Mheshimiwa - hicho tu!
Wanayajua Wanairamba, Siwajibiki kukwambia wewe. Na Panapohitaji ufafanuzi kila mwaka napita kila Kijiji kufafanua na kupata maoni yao
 
Wanayajua Wanairamba, Siwajibiki kukwambia wewe. Na Panapohitaji ufafanuzi kila mwaka napita kila Kijiji kufafanua na kupata maoni yao
Nauhakika hiyo kila mwaka mwisho ni mwaka huu kwani kuanzia mwakani wewe utatakiwa kushirikiana na mbunge ajaye kumpa ama kumuhoji taarifa ya kijiji husika
 
Wanayajua Wanairamba, Siwajibiki kukwambia wewe. Na Panapohitaji ufafanuzi kila mwaka napita kila Kijiji kufafanua na kupata maoni yao
Mhe.Mwigulu Nchemba kumbe upo Mheshimiwa!
Mimi swali langu ni dogo tu Mheshimiwa,hivi mbona siku hizi huvai Skafu kama zamani?
Wewe ulituaminisha kuwa kuvaa Skafu ni kuonyesha uzalendo uliotukuka, Je uzalendo wako hupungua ama kuongezeka kulingana na madaraka uliyonayo? Ni hayo tu Mheshimiwa!
 
Wanayajua Wanairamba, Siwajibiki kukwambia wewe. Na Panapohitaji ufafanuzi kila mwaka napita kila Kijiji kufafanua na kupata maoni yao
Ya kila kijiji hapana Mheshimiwa - mbona sijakuona wala kukusikia kijijini kwetu. Ila bhana shangazi yangu bado anavaa ile t-shirt ulimgawia wkt wa Uchaguzi MWaka 2015. Ulimsaidia sana Mheshimiwa.
Hoja yangu kubwa naiona ni wewe kujikita sana ktk siasa za Nchi badala ya kujali Jimbo letu. Umeshindwa kuwaunganisha Wanairamba wawe kitu kimoja na ndiyo maana kila inapotokea uchaguzi wanatokea utitiri wa kuwania hiyo nafasi. Nashindwa kusema wale wanaotokeza nao wameshindwa kuwaunganisha wanaIramba kwa kuwa hawajapata nafasi.
Nikiangalia kuanzia enzi za Kiula mpaka wewe hamna hata mmoja aliyewahi kujaribu kutengeneza mtandao mkubwa kwa watu wa Iramba wenye uwezo kwa ajli ya maendeleo ya jimbo letu. Huko Dar-es-Salaam nasikia kuna vi-umoja ambavyo vinajaribu kuwaweka WanaIramba waliopo nchini na nje ya nchi ili waweze kusaidia katika kuiendeleza Iramba na wewe umekuwa ukiwekwa kama Kiongozi lakini jukumu lako hulitekelezi ipasavyo na mwisho wa siku kinachokusudiwa hakifikiwi. Kuna experience nzuri tu kuwa WanaIramba waliowahi kubahatika kupata nafasi ya kiuongozi humalizwa haraka kwa sababu huwa hawajajitengenezea network nzuri kwao. Mfano Mzee Nalaila Kiula akiwa Waziri Maarufu alipogeukwa alimalizwa kwa urahisi sana na kwa kuwa alitumia mbinu za kuwahonga honga wapiga kura Iramba basi ndiyo ikawa mwisho wake na hamna anachoweza kujivuna alikifanya Iramba. Kuna David Jairo naye alipogeukwa hamna mwanaIramba alilisikitika kuwa mtu wao kaonewa.
Ukweli mnajisahau sana mnapopata uongozi wa kinchi- sijui inakuwa kama mmelogwa?! Sasahivi nikitafaksari hata posts zako ingawa na ukorofi bado unao kama ulivyonijibu mimi kuwa "huwajibi kuniambia mimi" lakini ndani yako kuna hofu. Hofu uliyonayo ni wewe kutofautiana na Mkulu wako. Unaegemea kwa wananchi lakini ukweli miaka kumi uliyokaa tayari inachosha na kidemokrasia kwa kweli anatakiwa mtu mwingine wewe mbinu zako ni zile zile za mbwa mzee. Ushauri wangu - kwa kuwa una Phd na unaufahamu uchumi vizuri na nafasi ambayo umekwishaipata ni vema ukaangalia kazi za kimataifa ili ukikomaa kwa ajili ya kurudi kugombea Urais Mwaka 2025. Kwa Iramba unapaswa kumtafuta mtu wa kukurithi ili utaporudi kugombea Urais aweze kukupa nguvu kwani ukiwa huko unaweza ukamsaidia kuletea maendeleo jimbo letu.
Leo naandika hivi na kwa kuwa wewe ni mwanasiasa unaweza usinielewe ila utapokuja kukatwa wkt wa uchaguzi utaikumbuka hii post urudie kuisoma tena. Angalia wale ambao unaona wana nia ya kugombea au wale ambao wananchi wanawataja taja panga nao namna utavyowaachia na usigombane nao utakuwa umejitengenezea heshima sana.
 
LABDA MB AJAE WA JF, ILA KWA IRAMBA WASUBIRIE WANAIRAMBA WAKUPE MAJIBU
Mayu lisemwalo lipo - usipuuze kwa maneno ya kejeli hivyo. Kiula, Kilimba n.k wakati wanatoka kwenye Ubunge hawakuamini. Wewe bado kijana na umeshatumikia awamu mbili nakushauri kuwa flexible angalau anza hata kuandaa mrithi ili uondoke kwa heshima na hata ukiamua kurudi after 5 years ukikosa Urais utakuwa unaheshimika sana. Jipe likizo ndugu yangu. Niaminin mimi ukikosa Ubunge Mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wako kurudi kwenye chati tena.
 
Umekosa kazi ya kufanya? Umekosa story ya kuandika? Ongelea hata Simba na Yanga tu. Kuliko KUONGELEA USICHOKIJUA.
Nakupa heko sana Kamanda. Angalau huwa unajibu hoja - kwangu mimi ungekuwa Mbunge wangu kura unapata tu mwaaaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…