Muzzle ipo [emoji23][emoji23][emoji23]
Umeishashindwa kumuhimiri...hiyo Muzzle unaifungaje!!?
=====
Ila uzi huu umenikumbusha tukio la utotoni...! Niliwahi kupewa zawadi ya mbwa mdogo na familia rafiki na yetu. Kalivyo kua kua nikawa na kaachia kambwa hako...! Kisha nikapata ushauri kuwa nikachanganyie nyigu/ dondola na nyuki kwenye chakula kawe kakali nikafanya hivyo kwa dozi ya wiki ya wadudu hao.
Siku moja tulienda shambani ( mbali kidogo na nyumbani) tukasahau kukafungia vizuri kwenye banda kambwa kangu hako, na jiikoni tuliegesha mlango ( waliowahi kukaa shamba watakuwa wananielewa). Jikoni tuliacha kiporo safi juu ya mafiga. Jua lilipokolea shambani nikaagizwa nikaandae mazingira ya mlo wa mchana siku hiyo. Kwa kuwa nilikuwa na njaa akili ikawa imegota kwenye kiporo wakati natoka shambani kurudi nyumbani.
Kufika nyumbani kwa mbali kidogo nikaona mlango wa jiko umepigwa chini! Nikajua kuna namna! Nikajihami, nikatafuta tawi la mti imara mkavu kutoka kwenye uzio hapo hapo nyumbani! Akili ikanituma nisipitie mlangoni nizunguke kwa kunyata kwenda kuchungulia ndani ya jiko kupitia kwenye matundu ama nikifanikiwa kwenye dirisha dogo nyuma ya jiko! Kufika, kwenye tundu la kwanza sikuona vizuri ndani lakini nikasia dalili zote za kiporo mafigani kushambuliwa na mbwa!! Nikajua watakuwa mbwa wa majirani! Kujiridhisha nikaenda kwenye dirisha dogo.
La haulah !!! Kuchungulia ndani ni kambwa kangu ndiyo kanakula kiporo!!! Kalivyoniona eti kakanguruma na kubweka! Nikapandwa na hasira! Nikazunguka kwa speed ili nije nikabananishe mlangoni!! Kufika mlangoni nikakakuta kamebeba kiporo katoroke nacho! Hasira zikazidi, nikanyanyua lile tawi la mti kukadunda...kulishusha kakakwepa huku nako eti kamefura kwa hasira... nikanyanyua tawi kwa mara nyingine kushusha kakajikinga na sufuria la kiporo huku kamejisogeza kwenye kona!!! Na sasa kakawa kametuna na kamefura hasa! Machale yakanicheza kuwa sasa...Niongeze tahadhari...Nikanyanyua tawi mara ya tatu kukasurubu!!
Halooh!!! Kambwa kakalirukia tawi lile juu kwa juu na kulidaka kakashuka nalo. Mbilinge ikaanza kunyang'anyana tawi...! Asikuongopee mtu, mpaka muda huu kihoro kimeishaniingia! Kambwa kakafanikiwa kuninyang'anya silaha!! Kakadhibiti tawi! Tukabaki tumeangaliana! Kwenye pembe nyingine ya jiko nikaona mchi wa kinu...Nikawa na vizia kuuchukua ! Aisee...! Mbwa yule, sasa siyo kambwa tena, akarukia kwenye pembe ya mchi wa kinu huku kabeba tawi alilonipora!
Mpaka hapo nikaona nilirudishe majeshi nyuma, nitoke humo jikoni! Kugeuza shingo, akanirukia na kunitupa chini! Akanitia meno kwenye mkono wa kushoto niliokuwa natumia kumshambulia! Kisha mbio akatokomea kwenye mashamba ya majirani ya karibu na nyumbani
Zilikuwa Dakika kama tano hivi za heka heka na mbwa yule niliyepewa zawadi, kumbuka siyo kambwa tena!
Nilipoona picha za mbwa huyu hatari kwenye uzi huu nikamkumbuka mbwa wa zawadi, naye alikuwa na masiko yaliyolala na mfupi ila alikuwa na mkia mrefu! Kwa hiyo, si dondola wala nyuki waliokuwa wamemuongezea uhatari mbwa wangu wa zawadi bali ni asili yake ya kiumbwa.
Niwatakie Jumapili njema.