Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Aiseee don't buy this dogs hawafundishiki Mbwa pekee mwenye akili hata ukae usafir ukae miaka 5 lakini siku ya kurudi ata vibe na wewe ni Germany Shephered kwanza hao Rotwailler wana Visasi sanaaa ukimchapa anahifadhi moyoni
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]anahifadhi moyoni
 
Mkuu nafikiri kuna makosa ya kimatumizi maana kwa nijuwavyo hawa jamii hiyo ya mbwa huwa ni walinzi kwenye sehemu ambayo watu wanakuwa hawapo kwa muda huo.kama vile bank au mahali panapohifadhiwa vito vya thamani na huwa wanawekwa baada ya muda wa kazi na kuondolewa kabla ya muda wa kazi na watu maalumu na wenye mava,I maalumu, hawa ni moja ya jamii ya mbwa ambayo ni wakali sana na uwezi wao wa kupokea amri ni mdogo sana wao kazi yao ni kushambulia kilichoko mbele yao.
Mbwa hawa hufugwa na polisi na kampuni maalum za ulinzi na si watu binafsi,
Hi ni sawa kabsa
 
mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Asante kwa maelezo yaliyojitosheleza.
Kwa hiyo wanaogopa maji na ving'ora, siyo!?

Hata hivyo, kwa maelezo uliyotoa ninaona wazi kabisa hapa kuwa kufuga mbwa hawa ni sawa na kufuga nyoka aina ya cobra mwenye kichaa!!

Yaani maelezo yako, yanaonyesha kabisa kuwa hao Mbwa wanajaribu kutunyang'anya ufalme tuliopewa wa kutawala wanya walioko duniani.

Yaani mimi pia ni we mbwa mwenzao, maana kuwa kiongozi ( leader) wa mbwa lazima uwe mbwa! Mimi natakiwa kuwatawala( boss) mbwa, na si vinginevyo! Ingawa kuwatawala huko ni pamoja na kuhakikisha nawapatia mahitaji yote wanayotakiwa kupewa kama wanyamaa wa kufugwa.
 
Hii hapa
images%20(3).jpg
Kha ! Mbwa anakata jicho kama "mrekebisha wajeuri" ndani ya kundi?
 
Asante kwa maelezo yaliyojitosheleza.
Kwa hiyo wanaogopa maji na ving'ora, siyo!?

Hata hivyo, kwa maelezo uliyotoa ninaona wazi kabisa hapa kuwa kufuga mbwa hawa ni sawa na kufuga nyoka aina ya cobra mwenye kichaa!!

Yaani maelezo yako, yanaonyesha kabisa kuwa hao Mbwa wanajaribu kutunyang'anya ufalme tuliopewa wa kutawala wanya walioko duniani.

Yaani mimi pia ni we mbwa mwenzao, maana kuwa kiongozi ( leader) wa mbwa lazima uwe mbwa! Mimi natakiwa kuwatawala( boss) mbwa, na si vinginevyo! Ingawa kuwatawala huko ni pamoja na kuhakikisha nawapatia mahitaji yote wanayotakiwa kupewa kama wanyamaa wa kufugwa.
Kila mnyama anatabia zake, ili uweze kuishi naye lazima ujue tabia zake, simple.
 
Hawa mbwa ni hatari kuliko maelezo ....hili tukio lilitokea karibu kabisa na nyumbani kwangu sikulala usiku huo nilianza kusikia milio ya risasi kuanzia saa 7 mpaka saa 9 usiku ya aina mbalimbali ya bunduki nikajua ni majibishano ya risasi ya polisi na majambazi kumbe ni majirani waliojitolea kuuwa mbwa wale lakini wakashindwa mpaka pale askari maalum walipowasili ndio wakafanikiwa kuuwa wale mbwa huku kijana akiwa hoi....kila mtu alikuwa hoi na tukio hili....
Kweli hawa ni loaded gun! Walikuwa wanakwepa na risasi hao...masaa mawili mnakurupushana na mbwa kwa risasi!!!
 
Muzzle ipo [emoji23][emoji23][emoji23]
Umeishashindwa kumuhimiri...hiyo Muzzle unaifungaje!!?
=====
Ila uzi huu umenikumbusha tukio la utotoni...! Niliwahi kupewa zawadi ya mbwa mdogo na familia rafiki na yetu. Kalivyo kua kua nikawa na kaachia kambwa hako...! Kisha nikapata ushauri kuwa nikachanganyie nyigu/ dondola na nyuki kwenye chakula kawe kakali nikafanya hivyo kwa dozi ya wiki ya wadudu hao.

Siku moja tulienda shambani ( mbali kidogo na nyumbani) tukasahau kukafungia vizuri kwenye banda kambwa kangu hako, na jiikoni tuliegesha mlango ( waliowahi kukaa shamba watakuwa wananielewa). Jikoni tuliacha kiporo safi juu ya mafiga. Jua lilipokolea shambani nikaagizwa nikaandae mazingira ya mlo wa mchana siku hiyo. Kwa kuwa nilikuwa na njaa akili ikawa imegota kwenye kiporo wakati natoka shambani kurudi nyumbani.

Kufika nyumbani kwa mbali kidogo nikaona mlango wa jiko umepigwa chini! Nikajua kuna namna! Nikajihami, nikatafuta tawi la mti imara mkavu kutoka kwenye uzio hapo hapo nyumbani! Akili ikanituma nisipitie mlangoni nizunguke kwa kunyata kwenda kuchungulia ndani ya jiko kupitia kwenye matundu ama nikifanikiwa kwenye dirisha dogo nyuma ya jiko! Kufika, kwenye tundu la kwanza sikuona vizuri ndani lakini nikasia dalili zote za kiporo mafigani kushambuliwa na mbwa!! Nikajua watakuwa mbwa wa majirani! Kujiridhisha nikaenda kwenye dirisha dogo.

La haulah !!! Kuchungulia ndani ni kambwa kangu ndiyo kanakula kiporo!!! Kalivyoniona eti kakanguruma na kubweka! Nikapandwa na hasira! Nikazunguka kwa speed ili nije nikabananishe mlangoni!! Kufika mlangoni nikakakuta kamebeba kiporo katoroke nacho! Hasira zikazidi, nikanyanyua lile tawi la mti kukadunda...kulishusha kakakwepa huku nako eti kamefura kwa hasira... nikanyanyua tawi kwa mara nyingine kushusha kakajikinga na sufuria la kiporo huku kamejisogeza kwenye kona!!! Na sasa kakawa kametuna na kamefura hasa! Machale yakanicheza kuwa sasa...Niongeze tahadhari...Nikanyanyua tawi mara ya tatu kukasurubu!!

Halooh!!! Kambwa kakalirukia tawi lile juu kwa juu na kulidaka kakashuka nalo. Mbilinge ikaanza kunyang'anyana tawi...! Asikuongopee mtu, mpaka muda huu kihoro kimeishaniingia! Kambwa kakafanikiwa kuninyang'anya silaha!! Kakadhibiti tawi! Tukabaki tumeangaliana! Kwenye pembe nyingine ya jiko nikaona mchi wa kinu...Nikawa na vizia kuuchukua ! Aisee...! Mbwa yule, sasa siyo kambwa tena, akarukia kwenye pembe ya mchi wa kinu huku kabeba tawi alilonipora!

Mpaka hapo nikaona nilirudishe majeshi nyuma, nitoke humo jikoni! Kugeuza shingo, akanirukia na kunitupa chini! Akanitia meno kwenye mkono wa kushoto niliokuwa natumia kumshambulia! Kisha mbio akatokomea kwenye mashamba ya majirani ya karibu na nyumbani

Zilikuwa Dakika kama tano hivi za heka heka na mbwa yule niliyepewa zawadi, kumbuka siyo kambwa tena!

Nilipoona picha za mbwa huyu hatari kwenye uzi huu nikamkumbuka mbwa wa zawadi, naye alikuwa na masiko yaliyolala na mfupi ila alikuwa na mkia mrefu! Kwa hiyo, si dondola wala nyuki waliokuwa wamemuongezea uhatari mbwa wangu wa zawadi bali ni asili yake ya kiumbwa.

Niwatakie Jumapili njema.
 
Umeishashindwa kumuhimiri...hiyo Muzzle unaifungaje!!?
=====
Ila uzi huu umenikumbusha tukio la utotoni...! Niliwahi kupewa zawadi ya mbwa mdogo na familia rafiki na yetu. Kalivyo kua kua nikawa na kaachia kambwa hako...! Kisha nikapata ushauri kuwa nikachanyie nyigu/ dondola na nyuki kwenye chakula kawe kakali nikafanya hivyo kwa dozi ya wiki ya wadudu hao.

Siku moja tulienda shambani ( mbali kidogo na nyumbani) tukasaha kukafungia vizuri kwenye banda kambwa kangu hako, na jiikoni tuliegesha mlango ( waliowahi kukaa shamba watawanielewa). Jikoni tuliacha kiporo safi juu ya mafiga. Jua lilipokolea shambani nikaagizwa nikaandae mazingira ya mlo wa mchana siku hiyo. Kwa kuwa nilikuwa na njaa akili ikawa imegota kwenye kiporo wakati natoka shambani kurudi nyumbani.

Kufika nyumbani kwa mbali kidogo nikaona mlango wa jiko umepigwa chini! Nikajua kuna namna! Nikajihami, nikatafuta tawi la mti imara mkavu kutoka kwenye uzio hapo hapo nyumbani! Akili ikanituma nisipitie mlangoni nizunguke kwa kunyata kwenda kuchungulia ndani ya jiko kupitia kwenye matundu ama nikifanikiwa kwenye dirisha dogo nyuma ya jiko! Kufika, kwenye tundu la kwanza sikuona vizuri ndani lakini nikasia dalili zote za kiporo mafigani kushambuliwa na mbwa!! Nikajua watakuwa mbwa wa majirani! Kujiridhisha nikaenda kwenye dirisha dogo.

La haulah !!! Kuchungulia ndani ni kambwa kangu ndiyo kanakula kiporo!!! Kalivyoniona eti kakanguruma na kubweka! Nikapandwa na hasira! Nikazunguka kwa speed ili nije nikabananishe mlangoni!! Kufika mlangoni nikakakuta kamebeba kiporo katoroke nacho! Hasira zikazidi, nikanyanyua lile tawi la mti kukadunda...kulishusha kakakwepa huku nako eti kamefura kwa hasira... nikanyanyua tawi kwa mara nyingine kushusha kakajikinga na sufuria la kiporo huku kamejisogeza kwenye kona!!! Na sasa kakawa kametuna na kefura hasa! Machale yakanicheza kuwa sasa...Niongeze tahadhari...Nikanyanyua tawi mara ya tatu kukasurubu!!

Halooh!!! Kambwa kakalirukia tawi lile juu kwa juu na kulidaka kakashuka nalo. Mbilinge ikaanza kunyang'anyana tawi...! Asikuongopee mtu, mpaka muda huu kihoro kimeishaniingia! Kambwa kakafanikiwa kuninyang'anya silaha!! Kakadhibiti tawi! Tukabaki tumeangaliana! Kwenye pembe nyingine ya jiko nikaona mchi wa kinu...Nikawa na vizia kuuchukua ! Aisee...! Mbwa yule, sasa siyo kambwa tena, akarukia kwenye pembe ya mchi wa kinu huku kabeba tawi alilonipora!

Mpaka hapo nikaona nilirushe majeshi nyuma, nitoke humo jikoni! Kugeuza shingo, akanirukia na kunitupa chini! Akanitia meno kwenye mkono wa kushoto niliokuwa natumia kumshambulia! Kisha mbio kakatokomea kwenye mashamba ya majirani ya karibu na nyumbani

Zilikuwa Dakika kama tano hivi za heka heka na mbwa yule niliyepewa zawadi, kumbuka siyo kambwa tena!

Nilipoona picha za mbwa huyu hatari kwenye uzi huu nikamkumbuka mbwa wa zawadi, naye alikuwa na masiko yaliyolala na mfupi ila alikuwa na mkia mrefu! Kwa hiyo, si dondola wala nyuki waliokuwa wamemuongezea uhatari mbwa wangu wa zawadi bali ni asili yake ya kiumbwa.

Niwatakie Jumapili njema.
Muzzle ndiyo wanatumia ma Dr wao, pole sana kwahiyo ulikuwa unapigana na mfugo wako mwenyewe, haaa haaa kama nakuona unavyoruka ruka macho yamekutoka [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namfuga vizuri na anamiaka minne nilipomkuta kwa ndugu tukazoeana vizuri tu japo Kuna machache ambayo mtoa mada hajakosea

Wanawivu mno
Visasi vyao haviishi ,imagine mpk leo nasisitiza watu wasiache viatu nnje Mana anapenda kula Sana viatu vya kila Aina
-wanataka wapendwe Mana kila cku nikimfungulia usiku anataka nimkune tumboni.
-wanashambulia kwa kuua tu sio kwa kujeruhi ,ameua kanga watatu na kuku wengi akipata nafasi ya kuingia bandani anafanya mauaji co kujeruhi

Ni hayo tu kwa huyu mbwa wangu
 
Mbwa anaekula kuku nasemaa atawahi peponi mapema sanaa subamiit
 
Back
Top Bottom