Mbwana Makata awa kocha bora, awabwaga Hans van Pluijm na Goran Kopunovic

Mbwana Makata awa kocha bora, awabwaga Hans van Pluijm na Goran Kopunovic

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Kocha alieifundisha timu ya Tanzania Prisons kwa mechi 7 tu kwa msimu wa ligi wa 2014-2015 Mbwana Makata amechaguliwa kama kocha bora, akiwabwaga makocha wa yanga na simba Hans van Pluijm na Goran Kopunovic.

Shabani Kado amechaguliwa kipa bora wa msimu.

Simon Msuva amechaguliwa kama mchezaji bora wa msimu akiwabwaga akina Mrisho Ngassa na Mohammed Hussein "Tshabalala"
 
Sijawahi kuona uharo kama huu katika maisha yangu ya kupenda soka. Iweje kusiwe na professional hata mmoja kwenye tuzo hizi? hivi okwi Pascal wawa wanakosaje?
TFF na bodi ya ligi mmetepeta
 
Dah Tanzania kuna maajabu kwel duh mtu kafundisha mechi 7 kapewa kocha bora duh? Uhalal ulikuwa hv kocha bora hans na msuva mchezaji bora na kipa bora n barthez.

Na mm si mpenz wa yanga sijawah kuipenda yanga ila ukwel usemwe bwana hatuna tuwezalo hadi tunzo?

Na kipengele cha mchezaji bora tatu bora ilikuwa ni msuva, okwi na paschal wawa
 
tanzania bado sana kwa mtindo huu. ndo maana mpira umedumaa
 
Duh huyu Mbwana Makata sehemu kubwa ya msimu alikuwa kocha wa JKT Oljoro timu ya daraja la kwanza ameichukua prison mechi hazizidi tano ndio kocha bora kumshinda Kocha kama wa Yanga aliyeiongoza timu kuchukua ubingwa kwa soka safi na idadi kubwa ya magoli haki ya nani hii nchi mpira hautaendelea kamwe kama hawa wanaosimamia soka letu wataendelea kuwa madarakani.
 
Sijawahi kuona uharo kama huu katika maisha yangu ya kupenda soka. Iweje kusiwe na professional hata mmoja kwenye tuzo hizi? hivi okwi Pascal wawa wanakosaje?
TFF na bodi ya ligi mmetepeta

Nafikiri hizi tuzo ni kwa wachezaji wazawa tu,sidhani kama huyo Tshabalala alistahili kuwepo top 3.Kuna matatizo kwenye vigezo wanavyotumia kupata wachezaji/makocha bora hilo lilionekana hata kwa zile tuzo za mchezaji bora wa kila mwezi
 
Watanzania mnamajungu sana ***** zenu,hapa wange wachagua wachezaji wa kigeni mge piga kelele mpka bas,watanzania wengi ni mafala.!!
 
Mpira wetu wa bongo hauwezi endelea kwa vituko kama vinavyojitokeza, hivi iweje golikipa bora hata kwenye timu ya taifa hayumo? Wanatumia vigezo gani? Kocha bora anapewa alonusurika kushuka daraja,haya ni maajabu mengine ya Tz
 
Dah Tanzania kuna maajabu kwel duh mtu kafundisha mechi 7 kapewa kocha bora duh? Uhalal ulikuwa hv kocha bora hans na msuva mchezaji bora na kipa bora n barthez. Na mm si mpenz wa yanga sijawah kuipenda yanga ila ukwel usemwe bwana hatuna tuwezalo hadi tunzo? Na kipengele cha mchezaji bora tatu bora ilikuwa ni msuva, okwi na paschal wawa

Hapo kwa mchezaji bora, kwa Msuva ni sahihi kabisa. Kwa makocha kuna mushkeli kidogo

Hans kafundisha nusu msimu, kama ilivyo kwa Goran. Kama walitaka kocha bora labda angekuwa yule aliyemaliza msimu mzima. Kocha wa Yanga pamoja na kuibadilisha Yanga kiufundi na soka zuri lkn ameitoa katika nafasi ya 2 hadi ya kwanza. Kocha wa Simba kaitoa ktk nafasi ya 10 sijui hadi nafasi ya tatu. Wanatofautiana kidogo.
 
Sijawahi kuona uharo kama huu katika maisha yangu ya kupenda soka. Iweje kusiwe na professional hata mmoja kwenye tuzo hizi? hivi okwi Pascal wawa wanakosaje?
TFF na bodi ya ligi mmetepeta

Mkuu, kwani kwako profesheno ina maana mtu kutoka nje? Ngassa au Msuva hawawezi kuwa pros?
 
Dah Tanzania kuna maajabu kwel duh mtu kafundisha mechi 7 kapewa kocha bora duh? Uhalal ulikuwa hv kocha bora hans na msuva mchezaji bora na kipa bora n barthez.

Na mm si mpenz wa yanga sijawah kuipenda yanga ila ukwel usemwe bwana hatuna tuwezalo hadi tunzo?

Na kipengele cha mchezaji bora tatu bora ilikuwa ni msuva, okwi na paschal wawa

Mkuu hata huyo Barthez uliyempendekeza kadaka mechi kama 8 au 9 za mzunguko wa pili wa ligi, mzunguko wa kwanza wote Dida alisimama langoni.
 
Kwa Tanzania bado saana katika suala la Tunzo..kila mara wanabugi tuuu...hakuna kitu ambacho tunaweza kujivunia..kuanzia TFF mpaka serikali ya Maccm(upande wa michezo)
 
Kocha alieifundisha timu ya Tanzania Prisons kwa mechi 7 tu kwa msimu wa ligi wa 2014-2015 Mbwana Makata amechaguliwa kama kocha bora, akiwabwaga makocha wa yanga na simba Hans van Pluijm na Goran Kopunovic.

Shabani Kado amechaguliwa kipa bora wa msimu.

Simon Msuva amechaguliwa kama mchezaji bora wa msimu akiwabwaga akina Mrisho Ngassa na Mohammed Hussein "Tshabalala"
umefika wakati mamlaka za udhibiti (regulatory institutions) wa sanaa na michezo zidai and kujiridhidha kwanza vigezo vitavyotumika kwenye uteuzi wa tunzo mbalimbali nchini. Vigezo hivyo vielezwe waziwazi kwa watu wote ili hata pale uteuzi utapofanywa kwa kura za wadau, kila mdau atapiga kura yake kwa kuzingatia vigezo hivyo. Bila ya hivyo tutabaki kila siku tukilalamikia matokeo ya Kili Music Awards, Bongo Star Search, Wanamichezo Bora wa Mwaka, n.k.
 
Mkuu hata huyo Barthez uliyempendekeza kadaka mechi kama 8 au 9 za mzunguko wa pili wa ligi, mzunguko wa kwanza wote Dida alisimama langoni.

Barthez kadaka mechi zisizopungua 15, kwangu mimi ALISTAHILI TUZO ya kipa bora kuliko Shabani Kado.
Huyu Mbwana Makata anapataje tuzo ya kocha bora jamani? Dah
 
Barthez kadaka mechi zisizopungua 15, kwangu mimi ALISTAHILI TUZO ya kipa bora kuliko Shabani Kado.
Huyu Mbwana Makata anapataje tuzo ya kocha bora jamani? Dah

koroga sumu ufe,simba na yanga mnamatatizo..!!
 
Kumbe hili la Makata limeonwa na wengi, nilidhani peke yangu...

Hicho kigezo kilichotumika ni kigezo cha kipumbavu kuwahi kutokea...

Hao Prisons wenyewe wamebaki ligi kuu kwa kudra tu...

Hadi siku ya mwisho walikuwa wamekalia kuti kavu na ni upumbavu wa marefa waliochezesha mechi ya Stand Utd na Ruvu Shooting walioifanya Prisons ibaki ligi kuu...
 
Mbwana Makatta Kaifundisha Prison Mechi Nne tu na sio Saba jamani
 
Back
Top Bottom