Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za wakati wakuu,

Panda gari popote ulipo za kwenda Mbagala rangi tatu ukifika nenda mpaka round about ya Chamazi kunja kushoto tembea kidogo utaona shule ya msingi mbele kidogo utaona msikiti upande wa kulia kunja kulia utaona nyumba kama kigorofa kidogo hivi hapo utakuwa umefika kwa kina SAMATTA, Mtanzania wa kwanza kucheza premier league na kuweka rekodi mbalimbali.

Sasa lengo la mada hii ni kuwakumbusha vijana tunapopata hela au umaarufu kidogo tusiwasahau wapenzi wetu na watu waliotuvumilia tukiwa hatuna kitu.

Kipindi Samatta anataka kuoa alipishana na mzee wake kwani baba yake ni mtu wa dini sana vile vile wanasema jungu kuu halikosi ukoko hivyo anawajua wanawake vizuri sana. Samatta alishatambulisha wanawake wengi kwa lengo la kuwaoa akiwemo yule mzungu kipindi yupo TP MAZEMBE ila mzee wake alikataa na kumwambia awe makini kwani hilo suala sio la kukurupuka.

Basi bwana baada ya kuona mzee kila binti analeta pingamizi ikabidi amshirikishe mzee unataka nioe mwanamke wa aina gani kumbe mzee ana hesabu zake kitambo kuna mwanamke Samatta alizaa nae. Baada ya tafakuri ya mda mrefu ikabidi akubali maana mwanamke alizaa naye toka Samatta anatoka katika safari ya mpira japo hawakuwa karibu baada ya Samatta kuwa mbali kwa ajili ya mpira.

Basi kijana ikabidi akubali wazo la baba yake na kuvuta jiko tena bila matangazo wala promo walialikwa watu wachache tena wale wakaribu wengine waliishia kuona picha tu Instagram ila tayari tukio lishafanyika watu walitegemea bonge la harusi na matangazo kibao ila kwa Samatta haikuwa hivyo.

Na katika vitu ambavyo Samatta amefanikiwa ni kuwakwepa hawa maslay queen wa bongo. Angewaendekeza angekuwa kama mwenzake Hasheem Thabiti na wengine wengi waliopotea kwa kuendekeza mapenzi. BIG UP TO HIM!

NB: Wanaume tunapopata pesa wapenzi wetu wa zamani tuliowapata kabla hatuna kitu ndio wa kuoa kama unataka uwe kama Eboue basi endekeza ma slay queen.
 
Swala la kuoa oa mwanamke unayempenda full stop , kuchaguliwa mke believe me lazima utatoka nje tuuu....!! Atakuwa kama bortion tu home
Mkuu kutoka nje hakuna uhusiano na kuchaguliwa, kunbuka watu wengi miaka hii hawachaguliwi na ndio hao wachepukaji wakuu na wanaouana kwa wivu wa mapenzi.

Tatizo mnashindwa kutofautisha ushauri wa wakubwa na kuchaguliwa mke. Kwa mfano huo wa Samatta hapo hakuchaguliwa sababu baba yake aliwafahamu mademu wengi wa Samatta ila akashauri bora huyo alonae sasa.

Narudia tena kuchepuka hakuhusiani na kuchaguliwa.
 
Swala la kuoa oa mwanamke unayempenda full stop , kuchaguliwa mke believe me lazima utatoka nje tuuu....!! Atakuwa kama bortion tu home
Hapana mkuu tatizo wanawake wengi ukiwa na hela wanakuwa na tamaa na wanaweza wakafanya chochote ili wapate hela refer to,

Didier Drogba
Emanuel eboue
Na mchezaji mmoja wa nigeri nimemsahau jina.

Mwanamke usipokuwa na hela atachepuka na mwenye hela na ukiwa na hela anawaza atakumaliza vipi ili awe na uhuru wakuzitumia peke yake refer,

Jacqueline mengi
Mke wa msuya
Mbagala rangi tatu kuna jamaa ana maduka makubwa ya jumla aliponea chupu chupu kufa baada ya mke wake kumewekea sumu.

Hata diamond anaogopa kuoa kwasababu hyo anaogopa ma gold digger.
 
Romy Jones alisema kitu poa sana alipohojiwa na salama "mshamba ni ngumu sana kukutana na madawa ila watoto wa mjini ndio kugusa maana wanajaribu kila aina ya ujanja".

RAY C alisema kilichomuangusha kikubwa ni watu waliomzunguka na hakumsikiliza hata mama yake alipokuwa hot na pale alipomkataa lord eyes ambaye alichangia anguko lake

Samatta kaweza kiasi flani kucontrol vitu vyote viwili. Mungu ampiganie asee
 
Back
Top Bottom