Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

Habari za wakati wakuu,

Panda gari popote ulipo za kwenda Mbagala rangi tatu ukifika nenda mpaka round about ya Chamazi kunja kushoto tembea kidogo utaona shule ya msingi mbele kidogo utaona msikiti upande wa kulia kunja kulia utaona nyumba kama kigorofa kidogo hivi hapo utakuwa umefika kwa kina SAMATTA, Mtanzania wa kwanza kucheza premier league na kuweka rekodi mbalimbali.

Sasa lengo la mada hii ni kuwakumbusha vijana tunapopata hela au umaarufu kidogo tusiwasahau wapenzi wetu na watu waliotuvumilia tukiwa hatuna kitu.

Kipindi Samatta anataka kuoa alipishana na mzee wake kwani baba yake ni mtu wa dini sana vile vile wanasema jungu kuu halikosi ukoko hivyo anawajua wanawake vizuri sana. Samatta alishatambulisha wanawake wengi kwa lengo la kuwaoa akiwemo yule mzungu kipindi yupo TP MAZEMBE ila mzee wake alikataa na kumwambia awe makini kwani hilo suala sio la kukurupuka.

Basi bwana baada ya kuona mzee kila binti analeta pingamizi ikabidi amshirikishe mzee unataka nioe mwanamke wa aina gani kumbe mzee ana hesabu zake kitambo kuna mwanamke Samatta alizaa nae. Baada ya tafakuri ya mda mrefu ikabidi akubali maana mwanamke alizaa naye toka Samatta anatoka katika safari ya mpira japo hawakuwa karibu baada ya Samatta kuwa mbali kwa ajili ya mpira.

Basi kijana ikabidi akubali wazo la baba yake na kuvuta jiko tena bila matangazo wala promo walialikwa watu wachache tena wale wakaribu wengine waliishia kuona picha tu Instagram ila tayari tukio lishafanyika watu walitegemea bonge la harusi na matangazo kibao ila kwa Samatta haikuwa hivyo.

Na katika vitu ambavyo Samatta amefanikiwa ni kuwakwepa hawa maslay queen wa bongo. Angewaendekeza angekuwa kama mwenzake Hasheem Thabiti na wengine wengi waliopotea kwa kuendekeza mapenzi. BIG UP TO HIM!

NB: Wanaume tunapopata pesa wapenzi wetu wa zamani tuliowapata kabla hatuna kitu ndio wa kuoa kama unataka uwe kama Eboue basi endekeza ma slay queen.
Dingi kaona mbali, ukiwa star na pesa mingi, utapendwa kwa ajili ya kitu na sio kwa ajili ya utu na mapenz.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Huwa tunafeli saana hapo kwenye ndoa, utataka mwanamke wa kugongwa uoe,hiyo shida,wazee wa zamani walifaulu kwa kuchaguliana wake,ila siku hizi utandawazi tunaokota okota tu, ndio tunaokota majini yanatunyonya damu.

[emoji3][emoji3]
 
Mleta mada unatania aisee, Yani nikamate Hela ya maana halafu naanzaje kuwaacha hawa ma slay queen wa Bongo? Lazima nitembeze rungu mpaka watafutane.
 
akija likizo huwa anajifungia kwake kule kijichi. anacheza playstation na kufanya warm up mida ya alfajiri na washkaji zake wa kitaa.

huwezi kumuona anazurula kidimbwi, juliana au element na machawa/wadada wa mujini. samata is a very humble guy. hana makuu japo pesa anayo.
 
Hapana mkuu tatizo wanawake wengi ukiwa na hela wanakuwa na tamaa na wanaweza wakafanya chochote ili wapate hela refer to,

Didier Drogba
Emanuel eboue
Na mchezaji mmoja wa nigeri nimemsahau jina.

Mwanamke usipokuwa na hela atachepuka na mwenye hela na ukiwa na hela anawaza atakumaliza vipi ili awe na uhuru wakuzitumia peke yake refer,

Jacqueline mengi
Mke wa msuya
Mbagala rangi tatu kuna jamaa ana maduka makubwa ya jumla aliponea chupu chupu kufa baada ya mke wake kumewekea sumu.

Hata diamond anaogopa kuoa kwasababu hyo anaogopa ma gold digger.
Mmmh ni nondo ila kwa Msuya sidhani kama una uhakika.!
 
Back
Top Bottom