Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

Mbwana Samatta alivyoruka viunzi vya Wadada wa Bongo na Wazungu

Kosa la baba liko wapi hapo?
Basi bwana baada ya kuona mzee kila binti analeta pingamizi ikabidi amshirikishe mzee unataka nioe mwanamke wa aina gani kumbe mzee ana hesabu zake kitambo kuna mwanamke Samatta alizaa nae. Baada ya tafakuri ya mda mrefu ikabidi akubali maana mwanamke alizaa naye toka Samatta anatoka katika safari ya mpira japo hawakuwa karibu baada ya Samatta kuwa mbali kwa ajili ya mpira.
👆🏽
 
Habari za wakati wakuu,

Panda gari popote ulipo za kwenda Mbagala rangi tatu ukifika nenda mpaka round about ya Chamazi kunja kushoto tembea kidogo utaona shule ya msingi mbele kidogo utaona msikiti upande wa kulia kunja kulia utaona nyumba kama kigorofa kidogo hivi hapo utakuwa umefika kwa kina SAMATTA, Mtanzania wa kwanza kucheza premier league na kuweka rekodi mbalimbali.

Sasa lengo la mada hii ni kuwakumbusha vijana tunapopata hela au umaarufu kidogo tusiwasahau wapenzi wetu na watu waliotuvumilia tukiwa hatuna kitu.

Kipindi Samatta anataka kuoa alipishana na mzee wake kwani baba yake ni mtu wa dini sana vile vile wanasema jungu kuu halikosi ukoko hivyo anawajua wanawake vizuri sana. Samatta alishatambulisha wanawake wengi kwa lengo la kuwaoa akiwemo yule mzungu kipindi yupo TP MAZEMBE ila mzee wake alikataa na kumwambia awe makini kwani hilo suala sio la kukurupuka.

Basi bwana baada ya kuona mzee kila binti analeta pingamizi ikabidi amshirikishe mzee unataka nioe mwanamke wa aina gani kumbe mzee ana hesabu zake kitambo kuna mwanamke Samatta alizaa nae. Baada ya tafakuri ya mda mrefu ikabidi akubali maana mwanamke alizaa naye toka Samatta anatoka katika safari ya mpira japo hawakuwa karibu baada ya Samatta kuwa mbali kwa ajili ya mpira.

Basi kijana ikabidi akubali wazo la baba yake na kuvuta jiko tena bila matangazo wala promo walialikwa watu wachache tena wale wakaribu wengine waliishia kuona picha tu Instagram ila tayari tukio lishafanyika watu walitegemea bonge la harusi na matangazo kibao ila kwa Samatta haikuwa hivyo.

Na katika vitu ambavyo Samatta amefanikiwa ni kuwakwepa hawa maslay queen wa bongo. Angewaendekeza angekuwa kama mwenzake Hasheem Thabiti na wengine wengi waliopotea kwa kuendekeza mapenzi. BIG UP TO HIM!

NB: Wanaume tunapopata pesa wapenzi wetu wa zamani tuliowapata kabla hatuna kitu ndio wa kuoa kama unataka uwe kama Eboue basi endekeza ma slay queen.
Wewe jamaa upo kumbe bado
 
Ee mungu nisaidie kuna pisi kali virginometer imetembea mile nyingi balaa inataka kutua kontena kwangu na ndio muda mafanikio yanabisha hodi.
amina
 
Ee mungu nisaidie kuna pisi kali virginometer imetembea mile nyingi balaa inataka kutua kontena kwangu na ndio muda mafanikio yanabisha hodi.
amina
Anakuja kula mafao.
Ukiona pisi kali zinakuzengea una harufu ya mafanikio hao wako kama tai wale wala mizogo hunusa mzoga toka mbali yaani
 
Mimi nikiwa star aiseeh kuoa kutasubiri sana.. nitakula watoto hao wa insta na bongo movie kama nini
😁😁 achana na hao waigizaji hata sio wakali! Kuna vile vi dem vinapostigi clips wanaimba nyimbo za ma star daah! Wanakuwaga wakali balaa
 
Kumbe lisammata Na bichwa kubwa lile la kufungia magoli haliwezi kujiamulia mke wa Kuoa?
 
Back
Top Bottom