Mbwana Samatta avunja rekodi kedekede

Mbwana Samatta avunja rekodi kedekede

Dada yangu naomba utofautishe kati ya kuvunja rekodi na kuweka rekodi.
Mie naona Samatta ameweka rekodi.

Kuvunja rekodi maana yake lazima kuna mtu aliweka rekodi fulani halafu mwingine akaizidi ile ambayo iliwekwa awali.
Mfano kwenye riadha tunaona kwamba mwanariadha fulani alikimbia mfano mita 100 kwa sekunde 15 hiyo ameweka rekodi. Mwingine akaja akakimbia mita hizo kwa sekunde 10. Huyo aliyekimbia ndio kavunja rekodi na pia kaweka rekodi mpya.

Sasa naomba unieleze Samatta alipovunja rekodi ni wapi zaidi ya kuweka rekodi?

Kwa mtazamo wangu Samatta hajavunja rekodi bali ameweka rekodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaharibu uzi sasa hivi.

Samatta ni kijana wa mfano kwanza hana maringo na mstaarabu sana ukitaka kuthibitisha angalia pesa anayolipwa na maisha anayoishi....pia angalia lile sakata alivyokua anashambuluwa na sisi watanzania kwa kucheza vibaya timu ya taifa angalia jinsi alivyojibu jwa utulivu na upole.

Sent using Jamii Forums mobile app
We kwani unfikiri point ya mleta mada ilikuwa ni nini? au we ni mgeni hapa jamvini?
 
Mechi za Aston Villa za EPL zijazo,

Villa vs Spurs
Southampton vs Villa
Leicester vs Villa
Villa vs Chelsea
Newcastle vs Villa
Villa vs Wolves
Liverpool vs Villa
Villa vs Manchester utd
Villa vs Palace
Everton vs Villa
Villa vs Arsenal
Westham vs Villa,

Hapa Aston villa lazima wakaze,mechi ni ngumu,Samatta apige kazi ili hata kama Villa itashuka Championship,yeye asajiliwe na team nyingine inayoshiriki EPL,

Good luck MBWANA SAMATTA,
Good luck ASTON VILLA.
Kweli hizi gemu ni ngumu sana
 
Bibi usiwe mbishi, kasikilize mahojiano ya Kikwete na Salim Kikeke kupitia youtube wakati akiwa rais. Kasema wazi kabisa kuwa yeye ni shabiki wa newcastle. Hiyo spurs alikwambia wapi?
 
Bibi usiwe mbishi, kasikilize mahojiano ya Kikwete na Salim Kikeke kupitia youtube wakati akiwa rais. Kasema wazi kabisa kuwa yeye ni shabiki wa newcastle. Hiyo spurs alikwambia wapi?
Kabadili Tu. Hata Mimi kuna wakati nilikuwa shabiki wa Arsenal lakini nikahamia kuishabikia Liverpool kwa ajili ya Mohamed Salah na sasa pia naishabikia Aston Villa kwamahili ya Mbwana Samatta.

Upo hapo ulipo.

Na hayo ni kwa ajili ya Waislam wenzangu. Kumbuka hilo.
 
Back
Top Bottom