Mbwana Samatta avunja rekodi kedekede

Mbwana Samatta avunja rekodi kedekede

Ma Shaa Allah.

Kijana wetu amevunja rekodi zifatazo mpaka sasa...

1) Mtanzania wa kwanza kucheza Premier League ya Uingereza.

2) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la Premier League.

3) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la Premier League kwenye mechi ya kwanza.

4) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la kichwa la kwanza la Aston Villa toka msimuu huu uanze.

5) Mchezaji wa kwanza kupanda thamani ndani ya Premier League msimu huu ndani ya mechi mbili tu.

Ongezea...

Samatta anatarajiwa kucheza tena tarehe 16-02-2019 wakati timu take itapopambana na Tottenham (timu ya Uingereza anayoshabikia Kikwete).

Tumuombee dua njema kijana wetu, anatupeperushia bendera yetu ya Tanzania vizuri kabisa huko Uingereza.

Allah amuondolee na amuepushe na hassad zote. Amiiin.
16-02-2019[emoji777]
16-02-2020[emoji818]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binadamu ni kama toy tu empty CD. Ukiliwahi ukalichomeka itikadi zako mwenyewe tu unazojua, utaliendesha kama roboti.
 
Utaharibu uzi sasa hivi.

Samatta ni kijana wa mfano kwanza hana maringo na mstaarabu sana ukitaka kuthibitisha angalia pesa anayolipwa na maisha anayoishi....pia angalia lile sakata alivyokua anashambuluwa na sisi watanzania kwa kucheza vibaya timu ya taifa angalia jinsi alivyojibu jwa utulivu na upole.

Sent using Jamii Forums mobile app

Maadili


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kikwete ni shabiki wa NewCastle United, na sio Tottenham kama unavyosema. Kuna kipindi alienda UK na wakati huo PM wa UK ni Tony Blair, alimpa hadi Jersey ya Newcastle United,yenye jina la Kikwete@FaizaFoxy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo (yupo) aliye/waliokwisha cheza ligi zingine za Ulaya, hata yeye mwenyewe kishacheza ligi nyingine Ulaya.

Hapa amevunja rekodi na ndiyo kaweka hiyo rekodi mpya. Huwa sikisii.
Acha ubishi bibi. Samatta rekodi hajavunja bali ameweka.
 
Utaharibu uzi sasa hivi.

Samatta ni kijana wa mfano kwanza hana maringo na mstaarabu sana ukitaka kuthibitisha angalia pesa anayolipwa na maisha anayoishi....pia angalia lile sakata alivyokua anashambuluwa na sisi watanzania kwa kucheza vibaya timu ya taifa angalia jinsi alivyojibu jwa utulivu na upole.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona analopwa pesa ya kawaida sana
 
Back
Top Bottom