Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Io paragraph yako ya mwisho inakufunga tena. Kazi ya striker ni kufunga no matter kafungia shingo, kichwa, au mkonoo. .

Refer to chicharito

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama kafungia tako au gegedo ili mradi kafunga kwani ndio kazi yake.

Huyu mleta mada usikute hana hata ujuzi wa mpira zaidi tu ya kuwa mnywa kahawa wa magemgeni

Aache uchawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mleta Uzi umeamua kutupima mahaba yetu kwa Samata anyway baada ya kusoma nyuzi kadhaa nimepoa nimeona kwanza nihoji dhamira yako mwandishi.
Striker unataka afunge kwa kuremba kivipi? Lukaku kuna kipi anachofunga kwa kuremba,Je unadhani kufunga ni rahisi kama unafunga kamba ya viatu? Hao wanaocheza ulaya unasema wanafunga eti kwa uzuri,unamjua Benteke we mpira wote anacheza ulaya mpaka match ya Jana nadhani ni game ya 17 hajafunga goal lolote. Usiwe na motive za kudemoralize wenzio kwa husuda zako kazi ya kucheza ligi kubwa kama uingereza sio kazi rahisi so kwa samata huko alipo ni sehemu sahihi sema anatakiwa ajaribu kujitahidi zaidi japo anaweza akajitahidi na asipate nafasi ya kuja kucheza EPL maama EPL sio lele mama Leo hii tunaona wachezaji tena wazawa wa England kama kina Calton Cole,Jermain Jena's,Penant pamoja nakuzaliwa mpira ulikoanzia wakashindwa kutamba hapo EPL wakajaishia kucheza India premier league.

Hivyo nakushauri usimlete mifano kijana wetu kwa kumkatisha tamaa eti kwa kisingizio cha huvutiwi na ufungaji wake. Samatta sio Bergkamp,Messi wala Ronaldo De Lima ambao walikuwa wakali wa sexy goals.

Wacha azidi kucheza kadri Mungu atakavyombariki kwani kipimo cha kucheza kwa kiwango sio kucheza EPL yuko wapi Saido Berahino? Jana nilikuwa naangalia Betis Vs Sevila ndio nikajua why William Cavalho ameshindwa pata timu England so usimnange Samata hata alipo panamfaa zaidi aongeze juhudi kidogo apate team zenye Mshahara mkubwa ili aje astaafu vizuri na maisha yake na wanaomtegemea yawe ya raha. Hiyo Bar ya Samatta aje EPL ndio uridhike ni mfano wa kusadikika Handicap ziko nyingi sana kwa samatta ukianzia Historia yetu kimpira so uwezo wake ndio umedefy hata hicho kigezo ndiomaana mpaka tunamuona Europa angekuwa mchovu usingemuona kikosini wazungu hawaangalii bahati.
 
sijadis mkuu...ukisoma uzi vizuri utagundua kuwa niliousema ni ukweli mtupu...labda tatizo lako ni kuwa huangalii mechi za Genk live sansana unaangalia updates na clips kwa akina Shaffii Dauda na Millard Ayo!.... Jaribu kuangalia mechi za KRC Genk utarudi kunipa tawile!
Krc genk inaonekana channel gan maana mi natumia dstv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.
Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.
Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).
Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.
Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.
huku kumponda Samatta mbona sasa?
au kwa vile amewa diss watu kuwa "Dar iitwe Kolomije"?
 
Naona mtoa mleta Uzi umeamua kutupima mahaba yetu kwa Sammata anyway baada ya kusoma nyuzi kadhaa nimepoa nimeona kwanza nihoji dhamira yako mwandishi.
Striker unataka afunge kwa kuremba kivipi? Lukaku kuna kipi anachofunga kwa kuremba,Je unadhani kufunga ni rahisi kama unafunga kamba ya viatu? Hao wanaocheza ulaya unasema wanafunga eti kwa uzuri,unamjua Benteke we mpira wote anacheza ulaya mpaka match ya Jana nadhani ni game ya 17 hajafunga goal lolote. Usiwe na motive za kudemoralize wenzio kwa husuda zako kazi ya kucheza ligi kubwa kama uingereza sio kazi rahisi so kwa samatta huko sehemu sahihi sema anatakiwa ajaribu kujitahidi zaidi japo anaweza akajitahidi na asipate nafasi ya kuja kucheza EPL maama EPL sio lele mama Leo hii tunaona wachezaji tena wazawa wa England kama kina Calton Cole,Jermain Jena's,Penant pamoja nakuzaliwa mpira ulikoanzia wakashindwa kutamba hapo EPL wakajaishia kucheza India premier league.

Hivyo nakushauri usimlete mifano kijana wetu kwa kumtisha tamaa eti kwa kisingizio cha huvutiwi na ufungaji wake. Samatta sio Bergkamp,Messi wala Ronaldo De Lima ambao walikuwa wakali wa sexy goals.

Wacha azidi kucheza kadri Mungu atakavyombariki kwani kipimo cha kucheza kwa kiwango sio kucheza EPL yuko wapi Saido Berahino? Jana nilikuwa naangalia Betis Vs Sevila ndio nikajua why William Cavalho ameshindwa pata timu England so usimnange Samatta hata alipo panamfaa zaidi aongeze juhudi kidogo apate team zenye Mshahara mkubwa ili aje astaafu vizuri na maisha yake na wanaomtegemea yawe ya raha. Hiyo Bar ya Samatta aje EPL ndio uridhike ni mfano wa kusadikika Handicap ziko nyingi sana kwa samatta ukianzia Historia yetu kimpira so uwezo wake ndio umedefy hata hicho kigezo ndiomaana mpaka tunamuona Europa angekuwa mchovu usingemuona kikosini wazungu hawaangalii bahati.
umecomplicate sana kaka....Kama umeweza kukiri ya kwamba wapo washambuliaji kama akina Lukaku na Benteke ambao hawafungi magoli mara kwa mara hasa Benteke aliyekaa mechi 17. Je unadhani ni kwanini wachezaji hao uliowataja hapo juu hawafungi mara kwa mara au wanafunga magoli ya kawaida? Tunarudi kwenye sababu ileile ya ukawaida na ubutu wa mchezaji kwani hata hao akina Lukaku na Benteke kinachoonekana nao pia wana bahati ya kuwepo hapo walipo kwani wapo wachezaji wazuri pengine wa kumudu nafasi zao ila hawajapewa nafasi...so, ukiona mchezaji ana kiwango cha kawaida na bado anaendelea kuaminiwa ujue huyo ana bahati kubwa sana........kuhusu Samatta Usilete ubishi maana nina uhakika huangaliagi Mechi za Genk, zaidi ya kusikia matokeo ya vijiweni na viclip kwenye page za akina Shafii Dauda na Millard Ayo!
 
huku kumponda Samatta mbona sasa?
au kwa vile amewa diss watu kuwa "Dar iitwe Kolomije"?
Tunajaribu kuusema ukweli...japo vijana wanaleta ushabiki badala ya facts
 
Watu wasiojua mpira hoja zao za hovyo sana. Mkuu jua tu kuwa kuna aina tofauti tofauti za wachezaji. Kuna strikers ambo wao wanaitwa 'target man' na 'goal poachers' yani hao utawaona wakitupia kambani tu wala hutakaa uwaone wakilamba mabeki vyenga labda kwa nadra sana.

Wapo ma player wakubwa na majina yao waliokuwa hivyo na wakawa ma legend katika soka mfano Ruud Van Nestleroy. Huwezi kumfananisha na De Lima kiuchezaji lakini wote ni ma striker walikuwa wanatupia day in day out.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wasiojua mpira hoja zao za hovyo sana. Mkuu jua tu kuwa kuna aina tofauti tofauti za wachezaji. Kuna strikers ambo wao wanaitwa 'target man' na 'goal poachers' yani hao utawaona wakitupia kambani tu wala hutakaa uwaone wakilamba mabeki vyenga labda kwa nadra sana.

Wapo ma player wakubwa na majina yao waliokuwa hivyo na wakawa ma legend katika soka mfano Ruud Van Nestleroy. Huwezi kumfananisha na De Lima kiuchezaji lakini wote ni ma striker walikuwa wanatupia day in day out.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona kama umetoka nje ya mada....Au hujastuka? soma tena uzi vizuri halafu ndio ucomment
 
Mleta Uzi ambae unajipambanua kama mfuatiliaji wa match za Samatta me nakuja kukujibu na vitu live maana hiyo Genk wote tunaiangalia na kama kweli unaifuatilia Genk utakuwa ulikuwa unamfahamu Niko Kalleris ambae yeye ndio alikuwa anagombea namba na Samatta amehama msimu huu kaenda PAOK anako kaa benchi,mchezaji mwingine alikuwa akicheza cheza kipindi Samatta yuko bench ni Puzuelo mspain huyu na hao wote nawengine wengi Samatta kawakalisha katika list ya wachezaji waliowahi kucheza Genk na kufunga magoli mengi.Samatta anamagoli mengi kuliko Kevin De Bruyne na Benteke kwa kipindi walichocheza Genk ifuatayo ni jedwali la vielelezo ili ujue why wazungu wanaimba Samagoal.

View attachment 855948View attachment 855951
Screenshot_20180903-201424.jpg
View attachment 855950
 
Aisee!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mwisho mkuu naona katika Uzi wako ukiletewa hoja unakuja kwa kupaniki na kauli za kejeli,ningeweza kuwa aggressive na kauli mbovu kama wengi walivyokuita majina ya kila aina ila naona unapoona wengine tumekujibu kwa hoja unakuja na kauli za kimama ukijiaminisha we ndio unajua kila kitu wengine tunaangalia vijiclip bila kujiridhisha ubora wa MTU ambae humfahamu. Nakushauri tu kama kijana mwenzangu stick kwenye hoja na jibu hoja kwa hoja maneno ya kejeli hayakujengei kuonekana we unauhalali wa kujua kila ulichokileta katika Uzi wako. Jifunze utu hata kwa usiyemjua.
 
wee nawe sio mzima...so kila anayetoa analysis ya mpira ajibiwe hivyo? Kwamba positive views ni sawa ila negative ni kosa?...acha ushamba mdau!
Wewe ndiyo mshamba.

Humud ndiye mchezaji tunayeweza kumuita ana bahati siyo Samata.
 
Back
Top Bottom