Mbwembwe gani ulianza nazo mwaka??

Mbwembwe gani ulianza nazo mwaka??

Mwaka ulivyoanza watu huwa wanajitahidi kubadili tabia ama kujaribu kufanya mambo mapya kwa mbwembwe za kila aina lakini kadri mda unavyoenda anajikuta kasharudi kwenye hali yake ya kawaida (default settings)

Mimi nilianza na jogging kwa mbwembwe zote,nilijitahidi niwe nakunywa siku za wkend tu,nilianza kusoma vitabu pia lakini kadri mda unavyoenda naona nisharudi kwenye settings zangu za zamani

Wewe ulianza na mbwembwe gani?

Hahaha nimekumbuka pia nilianza na mbwembwe za kujifanya nakula mboga mboga na matunda ila naona nisharudi kwenye hali ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivo ulivyo vianza ni vizuri kwa afya yako ulazimishe mwili uzoee iwe kawaida yako, mm nishauzoesha mwili wangu kunywa maji mengi, mbogamboga yaan hvyo don't miss nashazoea na matunda japo si mara mara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufanya mazoezi.kusoma E-Books na meditation mkuu " mnamo mwezi wa 11 mwaka jana baada ya kusikia mawaidha katika station ya radio fulani hivi online ...

Basi nikajikuta na hamasika sana kufanya hivyo vitu tajwa hapo kwenye Aya ya kwanza "....

Basi haraka harak bila ya kuchelewa ni kakaa chini na ku-create upya ratiba yangu " Ambayo ilikuwa inanilazimu kuamka saa 9:40 usiku "....... nikawa natekeleza hivyo vyote kwa kufuata mtiriliko wa ratiba " kisha baada ya hapo ndio najiandaa kwenda katika pilika zangu za kila siku ....

Mmh --, bahati mbaya ni kwamba sasa hivi nina week ya pili nimeshindwa kudumu katika program yangu "

Roho inaniuma

Sent using Jamii Forums mobile app
Rudi ujachelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilipanga huu mwaka ukianza tu nianze na ibada bahati mbaya hata kuanza sijaanza daah..

ila huu mwaka hautaisha wallah...Allah anisimamie katika hilo
 
Mimi nilianza na mbwembwe za kufa mtu kusoma vitabu kila siku kuamka mapema ,kupiga zoezi la kukata tumbo, kufanya meditation, ila cjui nimepotelea wapi maana nachapa ucngizi na mazoezi nimeacha hahah na novel yangu nimeishia katikati hahaha lkn nimegundua aya mambo lazima uwe na self discipline, commitment,passion and sucrifice lasivyo utaona mzigo na kuachia njiani nimegundua kabla hujaanza Fanya kitu hakikisha unakipenda and you enjoy it.....

am better here
 
Nilipanga nisome vitabu kama kumi, Nipo cha kwanza page ya tatu.
Nilipanga niache bia, nimeweza, though nahisi ntaanza kunywa very soon.
Mazoezi, nimeweza.
Nilipanga nisikilize podcast flani flani kama part ya personal development, naona Tetema imetawala kwenye playlist.
Ila kuna mengi tu, nimeweza, I am proud of myself.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom