MC acheni kuposti video za harusi na sendoff bila idhini

MC acheni kuposti video za harusi na sendoff bila idhini

Nyingine ni ushubwada 😂😂 kuna moja niliona, bwana harusi mtarajiwa anacheza, yan kwa kifupi sio furaha, ni aliranduka 🤣🤣
Nikasema ningekuwa mimi ndo bi. harusi, hakii namfinya kidogo ndo atulie
Ukute alionja kidogo kukata aibu 🤣
 
Hii inajitokeza zaidi katika siku za karibuni kutokana na maendeleo makubwa ya mtandao. Unakuta Kuna kipande fulani kinachukuliwa na mc katika video ya shughuli bwana Harusi na Bibi Harusi mnajikuta ghafla mnatrend mtandao iwe Ni kwa kituko au kwa uzuri.

Madhara yake kwa wahusika
Inaweza kusababisha msongo wa mawazo au kukuharibia heshima yako pahaka fulani.

MC kuweni makini na kazi zenu na usirushe maudhui katika kitandazi chako bila idhini ya wahusika.
Maxence Melo ndio mjumbe wa bodi ya faragha ya taarifa,alishatoa angalizo kwamba kuna mtu anaweza kushtakiwa na kudaiwa fidia kwa kutoa taarifa zake bila idhini
 
Tatizo Watanzania tumeshazoea kufanya mambo kienyeji. Yani mtu unamtafuta tu MC unampa hela aje kufanya shughuli yako bila hata mkataba wenye terms zako ambao atau sign mkishakubaliana.

Muwe mnawasainisha mkataba hao Ma MC ili ikitokea akikiuka terms za mkataba umshtaki akulipe damages.
 
Back
Top Bottom