MC acheni kuposti video za harusi na sendoff bila idhini

Nyingine ni ushubwada 😂😂 kuna moja niliona, bwana harusi mtarajiwa anacheza, yan kwa kifupi sio furaha, ni aliranduka 🤣🤣
Nikasema ningekuwa mimi ndo bi. harusi, hakii namfinya kidogo ndo atulie
Ukute alionja kidogo kukata aibu 🤣
 
Maxence Melo ndio mjumbe wa bodi ya faragha ya taarifa,alishatoa angalizo kwamba kuna mtu anaweza kushtakiwa na kudaiwa fidia kwa kutoa taarifa zake bila idhini
 
Clip inarekodiwa vizuri ila baada ya muda kakipande ka sekunde thelathini kanaenda kuwa kibwagizo huko TikTok na kuingiziwa sauti za vituko. Ukitaka u-rasmi funga harusi yako kwa mkuu wa mkoa period
Naam
 
Tatizo Watanzania tumeshazoea kufanya mambo kienyeji. Yani mtu unamtafuta tu MC unampa hela aje kufanya shughuli yako bila hata mkataba wenye terms zako ambao atau sign mkishakubaliana.

Muwe mnawasainisha mkataba hao Ma MC ili ikitokea akikiuka terms za mkataba umshtaki akulipe damages.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…