Udini,ukabila upo sana kwenye kutoa ajira sekta binafsi na utumishi wa umma,
Mkurugenzi wa taasisi ya umma akiwa Mkristo,muhaya,mchaga,Msukuma,hapo tegemea watu kutoka hiyo dini au kabila kupewa upendeleo.
Nchi hii ajira zinauzwa,Wala sio Swala la kufikirika,tribalism,nepotism,imeenea kila Kona.
Nchi ina makabila zaidi ya 120+,harafu ukute utumishi wa umma na nafasi za wakurugenzi Zimeshikwa na watu kutoka jamii mbili au tatu tu, unakuta asilimia 65 ya utumishi wa umma ni makabila mawili au matatu harafu makabila 118 yameachwa yapambanie asilimia 35tu !!!
Hiyo sio Sawa,tatizo la nchi hii na ccm hawana road map Wala vision,Hilo swala la kuuliza watumishi wa umma dini na kabila zao,sio kwamba wanataka kuboresha au kuleta usawa,hapa wanataka kuondoa wale wengi,waongeze wale waliokuwa wachache,
Wala sio kutafuta suruhisho la kudumu,Cha msingi wangepitia CV za watu kuona walifikaje hapo walipo,na wangeweka uwazi kwenye ajira za serikalini,waweke mfumo unaofanya kazi.