Nimekuwa mfatiliaji mzuri sana wa hawa wasanii wetu wa stand up comedy kwa mda mrefu lakini bado naona mambo si mazuri tofauti na kwa wenzetu wa Kenya. Mc PiliPili naona akijitutumua lakini sanaa yake bado holaa, kakosa ubunifu wa kutosha na kusababisha kuishia tu kwenye Maharusi.
Me nahisi imefika wakati ajifunze kwa wenzake akina Eric Omondi, Prof. Hamo Kansiime anne, Mc jessey na wengine wengi ili alete vitu vizuri. Lakini kingine akubali kuwa na management yenye watu wanaoweza kumsaidia kuwa mbunifu zaidi kwenye Sanaa ya uchekeshaji.