Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Wenye vipaji vyao, hawana hela ya kujipromoti.
Wenye hela hawana vipaji, ila wanaweza kujipromoti.

Hii ndio dunia bwana.
 
Huyu jamaa ni bingwa wa misemo ya kigogo ila tatizo alilonalo ni kukosa ubunifu. Kila siku anatumia mada zile zile. Angekuwa anatafuta na kubuni mambo mapya angefanikiwa sana. Yeye kila siku "mahindi mahindi"
 
msema kweli ni mpenzi wa Mungu...naungana na mleta uzi, hata mimi sijawahi kuguswa na uchekeshaji wake hata kidogo...in fact bora aangalie kitu kingine cha kufanya.
Hii gemu awaachie kina Mkali wenu,Maufundi na wengineo...
Idris ndiyo hajui kabisaaaaa....

NB:tuache kufosi mambo, kama kuspesholaizi na kitu angalia pale ambapo utaweza fanya bora zaidi...na hii ni imani yangu kuwa kila mtu anacho kitu(vitu) ambacho ana uwezo wa kukifanya kwa namna iliyo bora zaidi kuliko wengine...jitahidi kukigundua upige hela.
 

Nami nakuunga mkono!binafsi sichekeshwi na comedy anayofanya kaka Mc pilipili.
 
Kuna siku nilimuona TBC anaojiwa na yule dijalo.. sasa akawa anatoa kichekesho nilishangaa sana yani anaanza kucheka yeye kabla hata sisi hatujachekaa..nikazima tu nikasema uende kwa amani
 
Bora umenisemea brother, nilitamani kuja na uzi nikajua mapovu ya hapa ntapata hadi ya mipapai.

Sipendi kuamini kama mimi na wewe hisia zetu za furaha(kucheka) ziko mbali.
 
Kuna commedy moja MC Pili pili amecopy from Basket Mouth kama ilivyo. Na presentation yake wala haichekeshi.
 
Mi naangali stand up comedy nyingi sana pamoja na east africa kina salvador ,teacher mpamire wa uganda,na churchill show and raw nikiangalia hapa bongo mwenye uwez wa kufika level hizo namuona masanja...mc pilipili hana kipaji hicho cha kufanya stand up labda afanye kama kina mkwere vipindi vya kurecord anarudia rudia jokes kila mahali anafikikiri anakutana na watu wapya kila siku na wakati watu ni hao hao na siku hivi mtu ana angalia show zako you tube anaona unarudia mambo yale yale na la pili ana copy sana jokes za comedian wa nje jokes zake nyingi nishazisikia kwa kina salvodor wa uganda na trevo noah..!..inabidi kubadilika sana au abadili uelekeo ingawa kwa upande mwingine nimsifu anajua kuifanya hiyo biashara na kujibrand kama kina kingwendu,zembwela,marehem Max,majuto wangekuwa na jicho kama lake la kibishara hii wangekuwa mbali sana maana wanavipaji vya hali ya juu sema sanaa yao wanaifanya kienyeji sana...anaweza kubadili uelekeo wa kusimamia wenye vipaji kama anavyofanya churchill..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…