Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Mc Pilipili utanisamehee kwa ukweli huu "huna kipaji cha kuchekesha"

Uko sahihi kabisa. Si kwa kumwonea wivu. Ni kweli huyu mjamaa ni mropokaji na si mchekeshaji. Mimi ni mpenzi wa komedi sana na huwa nazifuatilia za ndani na za nje ya Tanzania .
Kitu ukiforce mbele kinakushinda. Kuna Comedy wanazicheza Marekani zisizo na sauti ni nzuri sana na mtu kama MC PILIPILI hawezi kuzicheza zile kwani anatumia muda mwingi na nguvu nyingi kulazimisha hadhira imwelewe.
 
Kuna mambo ya kupeana support na kuna mambo pia ya kuelezana ukweli, siko hapa kumkatisha mtu tamaa ila My Brother Mc Pilipili sanaa ya Uchekeshaji imekupiga Kanzu.
Speed ya standup comedy ilipo na ww unachokifanya ni Kigoma na London.

"Wapaka mafuta kwa mgongo wa chupa hamtakosekana kussuport comedy ya huyu mtu kinafiki,ila kwa mm binafsi,
Lazima tuiite beleshi beleshi na sio kijiko kikubwa. !"

Mc pilipili Ukumbuke tu,si kila anayepiga makofi basi anakupongeza , ukitaka uhakika muulize "Mbu".

WEWE SI MCHEKESHAJI.

AHSANTENI.
Tutamshauri awe kama wewe msaga soli na mchana majamvi
mtoa post nakuunga mkono
 
kufurahi ni hiari sio lazima, hata wewe mtoa post ni comedy kwa wengine
 
Kweli kabisa analazimisha lakini patupu
Kawaida yenu watz hamna jema wala uzalendo kwa watz wenzenu mapingwa wa kukosoa hamna hoja au mchango chanya.

Gonga mzigo pilipili nani kawahi kuwa kama. Wanakudiscuss kwakuwa wameshaona umetoka wao bado wako vijiweni kusogoa na hawana ishu
 
Halafu vichekesho vyake huwa anavirudia vile vile kila anapoenda ku-perfom.Hata akitoka nje ya nchi lazima atatoa kichekesho kile cha wakati wa ngonjera zamani shule ya msingi.Kwa kifupi sio mbunifu.Mara 100 hata Joti ana nafuu.
 
Kawaida yenu watz hamna jema wala uzalendo kwa watz wenzenu mapingwa wa kukosoa hamna hoja au mchango chanya.

Gonga mzigo pilipili nani kawahi kuwa kama. Wanakudiscuss kwakuwa wameshaona umetoka wao bado wako vijiweni kusogoa na hawana ishu
Kukoselewa ni kawaida. Kama ana akili huu uzi utamjenga. Sisi wateja wake lazima tumwambie ukweli.
 
Pilipili yuko juu kwasababu tz wenye vipaji wamekosa support ,ila kiukweli huyu jamaa hajawahi kunichekesha hata siku moja
 
Huyo idriss nae kafulia mpaka huruma yaani mtu upewe 600 millions na fame alafu mwishowe ugange njaa kwa kubaka talent za watu na kutangaza viredio vya vichochoroni?
Ndio ujue kuna akili ya pesa na akili ya kuvkia barbar
 
Back
Top Bottom