TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Chinembe ni Mungu yupi huyo????? Mungu ni wa rehema na hataki hata mmoja apotee.

Kama huyo Mungu wa Lowasa anaua kila atakayemsema basi atauwa watu wengi sana. Lile kusudi la kazi ya msalaba litakuwa limefitinika.

Bwana wetu Yesu Kristo alifanyiwa kila namna ya uovu akasema Baba wasamehe hawajui wafanyalo. Huyo Mungu wa kulipiza papo kwa papo !!!!!!! Mh!!!!! Wapi kazi ya MSALABA???

Damu zilizomwagika hata sasa kama ni mapenzi ya Mungu zitaenda kwa AMANI. Kama ni umafya na ushirikina basi tegemeeni KISASI cha Bwana.

Queen Esther


Mungu huyohuyo alisema, usihukumu kabla hujahukumiwa...
 
Kweli Lowassa Mungu anamlinda sana. Wansomdhihaki kuhusu afya yake ndo wanatangulia. Mungu ni mwema!
 
hakuna aijuaye kesho yake yule aliyesema ni mgonjwa bado yu hai. hakika mungu ni wa wote.
 
lkn c alimdhihak edo?,leo yeye katangulia na wengne kama kina nepi nauye wajipange

Mkuu suala la mauti halina siasa, kwa kauli yako hiyo unarudia makosa ya unaowakemea. Kuwa kama EL, samehe na usahau.

"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu." - Ayubu 14:1

Pole kwa wafiwa!
 
Kama hii ni habari ya kweli, NATUMAI IMETHIBITISHWA NA Moderator,
INASIKITISHA SANA TAIFA LETU LIMEFIKA PABAYA, WATANZANIA WENGI HUMU NAONA BADALA YA KUKUBALI MCHANGO WAKE ALIOULETA MCHUNGAJI MTIKILA KTK AMSHA AMSHA YA DEMOCRASIA, WATU WANAONGEA KANA KWAMBA WAO WATAISHI MILELE NA KUONGELEA 'MABAYA' KUWA ALIKUWA ANAMPONDA MTU FULANI SANA HIVYO KIMTAZAMO WAO WANAONA KAMA AMESTAHILI HIVI, NI MUNGU KAAMUA KUMCHUKUA MWANAE, HAMNA LINGINE HAPO.
Watanzania tumekubali kuwa watumwa wa siasa na siasa INATUGAWA vibaya sana, tumekuwa kama blue band na siasa ni kisu cha moto kikipita katikati yetu. INASIKITISHA SANA.
MUNGU AMETOA NA MUNGU AMETWAA, jina lake LIHIMIDIWE.
R.I.P Mchungaji, C.Mtikila.

Ww Specialize ktk Mazr yake. Wengine wa specialize ktk mabaya yake. Kwani shida ipo wapi? Ww fanya utakalo na wengine wafanye watakayo!!

Ww ni nani wa kuwachagulia watu mitizamo ktk mambo flaflani??
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

=====
UPDATE:

JamiiForums imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

Utabiri umetimia R .I.P
 
Mungu amlaze pema baba mchungaji, pamoja na yote kifo ni sehem ya maisha ya mwanadamu hakuna hata mmoja atakaekwepa hii njia hata kristo mwana wa mungu alikufa sembuse mwanadamu alie asili ya uovu? Kama mtu alikua anawaza na kunena tofauti na unavyotaka wewe ndio kupelekee ufurahie kifo chake? Wapendwa haya mabadilko yanayohitajika ndugu zangu yasijepelekea kukuingizeni jehanamu jamani!
 
Mungu awape nguvu wafiwa , ndugu, jamaa na marafiki, poleni sana..mbele yako nyuma yetu, pumzika kwa Amani Mchungaji Mtikila, tutakukumbuka daima!
 
Back
Top Bottom