Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chinembe ni Mungu yupi huyo????? Mungu ni wa rehema na hataki hata mmoja apotee.
Kama huyo Mungu wa Lowasa anaua kila atakayemsema basi atauwa watu wengi sana. Lile kusudi la kazi ya msalaba litakuwa limefitinika.
Bwana wetu Yesu Kristo alifanyiwa kila namna ya uovu akasema Baba wasamehe hawajui wafanyalo. Huyo Mungu wa kulipiza papo kwa papo !!!!!!! Mh!!!!! Wapi kazi ya MSALABA???
Damu zilizomwagika hata sasa kama ni mapenzi ya Mungu zitaenda kwa AMANI. Kama ni umafya na ushirikina basi tegemeeni KISASI cha Bwana.
Queen Esther
lkn c alimdhihak edo?,leo yeye katangulia na wengne kama kina nepi nauye wajipange
usitanie mkuu
Kama hii ni habari ya kweli, NATUMAI IMETHIBITISHWA NA Moderator,
INASIKITISHA SANA TAIFA LETU LIMEFIKA PABAYA, WATANZANIA WENGI HUMU NAONA BADALA YA KUKUBALI MCHANGO WAKE ALIOULETA MCHUNGAJI MTIKILA KTK AMSHA AMSHA YA DEMOCRASIA, WATU WANAONGEA KANA KWAMBA WAO WATAISHI MILELE NA KUONGELEA 'MABAYA' KUWA ALIKUWA ANAMPONDA MTU FULANI SANA HIVYO KIMTAZAMO WAO WANAONA KAMA AMESTAHILI HIVI, NI MUNGU KAAMUA KUMCHUKUA MWANAE, HAMNA LINGINE HAPO.
Watanzania tumekubali kuwa watumwa wa siasa na siasa INATUGAWA vibaya sana, tumekuwa kama blue band na siasa ni kisu cha moto kikipita katikati yetu. INASIKITISHA SANA.
MUNGU AMETOA NA MUNGU AMETWAA, jina lake LIHIMIDIWE.
R.I.P Mchungaji, C.Mtikila.
nasikia uchaguzi unasogezwa mpaka february
Wakuu,
Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.
=====
UPDATE:
JamiiForums imeongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.
Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.
Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.
Ndiyo hivyo jamani
Kwahiyo Lowasa ni mchawi au mungumtu?
duh hii sasa noma!Tetea na wewe ufe...nasiku ukifa ntalala bar sikupendi kabisa mkuu.