TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Mchungaji C.Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya gari maeneo ya chalinze.

Source:Star Tv

Jamani wiki mbili zilizopita alialikwa katika kituo cha television cha StarTv.Jambo kubwa ninalokumbuka ni jinsi alivyomkashifu mgombea Urais wa Chadema kuwa badala ya kutumia pesa kwenye kampeni wampeleke hospitali.

Kwa kweli jamani tuchague maneno ya kusema tunapozungumza,Swala la ugonjwa ni la Mungu ili isije ikaleta hisia za laana ya Mungu.
 
na huo ndo ukweli, anaweza kuishi mda mrefu but kwa mikikimikiki ya urais kwa ile afya ni BIG NOOO!

Muangalie Lowasa na Magufuli katika kipindi hichi cha kampeni nani afya inazorota?..
 
MTIKILA akiwa asubuhi STAR TV: juzi tu alisema:

"IKULU sio ICU...."

R.I.P Mtikila...!!!

Kuna mengi sana ya kujifunza hapa...

Mungu ndie anajua lini ALIKULETA DUNIANI na lini ATAKUONDOA DUNIANI...!!!

Sio mwanadamu kamwe... tuchunge sana ndimi zetu...!!!
 
Ni wendawazimu kufikiri kwamba kama humuungi mkono Lowasa utakufa,kifo ni mpango wa Mungu,rest in pc Mtikila!

Kuna maelfu kwa maelfu hawamuungi mkono Lowassa, kuna wachache wameenda mbele zaidi na kuchukua nafasi ya Mungu kwa Kumwita Lowassa ni Marehemu, Lowassa ni Jeneza, cha kushangaza na kusikitisha ni hawa wachache kutangulia wao kwa kumwacha yule wanayemwita Marehemu au Jeneza linalotembea! Kwa hili, mjifunze! Ila mkiendelea na Kushupaa na kuwa vipofu ya yanayoendelea, hamna namna mtakayopona! Mungu akurehemu na kukufungua ili uweze kuona na kufahamu yeye ni MUNGU wa aina gani!
 
R.I.P mtikila but watanzania tuna cha kujifunza hapa, kumnene mwenzako mabaya tuache kwani only God anajua nani atatangulia.
 
Kwani luwassa alikua mzungu....! Nyie ndo wajinga kweli... wapumbavu ndo wanapewa magodoro na vihela.. hii nchi haina amani watanzania sisi na wavumilia... (in bibi's vocal)
 
Ukweli utaendelea kusemwa tu no matter wasemaji wataendelea kufa maana hakuna kitu muhimu kama kusema na kusimamia unachokiamini.

Heri kufa kwa kusema na kusimamia unachokiamini kuliko kuishi kinafiki,I believe wapo watakao okota silaha alizoanguka nazo Mtikila na mapambano yataendelea.

You played your part man!!

R.I.P Mtikila.

Vipi kaacha kesi ngapi zinazoendelea mahakamani?
 
Mchungaji Mtikila amefariki bila kuomba radhi kwa kumkufuru roho Mtakatifu yeye ajaaliaye afya!
 
R. I. P mtikila, Ila hii ajali duh  mbona hana jeraha lolote duh mwili unaonekana haujaumia popote labda alikufa kwa mshituko
Majeraha ya ndani kama vile ini kupasuka utaona kwa kuangalia? Mara nyingi ajali za gari watu hufa kwa sababu ya massive brain injury inayotokana na gari kusimama ghafla. Kama unakumbukumbu za Newton's law of motion utanipata. Ndio maana tunaambiwa tufunge mikanda lakini waswahi tunaona ni usumbufu!
 
Mungu amlaze pema Mchungaji Mtikila. Yeye ametangulia tu wote sisi tunaelekea alikoenda/alikokwenda. Ni vigumu mno kumuelezea Mtikila alivyokuwa wakati wa uhai wake kwa masuala ya kisiasa na kijamii. He was a character. AnaudhI na kufurahisha kulingana na mtu yuko upande upi kisiasa.
 
Ni masikitiko kwa wana wa Tanganyika kwani wanatanganyika wa Njombe alikuwa wametoka kuzungumza nao na kunadi wagombea wawili wa ubunge na udiwani njombe mjini siku ya jana Habari ya kile alicho kisema Njombe Kitakujia kwa Kubofya hapa www.eliabu.blogspot.com :crying: Mungu ailaze mara pema poponi Roho ya Marehemu
 
Chadema mnapofurahia kifo hiki itabidi uchunguzi mkali uunganishe na dots za kifo cha Chacha Wangwe, inaonyesha mlivyofurahi basi kuna kitengo cha mambo hayo hapo kwenu, haiwezekani mfurahie msiba. Na ICC iunganishe matukio haya.

Sidhani kama chadema watafurahia kifo kwa kua ni pigo kwao kama uchaguzi utasogezwa.
 
Back
Top Bottom