TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

TANZIA Mch. Christopher Mtikila afariki baada ya kupata ajali, Msolwa - Chalinze mkoani Pwani

Nimemsikiliza mchungaji ambae walikuwa na mtikila kwenye gari. Amesema walipomaliza kuweka mafuta pale morogoro , waliondoka bila mtikila kufunga mkanda. Na speed ilikuwa kali sana licha ya mtikila kumsihi dereva kupunguza speed mara kwa mara.

Na mbeleni aliovertake gari ikamshinda . Tuachane na imani potofu na siasa za maji taka hazitatusaidia.
 
Inasikitisha pale watu wanapoingiza siasa katika kifo cha mtu. Kweli Mtikila alikuwa mpinzani binafsi asiyetengamana na upande. Alikuwa tayari kuvikosoa hata vyama vya upinzani. Huu ni msiba mzito kwa taifa letu kumpoteza mwanasheria mahili. Tusiweke mzaha katika mambo muhimu.
 
Mtikila_478_292.jpg

Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake

MWANASIASA machachari nchini, mwenye uthubutu na aliyesimamia misimamo yake, Mchungaji Christopher Mtikila, hatunaye. Mtikila alifikwa na mauti baada ya gari lake aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T189 AGM alilokuwa anasafiria kuacha njia na kupinduka eneo la Msolwa, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro, alfajiri ya kuamkia jana.

Wakati Mtikila akifikwa na mauti katika ajali hiyo inayoelezwa mwili wake ulitupwa nje ya gari baada ya kupinduka, watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha. Ajali iliyosababisha kifo cha Mchungaji Mtikila imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jafary Mohammed.

Alisema Mtikila na watu aliokuwa nao kwenye gari hilo lililokuwa linaendeshwa na George Steven (31) maarufu Ponera, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam lilikuwa likitokea Njombe ambako mchungaji huyo aliyekuwa hakaukiwi na harakati, alipita akitokea Rungwe kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya chama chake cha DP, Nicodemus Atuswege Ngwale.

“Gari hilo likiwa na abiria wanne akiwemo marehemu mkazi wa Mikocheni B, lilikuwa kwenye mwendo wa kasi, likaacha njia na kuserereka pembeni mwa barabara kisha kupinduka ambapo Mtikila alirushwa nje ya gari na kupoteza maisha papo hapo,” alisema Kamanda Mohammed. Mbali ya dereva, abiria wengine waliojeruhiwa ni Mchungaji Patrick Mgaya (57) na Ally Mohammed (42), wote wakazi wa Dar es Salaam.

“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi wa dereva huyo ambao ulisababisha ashindwe kulimudu gari na kuserereka pembeni ya barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha kusikitisha cha mwanasiasa huyo,” alisema Kamanda Mohammed.

Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio zilisema kuwa baada ya ajali hiyo majeruhi hawakupata msaada haraka kwani eneo hilo halina makazi ya watu. Naye Katibu Mwenezi Taifa wa DP ambacho Mtikila alikuwa mwenyekiti wake, Msambichaka Mferuzi alisema; “Taifa na Watanzania wote wamepata pigo kubwa sana kupotelewa na mpigania haki wao ambaye siku zote alisimama katika kutafuta haki na usawa kwa kila mtu.

Chama chetu kimepoteza kiongozi mahiri na ambaye alikuwa msingi wa chama chetu, tuna majonzi makubwa sana lakini yote ni kazi ya Mungu.” Mferuzi alisema taratibu za mazishi hazijakamilika hadi ndugu wa familia wakae kikao na chama, ili kupata mwafaka wa eneo ambalo watauhifadhi mwili wa marehemu.

Katika makazi ya marehemu yaliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, mamia ya waombolezaji wakiwemo wanachama wa chama cha DP pamoja na ndugu jamaa na marafiki walifika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila.

Mtikila ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65 na kama si kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa sasa angekuwa miongoni mwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtikila ambaye maisha yake ya kila siku yalitawaliwa na harakati za kisiasa, haki za binadamu na mengine mengine, alienguliwa na NEC kwa kuwa hakuwa na mgombea mwenza.
Akijitetea mbele ya NEC Agosti 21, mwaka huu, Mtikila alisema: “Nimeshindwa kuja na mgombea mwenza kwa sababu mke wake ameugua presha ghafla. Jambo hilo lilimfanya ashindwe kufika hapa.” Mtikila alidai alifika mapema NEC, lakini alilazimika kwenda Mahakama Kuu kwa ajili ya kuapa. Alidai kuwa mahakamani alitumia zaidi ya saa mbili kumsubiri mgombea mwenza, Juma Metu Juma ambaye hakutokea.

“Nilipotaka kumuona Mkurugenzi (Kombwey) nilijibiwa kuwa anashughulikia tatizo langu. Lengo lilikuwa kutaka kumueleza tatizo nililonalo. Kwanza taratibu na kanuni za NEC hazisemi chochote iwapo mgombea mwenza anapata dharura,” alisema Mtikila ambaye alikiri kuwa hakulipa Sh milioni moja licha ya kuwa nayo mfukoni. Baada ya maelezo yake kutoishawishi NEC, Mchungaji Mtikila alisema: “Mimi kugombea si tatizo, ila nataka kuweka mambo sawa.

Hata nisipogombea hiyo hainizuii kwenda mbinguni. Kwanza mtu mwenye uchu wa madaraka ya kwenda Ikulu anatakiwa kuepukwa kama ukoma.” Hii ilikuwa mara ya pili kwa Mtikila kushindwa kutekeleza masharti na hivyo kupoteza sifa za kuteuliwa na NEC kugombea urais. Mara ya kwanza ikiwa mwaka 2010.

Alishiriki mwaka 2005 na kupata asilimia 0.27 ya kura zote, huku Jakaya Kikwete akiibuka mshindi kwa asilimia 80.28. Historia yake Mchungaji Christopher Mtikila alizaliwa mwaka 1950 (ana umri wa miaka 65) huko Ludewa, mkoani Njombe.

Pamoja na shughuli za siasa, pia alikuwa mwanzilishi na mkuu wa Kanisa la Kipentekoste la Full Salvation. Lakini pia kwa muda mwingi wa maisha yake alijihusisha na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho “Liberty Desk”.
Kanisa lake ni moja ya makanisa machache nchini yenye vitengo vya namna hiyo. Umaarufu wa Mtikila ulikua sana mwanzoni mwa miaka ya 1990 kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, madai yake kuhusu kile anachokiita “uhujumu wa uchumi unaofanywa na watu ambao aliwaita magabacholi” na kesi mbalimbali za kikatiba alizokuwa akifungua katika Mahakama za Tanzania, ni kati ya mambo machache yaliyomfanya asikike kila kona ya nchi.

Kwa muda mrefu, chama chake cha DP hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na kukataa kwake kuitambua Zanzibar. Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na siyo Tanzania. Hata hivyo, ilimpasa abadili msimamo wake katika miaka ya hivi karibuni kwa kukubali kutafuta wanachama kutoka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) ndipo kikapata usajili wa kudumu.

Mwaka 1999 Mtikila alifungwa kwa mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba. Mwaka 2004 pia alihukumiwa kifungo kilichosimamishwa cha miezi sita kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya mkuu wa polisi wa wilaya ya Ilala.

Kwa ujumla maisha yake yamekuwa ni ya harakati muda wote, akipambana awezavyo, akisimama kidete inavyowezekana na akijikuta matatani kila uchwao. Mchungaji Mtikila ameacha mjane, Georgia na watoto.

Ubunge, urais na kesi za kikatiba Itakumbukwa kwamba, kabla ya kujaribu kuwania Urais, mara kadhaa alijaribu kuusaka ubunge, akianzia mwaka 1997, akiwania kwa tiketi ya Chadema kwa kuwa DP hakikuwa na usajili wa kudumu.

Hata hivyo, baada ya uchaguzi mdogo uliompa ushindi Crispin Haule wa CCM, Mtikila aliachana na Chadema na kurejea kukiimairisha chama chake. Mtikila aliyekuwa maarufu kwa watu wa rika zote, alikuwa na sifa kadhaa, moja wapo ikiwa ni kuwa kiongozi anayejishughulisha na mambo mengi mno na harakati zilizopitiliza, akiwa na ufahamu wa vitu vingi pia.

Aidha, alipambana kisheria na serikali kwa kufungua kesi za masuala mbalimbali dhidi ya serikali, zikiwemo za kikatiba. Aliwahi kufungua kesi ya kutaka wagombea binafsi kuruhusiwa katika uchaguzi wa Tanzania, wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila hati za kusafirioa na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya na polisi na nyinginezo.

Na juu ya yote, Mtikila aliyekuwa hajali kupanda pikipiki au Bajaji kuwahi harakati zake, zikiwemo za mahakamani, alikuwa mtu mwenye misimamo ya kipekee. Alipokuwa na ajenda zake, bila kujali hatimaye yake, alizisimamia kwa nguvu zake zote.

Mtikila ameaga dunia akiwa mwanasiasa mashuhuri nchini, akiwa na uwezo wa kuongoza kanisa (uchungaji), kuongoza chama cha siasa na kushinda mahakamani kupambana na Serikali kwenye kesi kubwa na ambazo nyingine alishinda.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Christopher Mtikila.

Imeandikwa na John Gagarini, Kibaha na Emmanuel Ghula, Dar

Chanzo kwa hisani ya Habari Leo
 
Kumetokea maneno mengi na baadhi kugeuzi kifo cha Mtikila mtaji wa kisiasa, habari za uhakika kwa uchunguzi wa gazeti la habari leo, taarifa za polisi zinathibitisha chanzo ni mwendo kasi wa gari aina ya Toyota Corola lililomilikiwa na Mtikila mwenyewe na kisha kuserereka kisha kuacha njia na kupinduka ambapo Mtikila alitupwa nje ya gari. Hizo habari za vijiweni achaneni nazo.
 
Kama mzee kingunge mwenye kadi namba 8 ya chama anataka mabadiliko wewe kijana mwenye kadi namba 2456000 unasubiri mpaka ushituliwe na juma nyoso? Tafakari chukua hatua
 
Inasikitisha pale watu wanapoingiza siasa katika kifo cha mtu. Kweli Mtikila alikuwa mpinzani binafsi asiyetengamana na upande. Alikuwa tayari kuvikosoa hata vyama vya upinzani. Huu ni msiba mzito kwa taifa letu kumpoteza mwanasheria mahili. Tusiweke mzaha katika mambo muhimu.

Ni weli kabisa nami nakubaliana nawe asilimia 100% Alikuwa mwkeli ingawa kuna watu walikuwa wanamdhihaki. Je kwa sasa issue ya kuwa Mgobea binafsi si ni sawa. Kwa sababu kwa sasa UKAWA wengi hawana jinsi, hawaipendi CCM hawampendi Lowasa lakini kwa kuwa yuko tu upande wa Upinzani hawajali athari ya baadawe wanataka kumpa tu je Kungekuwa na room ya mgombea binasfsi? Kwa hiyo Mtilikila alikuwa ni kwa ajili ya Mtanzania na si vinginevyo! Watanzania tumepoteza mmoja wapo wa Mashujaa!
 
ADUI WA TUTSI :WARAKA WA MTIKILA ULIOZAA OPERESHENI SANGARA


MAANGAMIZI YA KUTISHA YA WANANCHI
(Wanyarwanda wahusika na unyama dhidi ya Wasukuma)
Hii ni Taarifa ya kuteketezwa zaidi ya nyumba 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma kwa moto, pamoja na tani nyingi za mazao yao ambayo ni pamoja na mpunga, mahindi, maharagwe, mtama, dengu, uwele, serena, pamoja na mali zao zingine, katika eneo liitwalo Buligi, katika Wilaya ya Muleba. Unyama huu wahusika wamejaribu kuuficha kwa jina la ‘Opresheni Okoa mazingira’. Ni lengo la Katiba ya Nchi yetu na Sheria pamoja na taarifa ifuatayo, kwamba wote waliohusika na maangamizi haya waadhibiwe vikali, na wananchi wote waliofanyiwa unyama huu ni lazima walipwe fidia za mali zao na mateso ya kutisha waliyopata.
Baada ya kuchomewa nyumba zao na mali zao zote wananchi wengi wamelundikana makanisani, na wengi wako maporini wakikimbia unyama wa kutisha na kuporwa mali zao.
Vijiji vilivyoteketezwa ni pamoja na Nyamiranda, Itunzi, Kasharara na Kiteme. Uharamia uliendelea mpaka maeneo ya Karagwe na Biharamulo kama alivyoeleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika vyombo vya habari, kama gazeti la Mtanzania Toleo nambari 7142 la tarehe 17/11/2012. Utetezi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe wa maangamizi ya kutisha ya Wasukuma, kama ulivyokuwa ule wa Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, kwamba ilikuwa opresheni maalum iliyolenga kuondoa wahamiaji haramu wenye maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi ya Taifa ya Buligiuna ukweli. Lakini Wasukuma si wahamiaji haramu, kwa sababu ni wazawa katika nchi yao, na hayo maelfu ya ng’ombe katika hifadhi si ya Wasukuma bali ni ya Watusi wa Rwanda.
KIINI CHA MATATIZO YA WATUSI DUNIANI
Hakuna asiyejua kuwa malengo makuu ya kuanzishwa Umoja wa Mataifa ni pamoja na kulinda haki na usawa wa binadamu wote ulimwenguni, ili idumu amani na kuleta maendeleo katika kuboresha maisha ya binadamu. Ndiyo maana ile sera ya Makaburu ya udhalilishaji wa mtu mweusi au ubaguzi wa rangi waliyoiita apartheid ilipigwa vita na dunia yote, mpaka ikatokomezwa. Hata ushujaa wa Nelson Mandela unaopita umaarufu wa kiongozi mwingine yeyote duniani, aliupata kwa sababu ya uhanga wake katika kutetea usawa wa binadamu wa rangi zote duniani.
Lakini apartheid ya Makaburu haikuweza kuufikia ushetani wa Watusi, jinsi wanavyowadhalilisha Wahutu na Wabantu wengine, kwa imani yao chafu sana kwamba wao eti waliumbwa kwa ajili ya kutawala tu, na kwamba Wahutu waliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao! Ni makufuru yanayojulikana wazi ya Watusi kuwatema mate Wahutu au Wabantu wengine kwa kinyaa kama vile ni mavi mbele zao.
Na imani yao hii ya kishetani ndilo chimbuko la mbinu na mikakati yao yote ya kutawala siyo tu Maziwa Makuu bali hatimaye hata Afrika yote ya ‘watumwa’ wao! Tabia ya Watusi ya kula wao kwanza, halafu kuwatupia makombo watumwa wao (Wahutu), tena baada ya kuyatemea mate na makohozi, ni historia inayojulikana na kila mzawa wa Maziwa Makuu. Hata maendeleo yalipozidi kutowesha giza hili, bado wanawake Watusi walilazimika kudumisha udhalili wa Wabantu kwa kuolewa na wale wenye mali lakini mimba wapate kwa Watusi wenzao, ikibidi hata kwa ndugu zao wa damu kama hakuna Watusi wengine karibu. Historia itamuenzi shujaa Gregory Kayibanda wa Rwanda kuliko inavyomuenzi Nelson Mandela wa Afrika Kusini, kwa kutokomeza ile apartheid chafu kupindukia ya Watusi nchini Rwanda mwaka 1959.
Ukweli ni budi uheshimiwe na dunia kwamba Watusi wengi walikimbia kutoka Rwanda kufuatia mapindizi yale, kwa sababu ya kukwepa balaa ya kuwa chini ya watumwa wao! Watusiwalikimbilia Burundi na Tanganyika kwa baba yao Julius Nyerere, kujipanga kwa ajili ya “kurudisha ubwana wao juu ya watumwa wao” Rwanda. Kwa imani ya kishetani ya Watusi, Watanganyika kwao wao ni mataahira tu kama Wabantu wenzao yaani Wahutu. Hata bila kupayuka Watusi wanarithishana imani kwamba sisi tuliumbwa kwa ajili ya kuwa watumwa wao.
Ubwana wa Watusi uliimarishwa kwa kupandikizwa utwana katika mioyo ya Watanganyika, wa kuwaona Watusi kuwa bora kuliko Wahutu pamoja na hata sisi wenyewe! Hali hii ndiyo iliyowezesha Watusi kujipenyeza katika sehemu zote nyeti za utawala wa Nchi yetu, pamoja na uhodari wao katika matumizi ya rushwa ya mapesa na chambo cha wanawake zao (the Tutsi sexual diplomacy). Ndivyo Watusi walivyofanikiwa hata kuiteka kifikra jumuiya ya kimataifa, ikabariki na kuwasaidia kuangamiza Wahutu zaidi ya milioni sita, na hata kugeuza kibao kuhusu genocide ya Rwanda kwamba Wahutu ndio walioangamiza Watusi!
Ndiyo maana nchi yetu ilipokuwa na wakimbizi wa Kitusi na wa Kihutu, Watusi walipendelewa kwa kuhudumiwa kama wafalme na kuandaliwa kurudi “kuikomboa” Rwanda. Kwani ingawa Rwanda ilikuwa na utawala wa kidemokrasi wa Wahutu walio wengi kwa asilimia 85% Watusi wakiwa asilimia 14% tu, ni haramu Watusi kuwa chini ya Wahutu kwavile eti ni watumwa wao! Ni kweli kwamba matokeo ya ufisadi na utwana wa watawala wetu wanaoamini katika ubwana wa Watusi, ni pamoja na kufurahisha Watusi na baba yao Nyerere kwa kuhusika kwa serikali yetu katika yafuatayo:
1. Maangamizi ya Wahutu zaidi ya 6,000,000,
2. Uvamizi wa Jamhuri ya Rwanda kupitia Uganda na Burundi, ambapo maandalizi kwa sehemu kubwa yalifanyikia nchini mwetu kwa mkono wa Serikali ya CCM.
3. Kuhusika kikamilifu na mauaji ya kinyama ya marais watatu Wahutu wa Burundi na Rwanda yaani Melchior Ndadaye, Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamira pamoja na ujumbe wao wote, na ushetani mwingine wa kutisha.
4. Kujiuza utumwani kwa Watusi, na kutumika kuliingiza eneo la Maziwa Makuu katika Himaya yao, kwa kuwasaidia kuingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati hawana sifa kabisa kulingana na Mkataba wa Uundaji wa Jumuiya(EAC), kwa unyama wa ‘apartheid’ na genocide yao.
5. Kusaidia uvamizi wa DRC uliofanywa na Kagame na Mseveni, watawala wetu wakaivika aibu kubwa Nchi yetu kwa kukataa kushiriki katika Jeshi la SADC (SADC Alliance) la kusaidia ndugu zetu dhidi ya maharamia, Nchi yetu ikaongopea dunia bila aibu kwamba eti haiko upande wowote kati ya wavamizi na mnyonge aliyevamiwa!
6. Kuwarudishia RPF Wahutu takriban milioni moja kwa unyama usiosemeka, waliokuwa wameyakimbia mauaji ya kinyama ya RPF baada ya kuvamia nchi yao, RPF wakawapokea na kuwaangamiza wote, na kumwaga maiti zao kwa maelfu katika mto Kagera, zikawa zinafunika Ziwa Victoria mpaka General Mboma alipotoa Tamko la kuvamia Rwanda kukomesha ushetani huu wa RPF, kama wasingeacha unyama huo mara moja. Nchi yetu inakabiliwa na kisasi cha Mwenyezi Mungu! Na ishara tayari zinaonekana! Kuna kuacha upumbavu na kutengeneza na Mwenyezi Mungu, ama mapigo makali kuliko yaliyoipiga Misri, yatakayosimuliwa vizazi vyote!
Kwa ufisadi na utwana wa watawala wa nchi yetu kwa Watusi, bila chembe ya aibu wala hofu kwa Mwenyezi Mungu waliikaribisha katika ardhi yetu ICTR, ikiwa nyenzo maalum ya kuwasaidia Watusi kuangamiza Wahutu wote wenye uwezo kiuchumi na kifikra duniani! Kenya iliikataa ICTR katika ardhi yake, kwa kumwogopa Mungu kwa sababu ni nyenzo ya genocide iliyoangamiza mamilioni ya Wahutu, ikawafuata mpaka na wale milioni 2.5 waliokuwa wamekimbizia uhai wao Mashariki ya Congo, na kuwateketeza kinyama! Kupenyezwa kwa Watusi katika ngazi zote nyeti za utawala wa nchi yetu kumewezesha Utusi kuteka nyara sera za nchi yetu zitumikie maslahi ya Watusi, kwa gharama ya heshima ya utaifa wetu na maslahi ya nchi yetu.
Na siyo siri kwamba msingi wa laana hii yote iliyoonywa na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati, ulijengwa na dikteta Julius Nyerere, ambaye leo anawekwa mahali pa Mwenyezi Mungu na kufanyiwa ibada ya ‘ubaba’ wa Taifa! Utekelezaji wa ndoto ya Nyerere ya kuweka eneo lote la Maziwa Makuu chini ya Himaya ya Watusi unasimamiwa na vijana wake, madikteta Yoweri Museveni na Paul Kagame aliyeangamiza mamilioni mengi ya binadamu duniani kuliko Adolf Hitler.
Propaganda za ‘Jumuiya au Shirikisho la Afrika Mashariki’ zinazopigiwa debe kwa nguvu na hawa Watusi, ni katika ujenzi wa hiyo Himaya yao. Dikteta Yoweri Museveni ametangaza mara kadhaa haki yake ya kustahili kuwa Rais wa kwanza wa shirikisho la Maziwa Makuu (Himaya ya Watusi), na anacho kikosi cha majasusi zaidi ya 400 ndani ya Nchi yetu, yanaoiyeyusha nchi yetu kwa ajili ya kumezwa katika Himaya hiyo, na mafanikio yanaonekana kwa jinsi utawala wetu wa CCM unavyonyenyekea Watusi na kujidhalilisha kwao.

KUMEZWA KWA DRC KATIKA HIMAYA YA WATUSI
Mwuaji wa kutisha Paul Kagame alikwishaikamata DRC baada ya kufanikiwa kumwua Rais Laurent Kabila, akampenyeza madarakani Mnyarwanda Hypolite Adrien Christophe Kanambe kwa jina bandia la ‘Joseph Kabila’. Wauaji wa Rais Laurent Kabila baada ya kutoroshewa Rwanda walikimbiziwa hapa, ambapo walihamishiwa Norway kimya kimya. Mnyarwanda “Joseph Kabila” anayetawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama Gavana wa dikteta Paul Kagame, ni ndugu wa damu wa Mkuu wa Majeshi ya Kagame, yaani James Kabarebe, ambaye pamoja na Kayumba Nyamwasa ndio waliosimamia yale mauaji ya kutisha ya wale Wahutu milioni 2.5 waliokuwa wamekimbilia DRC, ilipovamiwa nchi yao na wauaji wa RPF. Ni sera ya Rwanda kuhakikisha kuwa DRC haiwi na Jeshi imara, mpaka hapo mkakati wa Himaya yao utakapokamilika.
Ndiyo sababu maafisa wa juu 7,000 wa Jeshi la DRC ni Wanyarwanda. Hypolite Kanambe (Joseph Kabila) anatumikia maslahi ya Rwanda kwa uzalendo wa hali ya juu, na Rwanda inapovamia DRC pilika za Hypolite A. C. Kanambe huwa ni usanii tu wa kuhadaa ulimwengu. Vinginevyo lazima DRC ingewapa silaha askari Wahutu waliojichimbia Congo, ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuutokomeza unyama wa Watusi. Hata uvamizi wa Rwanda wa RPF ulifanikiwa kwa kutanguliza vikwazo vikali sana, vilivyohakikisha kuwa majeshi ya Hayati Rais Habyarimana hayawi na silaha.
Historia ni budi iwe sahihi, kwamba vijana wa Nyerere yaani Museveni na Kagame walivamia Zaire kwa maelekezo ya baba yao, bila hayati Laurent Kabila, kwa malengo ya kupanua Himaya yao na kuteka tani za dhahabu na madini mengine mengi ya thamani Gbadolite, Kilomoto, Kinshasa, Kisangani na kwingine, kwa ajili ya kujipatia mabavu ya kiuchumi ya kupanulia Himaya yao, na kugharamia propaganda kali inayohadaa jumuiya ya kimataifa. Dunia ilipoanza kupigia kelele uvamizi huo, ndipo Nyerere alipomtafuta Laurent Kabila haraka, zikiwa zimepita wiki mbili baada ya uvamizi kuanza, na kumtanguliza yeye mbele katika kuhadaa ulimwengu, kwamba ni Wakongo wenyewe walikuwa wanaikomboa nchi yao kutoka kwa dikteta Mobutu! Uvamizi ulipoingia Kinshasa Kabila aliwageuka Watusi kizalendo, na kuwaambia sasa warudi kwao wawaachie Wakongo nchi yao.
Kwani aliyekusudiwa na Watusi kuwa gavana wa Rwanda wa koloni hilo ni Bizimana Karahamheto au ‘Bizima Karaha’ kwa jina la hadaa. Uporaji wa kutisha wa utajiri wa DRC ndio mtaji wa jeuri yote ya Kagame leo, ya kuchezea amani ya Maziwa Makuu, na kusambaza maelfu ya majasusi katika nchi za kusini mwa Afrika, kuzifanyia kazi chafu ili hatimaye zimezwe katika Himaya yao, mbali ya kugharamia kikosi chake cha Escadron de la mort kinachoua wapinzani wake popote walipo duniani.
Siri ya mkakati wa Nyerere wa Himaya ya Watusi ilionekana tangu alipotaka kuchelewesha uhuru wa Tanganyika, eti mpaka majirani wapate wao ili mkakati ufanikiwe, uhuni ambao ulishindwa kuuhadaa ushujaa kama wa Jomo Kenyatta. Mzee Jomo Kenyatta alipogundua jinsi Nyerere anavyochezea uhuru wa wana wa Tanganyika, hatimaye akaunajisi kwa ‘Muungano’ kwa ajili ya maslahi ya Wamarekani katika vita baridi, alilaani kwamba “Hakika Nyerere anatawala maiti”Ndiyo maana ni Watanganyika peke yao duniani wasiojali uhuru wao, wala hatima yao na vizazi vyao vijavyo, wala maslahi ya Nchi yao!
Hii ni baada ya kupigika vizuri vichwani mwao ili wawe kama makondoo ya mtawala, waweze kuvikwa kwa ulaini kongwa la utumwa kwa Watusi, kwa maslahi ya kifisadi ya watumwa walio madarakani, wanaouza utu wao na hatima ya Nchi yao kwa utamu wa tende na halua, zinazomung’unyika mara moja na kupotea! Saa ya ukombozi ni sasa! Ndivyo utaahira wetu unavyoonekana kwa dunia yote ya wenye akili kuhusu kongwa la utumwa la Watanganyika liitwalo “Muungano”, lenye maslahi ya kifisadi ya watwana wachache sana wanaotawala, kama si mmoja tu, lakini kwa gharama ya Uhuru wa Watanganyika, heshima yao na utambulisho wao kama Taifa takatifu la heshima tangu katika Unabii wa Mwenyezi Mungu, tena kwa gharama ya raslimali za Watanganyika na matrilioni ya fedha ya damu yao!
Utaahira wetu sisi Watanganyika unaonekana zaidi baada ya Zanzibar kujitoa rasmi katika huo ‘muungano’ kikatiba, ambapo kwa ajili ya maslahi ya kifisadi watawala wetu wanafumbia macho ukweli kwamba muungano umebatilika! Na kwa ujinga kama wa kuku anapodhani haonekani kwavile amefunika macho yake kwa bawa lake, hawa nao wamekazana kuudanganya ulimwengu kwamba muungano bado upo, na hata kulazimisha raia waukiri kiwendawazimu usanii huo!
Lakini ukweli ni kwamba baada ya Zanzibar kujitoa rasmi yaani kikatiba katika muungano, Wazanzibari ni wachache sana mafisadi na wasaliti waliohongwa madaraka watetee bila haya usanii wa muungano batili, kwa maslahi yao ya kibinafsi, huku wakisingizia maslahi ya ukupe wa Taifa lao (parasitic advantages) katika damu ya Watanganyika.
Kama chatu anavyomvunjavunja mnyama ili awe rahisi kumezeka, ndivyo Nyerere alivyowahasi kifikra Watanganyika na kuwafisha ari ya ukombozi wao na utaifa wao, mpaka kwa kafara ya mwenge, ili wawe rahisi kuvishwa kongwa la utumwa la Watusi. Upofushaji wa jinsi hii huua kabisa uzalendo ndani ya dhamiri ya kila raia katika nchi, na kuwaacha wananchi katika minyororo ya woga tu akilini mwao, badala ya uhanga kwa ajili ya Taifa lao.

KAGAME NA MUSEVENI - HATARI SANA KWA TAIFA LETU!
Uharamia anaoufanya Kagame kule Mashariki ya Congo hapa kwetu alifanikiwa siku nyingi. Tofauti ya DRC Mashariki na mikoa yetu ya Kagera na Kigoma ni kwamba wenzetu wanayo hata majeshi ya mgambo ya uzalendo wao yanayotetea ardhi yao na uhuru wao, kama vile Mai Mai. Lakini sisi tuliuawa kabisa uhanga wetu kwa ajili ya Nchi yetu.
Tumebaki kuwasujudia wageni wanaoteka na kuipora nchi yetu, na kututia utumwani katika nchi yetu wenyewe. Hii ndiyo raha ambayo Nyerere aliwaandalia Kagame na Mseveni kwa Watanganyika. Kagame tayari ameingiza katika Nchi yetu Wanyarwandazaidi ya 35,000 wenye silaha, wengi wakiwa katika mapori ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi na maelfu ya ng’ombe waliowaingiza kutoka kwao Rwanda na Uganda. Kwani kule kwao wamejiwekea sheria kali ya kuokoa mazingira yao, kwamba ni marufuku mtu kumiliki zaidi ya ng’ombe tano (5). Kwahiyo mamia ya maelfu ya ng’ombe zao wameziingiza katika ardhi yetu kwa njia za porini, na wapo Wanyarwanda wenye ng’ombe mpaka 10,000 mtu mmoja ndani ya Nchi yetu.
Maelfu mengi ya ng’ombe hao wa Wanyarwanda wanajulikana kuwa mali ya dikteta Paul Kagame mwenyewe na mawaziri wake, na wengine ni mali ya dikteta Yoweri Mseveni, wengi wakiwa hata na mihuri ya NRA! Mbali ya Hifadhi ya Taifa ya Buligi, maelfu mengi ya ng’ombe wao wamewaswagia katika mapori yetu ya Kasindaga, Katete, Kinesi (Karagwe), Nyakerera, Kyobuheke na Misambya na kwingineko, ambako Wanyarwanda wamejikatia mabuloku makubwa sana (Blocks) ambayo wazawa hawaruhusiwi kukanyaga, na wakithubutu ni kuuawa.
Kitendo cha Kagame na Museveni cha kuifanya Nchi yetu kwamba haina Utaifa na heshima ya mipaka yake (sovereignty and territorial integrity) kama zilivyo nchi zao, ni Tangazo la Vita!
Ni lazima tujibu mapigo kwa nguvu kuliko tulivyomjibu dikteta Idd Amin Dadah. Majeshi yetu yaanze mazoezi makali ya vita, na raia waanze upya mafunzo ya mgambo kwa ajili ya Nchi yetu. Kama lilivyoanza tatizo la uvamizi wa Kagame DRC Mashariki, maelfu ya Wanyarwanda tayari wamekamata ardhi yetu kubwa sana, kwa kutumia vibali bandia vya kuishi nchini, na makaratasi ya uraia bandia wa Nchi yetu. Jasusi la Kagame liitwalo Athanas Kafurama mara nyingi hudhalilisha wazawa wa nchi yetu kwamba hawana kitu vichwani, na kwamba Tanzania inamjali mtu mwenye pesa yaani kama wao, na siyo raia wake walalahoi! Kagame amefanikiwa kwa sehemu kubwa kuiteka kimya kimya mikoa yetu ya Kagera na Kigoma! Hata Mkuu wa Mkoa wa Kagera Col. Fabian Masawe unamwuma moyo, jinsi Kagame na Mseveni walivyopenyeza askari zaidi ya 35,000, waliojichimbia na maelfu ya ng’ombe, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Buligi. Wanyarwanda wamekamata ardhi yetu kubwa sana, bila kuwa hata na vibali vya kuwepo nchini mwetu. Kabla ya kueleza zaidi juu ya uvamizi wa Buligi mkoani Kagera, tunapenda ifahamike kwamba Mkoa wa Kigoma umeingiliwa na Wanyarwanda na Warundi zaidi ya 100,000, ambao tayari wameteka sehemu kubwa ya ardhi ya Taifa letu, katika upanuzi wa Himaya yao.
Tena wanajipenyeza kupitia katika makanisa maalum yanayoeleweka. Tayari wameanza kufanikiwa kukamata utawala wa Nchi yetu, kama vile Mnyarwanda aitwaye Peter Serugamba alivyoteka Jimbo la Kigoma Mjini, au Diwani John wa Kata ya Gungu. Watusi wamegundulika kuwamwagia rushwa viongozi wa vijiji na vitongoji ambao wanawatumia kuiteka ardhi yetu, na nafasi hizo wamepanga kuzichukua wao katika kuijenga Himaya yao.
Vikao vya Watusi vya mikakati yao ya kuitwaa Nchi yetu katika Himaya yao mjini Kigoma hufanyikia katika hoteli ya Coast View, iliyojengwa kwa mtaji uliotoka Rwanda, ambao ni utajiri ulioporwa Congo.
Watusi hawafichi katika majigambo yao, kwamba wanaweza wasilazimike kutumia nguvu za kijeshi kuitwaa ardhi ya Tanzania, kwa sababu eti wanaweza kutumia rushwa tu na akili kuichukua yote bila shida! Wanaujua udhaifu wetu kwa sababu walijipenyeza katika ngazi zote za utawala wa Nchi yetu, katika majeshi yetu, Uhamiaji, Taasisi zetu za fedha, Usalama wa Taifa n.k. Ndiyo maana Nchi yetu takatifu imetumika katika unyama wa kutisha kwa maslahi ya Watusi. Ni kweli pia kwamba nchi yetu inao watawala wanaoweza kununuliwa kirahisi kwa mapesa ya Wanyarwanda, ng’ombe zao na au mabinti wa Kitusi. Ndiyo maana wanampigia debe na kumwinamia mwuaji wa kutisha Paul Kagame, wakati wanajua kabisa kwamba:
1. Kagame amemwaga kinyama sana damu ya mamilioni ya Wahutu, ambao bado anaendelea kuwaua usiku na mchana, kuliko Adolf Hitler alivyowaua Wayahudi.
2. Kagame anaendesha mauaji dunia nzima, kwa kutumia kikosi chake maalum cha Escadron de la mort, ambacho ndicho alichotumia hata kumwangamiza Bingwa wetu wa Sheria, Hayati Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kosa la kuweka wazi katika ICTR kwamba mtuhumiwa mkuu wa genocide katika Maziwa Makuu ni dikteta Paul Kagame. Kagame alihofia kwamba kutokana na majumuisho ya mwisho ya Mwanasheria huyo, lazima Ulimwengu ungelazimisha kukamatwa kwake na kufikishwa mbele ya Sheria.
3. Kagame akiwa na cheo cha Meja alikuwa mstari wa mbele kumwua Rais Thomas Sankara wa Burkina Faso, kule Uagadougou.
4. Kagame alikuwa Burundi kwa ushirikiano wake muhimu na Jean Bikomagu, katika mauaji ya kikatili sana ya marehemu Rais Melchior Ndadaye.
5. Kagame ndiye aliyehusika kikamilifu na utunguaji wa ndege iliyomchukua Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda pamoja na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi.
6. Kagame analaaniwa na dunia nzima kwa kumfanyia unyama wa kutisha mwanasiasa mwanamke, shujaa Victoire Ingabire, ambaye amemtupa gerezani kwa kosa la kugombea Urais wa Rwanda akiwa Mhutu, na kosa la kuwa na kibali kwa wananchi wa Rwanda kuliko yeye aliyeloa damu ya mamilioni ya binadamu aliowaua kinyama.
7. Kagame amemwaga majasusi zaidi ya 1,000 katika Nchi yetu, wanaotumia ufisadi wa mapesa, ngono n.k katika kutengeneza mazingira ya kutekwa utawala wa nchi yetu na Watusi na hatimaye nchi yetu kuwa mkoa wa Himaya yao. Kama ilivyoelezwa juu, maelfu yao wamefanikiwa kujipenyeza katika taasisi zote nyeti za dola ya Nchi yetu. Walipoishika Uhamiaji waliitumia kujipa uraia na kukamata nafasi nyeti na ardhi yetu pia.
8. Maelfu ya majasusi wa Kagame wanajifanya wanashughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda, wengine wanajifanya wafanyabiashara au wanatafuta kuwekeza, wengine wanajifanya wanafunzi. Lakini ukweli ni kwamba Taifa letu liko uchi kwa Kagame, kwa sababu kila tunachokifanya katika Nchi yetu kinaripotiwa Rwanda masaa 24. Katika Jiji la Dar es Salaam, Mikocheni ndiko walikojaa Wanyarwanda hao kama kwao.
ANGALIZO: Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 kwa sababu moja tu kwamba ilishindikana viongozi wa nchi tatu wananchama yaani Tanzania, Kenya na Uganda kukutana pamoja, kwa ajili ya kupitisha maamuzi yote muhimu ya uendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya. Kwa sababu Rais Julius Nyerere alikataa kukaa meza moja na Rais Idd Amin Dadah wa Uganda, kwa sababu Amin alikuwa mwuaji.
“Siwezi kuchangia meza moja na mwuaji aliyeloa damu” alitamka Rais Nyerere, ulimwengu wote ukamuunga mkono hata mgomo wake uliposababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki!
SWALI: Ikiwa Nyerere alikataa kukaa meza moja na dikteta Idd Amin kwavile aliua binadamu takriban 350,000, Jumuiya ya Afrika Mashariki ikavunjika kwa sababu ya kuthamini uhai wa binadamu kuliko vitu vingine vyote, hawa watawala wetu wa leo wa CCM ni binadamu wa jinsi gani, ikiwa wanaweza kulikumbatia na kulipigia debe na hata magoti liuaji la kutisha kama Paul Kagame, lililoua kinyama binadamu zaidi ya 6,000,000 Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Kenya, na kuwapelekea wengine kifo kule kule Ulaya walikokuwa wamekimbizia uhai wao?
Watu wa hatari kuliko wote kuhusu amani katika Maziwa Makuu ni hawa madikteta, Paul Kagame na Yoweri Museveni, walioangamiza mamilioni ya raia wa Maziwa Makuu, wakavamia Jamhuri dada za Rwanda na Zaire (DRC) na kuangusha tawala za mataifa hayo huru, na kuipora Congo mpaka dunia nzima inawapigia mayowe kama majambazi ya hatari! Watawala wetu wanakuwa katika akili za namna gani wanapokwenda Kampala na Kigali, na kukaa na Kagame na Museveni na kuzungumzia eti amani katika eneo la Maziwa Makuu, wakati hao ndio wavunjaji makatili wa hiyo amani?
Hivi ni kweli akina Kikwete hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu, kiasi cha kuamua kumsaliti jirani mwema aliyevamiwa na kuangamiziwa mamilioni ya raia wake kwa kosa tu la kuwa Wahutu, na kuwasaidia maharamia waliomvamia? Ni aibu kubwa zaidi kwamba watawala wetu waliishia kukubali umamluki, wa kuwasaidia Kagame na Museveni majeshi eti yakawasaidie kuangamizia Wahutu waliopokonywa nchi yao ya Rwanda, na mashujaa wanaopinga udikteta wa damu wa Yoweri Museveni nchini Uganda! Huku ndiko kuhimiza kisasi cha Mwenyezi Mungu juu ya nchi yetu!

UHARAMIA ULIOFANYWA NA WANYARWANDA BULIGI
Kwanza kabisa, Wanyarwanda hawatasahaulika walivyotikisa Mkoa wa Kagera walipoingia kule kwa uharamia wa kutumia silaha, wakajulikana kwa ufupisho kama Wanyaru. Wanyarwanda waliteka magari, walipora fedha na mali zingine za wananchi, na zaidi waliteka ng’ombe za wananchi na kuzikimbizia Uganda, ambako walizibadilisha na kuleta nchini wale ng’ombe wa kwao, ambao wako tofauti na wetu kimaumbile.
Huu ni ujanja wa kawaida wa kijambazi. Uharamia wa Wanyarwanda ulishamiri mno mkoani Kagera, hapo Buligi pakawa kama makao yao makuu ya kutisha, ndiyo maana palipewa jina la Kosovo. Pori lote mpaka Kyamyorwa lilikuwa halipitiki kwa sababu ya hatari ya Wanyaru., ambao walikuja kutokomezwa na ulinzi wa jadi wa Wasukuma na ushirikiano wa dhati wa Kamanda mzalendo wa Polisi, Inspekta Samson ambaye hivi sasa yuko Wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Kutokana na umahiri wa Wasukuma katika kupambana na uharamia kwa ulinzi wao wa jadi au Sungusungu, Mheshimiwa Wilson Masilingi akiwa Waziri katika Ofisi ya Rais na Mbunge wa Muleba Kusini, alipopita mikoa ya Ukanda wa Ziwa aliwahamasisha Wasukuma kwamba wahamie maeneo ya Kyamyorwa na Kasindaga na kwingine mkoani Kagera, na kwamba wapewe na mashamba kwa sababu ni kweli kwamba Wasukuma kwa asili ni wazalishaji hodari.Wasukuma waliitika mwito huo na kuhamia huko, na ni kweli kwamba waligeuza eneo lile kuwa kitovu cha uzalishaji usio kawaida wa mazao ya mpunga, mahindi, dengu, mtama, ulezi, serena na mengine mengi, mbali ya ufugaji wao.
Baadaye Wasukuma hao walihamishiwa Buligi kutoka hapo Kyamyorwa, kwa maombi ya Waziri wa sasa wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, kwa msingi kwamba eneo hilo ni la kampuni ya Itente ambayo yeye ni mhusika. Profesa Anna Tibaijuka aliandika hata katika kitabu chake cha kampeni yake ya Ubunge wa Muleba Kusini, kuwa Wasukuma wengi walikuwa wamepewa eneo la Kyamyorwa kwa makosa, kwavile eneo hilo lilikuwa la Kampuni hiyo. Waziri Anna Tibaijuka anakiri kwamba aliwaombea Wasukuma Serikalini wakapewa uhamisho kwenda Buligi, na kwamba yeye mwenyewe aliwasaidia hata usafiri wa kuhamia Buligi. Wazalishaji wa Kisukuma waliongezeka huko Buligi, baada ya ndugu zao waliokuwa wamewaacha nyuma kuvutiwa na ushuhuda mwema wa uzalishaji wa wenzao waliotangulia huko, baada ya mageuzi ya eneo lililokuwa ‘Kosovo’ kuwa paradiso ya amani na maendeleo. Ni kweli kwamba Wasukuma walipofika uhamishoni Buligi, kwa uhodari wao katika uzalishaji na umahiri wao katika ulinzi wao wa jadi, waliigeuza ‘Kosovo’, ikawa kihenge cha chakula cha Mkoa wa Kagera, wakizalisha mpunga, mahindi, maharagwe, dengu, mtama, ngano, uwele, mihogo, migomba, viazi ulaya, vitunguu, nyanya, mboga na hata miti kwa ajili ya hifadhi ya mazingira, kwa kadri walivyoshauriwa kitaalamu. KWAHIYO ukweli hauwezi kukwepeka kwamba :
1. Uchomaji wa nyumba zaidi ya 500 za wananchi wa kabila la Wasukuma katika maeneo ya Buligi na mengineyo kwa kisingizio cha ‘Operation Okoa Mazingira’ ulilenga kuwaangamiza Wasukuma pamoja na mazao yao tele waliyokuwa nayo majumbani mwao pamoja na mali zao zingine zote.
2. Huko Buligi na maeneo mengine ambako Wasukuma wanazalisha kwa wingi mazao hayo yote, Wasukuma waliletwa na Serikali, si wavamizi.
3. Wasukuma hawakuvamia mapori ya Wanyarwanda au ya mtu mwingine yeyote. Kwani Vijiji vyote wanavyoishi vinawatambua, hata kwa mchango wao mkubwa sana katika uzalishaji.
4. Wasukuma hawajaingia katika Hifadhi ya Taifa, wala hawana ng’ombe hata mmoja katika Hifadhi, bali Wanyarwanda ndio wenye mamia ya maelfu ya ng’ombe katika Hifadhi, ambamo hata wanyamapori wetu Wanyarwanda wamewamaliza. Wanyarwanda huhonga mamilioni ya fedha na ng’ombe kwa maafisa wa wanyamapori na watumishi wengine wa umma. 5. “Operation Okoa Mazingira” haikulenga wahamiaji haramu ambao ni Wanyarwanda, wala mamia ya maelfu ya ng’ombe zao kutoka Rwanda na Uganda hususan katika Hifadhi ya Taifa, kwa sabau Wanyarwanda hawakuguswa kabisa, bali walikuwa wakishangilia wanavyofanyiwa unyama Wasukuma, ambao wala hawana ng’ombe katika Hifadhi kunakoharibiwa mazingira!
6. Nyumba za Wasukuma zilizoteketezwa hazikuwa katika Hifadhi, bali katika vijiji na vitongoji rasmi vyenye serikali halali za Vijiji na Vitongoji. Mfano ni nyumba 105 za Kishonga B Barabara ya 9, katika Kijiji cha Nyamilanda Kitongoji cha Nyakabingo, na Kijiji cha Itunzi Kitongoji cha Miziro. Wenyeviti wa Vijiji vya Nyamilanda na Itunzi ni mashahidi, na wanalalamikia unyama wa kuchomewa nyumba wananchi wao.
7. Uteketezaji wa nyumba za Wasukuma uliambatana na unyang’anyi wa pesa zao, kuanzia shs 100,000/- hadi shs 4,000,000/- kwa Msukuma mmoja, na kuwapa stakabadhi feki zilizoandikwa “WAZABUNI WA MASOKO/ MIALO/VIVUKO. Eti ADHABU kwa ajili ya hatia zilizobuniwa zikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira, kufyeka misitu ovyo, zingine ziliandikwa ‘Kusafirisha mifugo bila kibali’ Tunaambatanisha vivuli vya stakabadhi feki zilizotumika (Nambari 135559, 135519, 135562, 135356, 135520,135367). Tena walipora mapesa mengi sana kuliko waliyoandika katika stakabadhi, na walio wengi hawakepewa hizo karatasi! Huu ni unyang’anyi na ujambazi wa wazi kabisa! Tunawaachia kazi DCI na Takukuru.
8. Maelfu ya wananchi waliofanyiwa unyama huu walilundikana makanisani, kwa ndugu zao na marafiki zao, na wengi walilazimika kuishi maporini, ambako wanawake wapatao watatu walijifungua kama wanyamapori.
9. Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lemberis Kipuyo, ambaye alikuwa ameonwa na Mnyarwanda aitwaye Athanas Habamungu Kafurama, na kibaraka wa Wanyarwanda ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana aitwaye Julius Rwechungura, baada ya kuchangwa shilingi milioni 100 katika kikao cha Wanyarwanda katika kanisa lao la Butera tareke 31/10/2012, kulingana na majigambo ya Wanyarwanda na Kafurama mwenyewe, ndiye aliyeonekana kusimamia unyama huo, ingawa yeye ndiye mwangalizi wa amani na usalama katika Wilaya!
10. Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu unyama huu wa kutisha, alikiri kwamba wamechoma moto nyumba eti zilizokuwa katika Hifadhi, eti kwa ajili ya kulinda mazingira ya Mkoa wa Kagera na kuhamisha wahamiaji haramu wanaoingia na makundi makubwa ya ng’ombe katika Hifadhi.
11. Kama alivyoeleza Lemberis Kipuyo, unyama huo wa kutisha uliosukwa na Wanyarwanda na kutekelezwa kwa usimamizi wake yeye mwenyewe Mkuu wa Wilaya, ulianza tarehe 3/11/2012 saa 3 asubuhi katika eneo la Buligi. Na kama alivyosema hata yeye Mkuu wa Wilaya, maharamia waliowafanyia wananchi wa kabila la Wasukuma unyama huu ni: Askari wa Jeshi la Polisi Usalama wa Taifa Takukuru Wafanyakazi wa Idara ya Misitu Wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Wanyamapori, ambao baadhi yao walitambulika. Askari wa Jeshi la Ulinzi, waliotambulika kwa sare zao. Maharamia waliovaa sare za Mgambo. Lemberis Kipuyo alisema walikuwemo pia Wanasheria katika unyama huu.
12. Wananchi waathirika walipokusanyika Kituo cha Polisi Miziro, Mkuu wa Wilaya Lemberis Kipuyo alifika hapo. Lakini alipoombwa afike ajionee makazi ya wananchi wake yalivyoteketezwa, aliwapuuza isivyo kawaida hata kibinadamu, ingawa umbali haufiki hata kilometa! 13. Kwa kuhofia makusanyiko ya vilio vya Wasukuma, jasusi Mnyarwanda Athanas Kafurama alikwenda kumchochea Mkuu wa Wilaya azidishe unyama kwa madai kwamba eti Wasukuma wamejiandaa kuvamia Kituo cha Polisi Miziro. Ndipo unyama ulipozidishwa maradufu kuwaangamiza Wasukuma, na kuwawinda wale wote wanaoogopwa kama waelewa, na wengi ikawabidi kukimbilia maporini na kuishi huko kama wanyamapori licha ya mvua nzito.

WANYARWANDA WALIVYOIPINDUA OPRESHENI DHIDI YAO
(Kwa kuwageuzia kibao hicho Wasukuma)
Wanyarwanda walipoijua ‘Opresheni Okoa Mazingira’ kwamba imeandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwatokomeza wahamiaji haramu yaani wao, na kwavile waliwashika mkononi viongozi wote kuanzia Mkuu wa Wilaya kama walivyokuwa wanajigamba, na kama walivyokuwa wanajihami kwa rushwa kwa uharamia wao wote wanaoifanyia Nchi yetu, ndivyo walivyojipanga kuwatoa kafara Wasukuma Serikali yetu ilikuwa na taarifa zote za mikakati ya dikteta Kagame na Museveni juu ya Nchi yetu, yaani uvamizi wenye lengo la kuiteka ardhi yetu kama vile wanavyofanya Congo Mashariki, uporaji wa raslimali zetu, na walivyohamishia mamia ya maelfu ya ng’ombe zao katika Hifadhi za Taifa letu na utekaji wa ardhi ya wananchi, na hata kulisha mifugo yao katika mazao ya wananchi, wakitetewa na vibaraka wao ambao ni viongozi wetu wala rushwa.
Wamiliki halisi wa haya mamia ya maelfu ya ng’ombe ni marais na mawaziri wa Rwanda na Uganda, ambao wanayo mahusiano ya kifisadi na viongozi wetu mafisadi au Watusi kama wao. Ndiyo maana azma ya Serikali yetu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ imekuwa ikipozwa kwa ufisadi kwa muda mrefu, huku maadui wakizidi kujichimbia na kuangamiza mazingira.
Lakini kwa nguvu ya wale viongozi wetu waliobaki na uzalendo, Serikali yetu ilikazana na mpango kabambe wa OPERATION ‘OKOA MAZINGIRA’, kwa ajili ya kutokomeza kabisa uvamizi wa Watusi katika Nchi yetu (wahamiaji haramu), na kutowesha ng’ombe zote zilizoingizwa katika Nchi yetu, zenye kuhatarisha uhai wa vizazi vyetu vijavyo kwa kuharibu vibaya sana mazingira.
Kilio cha wananchi juu ya uvamizi wa ardhi yetu na kuingizwa maelfu ya ng’ombe katika Nchi yetu kutoka Rwanda na Uganda kilianza mwaka 2009. Wanyarwandawalipopata taarifa juu ya ‘Opresheni Okoa Mazingira’ dhidi yao, walifanya mikutano kadhaa mizito katika kanisa lao la Butera, linaloongozwa na Mtusi wa hatari aitwaye Augens. Tawi la kanisa hilo liko Chanyamisa, Karagwe, ambako pia linatumika kwa mikakati hii ya Kagame.
Opresheni Okoa Mazingira iliyokusudiwa kutokomeza wavamizi wa Nchi yetu na maelfu ya mang’ombe yao yanayoharibu mazingira ya Nchi yetu, iligeuzwa na walengwa, Wanyarwanda, kuwa unyama wa kutisha wa kutowesha katika eneo hilo wananchi wa kabila la Wasukuma, na kuwapora mali na ardhi wanayozalishia mavuno yaliyotia fora katika mkoa wa Kagera.
Katika kuwatwika Wasukuma dhoruba ya ‘Operation Okoa Mazingira’ ambayo iliwalenga wao, Wanyarwanda walianza kwa kuwachonganisha kirahisi kabisa Wasukuma na ndugu zao Wahaya; Kwavile Mhaya mwenye kulima ekari nne au tano ndiye aliyeonekana kuwa mkulima stadi, lakini Wasukuma wakawa wanalima ekari mpaka 50 mkulima mmoja, Wanyarwanda walitumia kwa ufundi wao kigezo hicho kupandikiza mbegu ya kijicho miongoni mwa Wahaya, ambao wamekuwa wepesi kukabidhi kwa Wanyarwanda ardhi yetu.
Hatimaye baadhi ya Wahaya walianza kuwanyoshea kidole Wasukuma kwamba eti wanakamata ardhi kubwa kuliko wao, ingawa mapori hayo yalikuwa yanakaa bure tangu uumbaji mpaka Wasukuma walipoyavamia kwa uzalishaji wa nguvu, hata wakawa wakivuna magunia ya mpunga mpaka 700 mkulima mmoja. Kwa hila za Wanyarwanda, Wahaya wa Muleba na sehemu zingine zilizofanyiwa kazi ya ufitini na Watusi, walianza kujikusanya vikundi vikundi kuandika barua za kuomba ardhi hiyo wanayozalishia Wasukuma, ili mashamba ya Wasukuma yamegwe na kupewa wao, kusudi Wanyarwanda wajipatie kutoka mikononi mwa Wahaya, ambao Watusi wanawachukulia kuwa wepesi zaidi wa kuwapasia wao. Kwa kuwatumia vibaraka wao kama Julius Rwechungura ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisana, Wanyarwanda siyo tu wameteka mamia ya ekari za ardhi yetu, bali wamekuwa wanapiga vita siku zote ya kuwafukuza Wasukuma ili wakamate wao maeneo yote.
Uharamia huu ndio uliopelekea Mkurugenzi wa Wilaya kumwamuru Afisa Mtendaji Kata ya Kyebitembe kuitisha mkutano wa tarehe 27/3/2012 kuhusu malalamiko ya Wasukuma dhidi ya Wanyarwanda. Mkutano huo ulipiga marufuku kumega ardhi yoyote inayotumiwa na wananchi wa kabila la Wasukuma, kwa ajili ya mapinduzi ya uzalishaji waliyofanikisha katika mkoa, walioingia katika maeneo hayo
...
 
BAADA ya kutokea kifo cha Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila maeneo ya Msolwa, Chalinze, mkoa wa Pwani, kuliibuka hisia nyingi kutokana na chanzo cha kifo hicho, ifuatayo ni taarofa ya jeshi la Polisi mkoa wa Pwani:-


TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA



Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni "B" Dar Salaam.

Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.

Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.

Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.

Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.

Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.

Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:


  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.


Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.
 
Polisi muwe mnafanya hivi kila mara, tusisikie tuu uchunguzi unaendelea, bravo
 
BAADA ya kutokea kifo cha Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila maeneo ya Msolwa, Chalinze, mkoa wa Pwani, kuliibuka hisia nyingi kutokana na chanzo cha kifo hicho, ifuatayo ni taarofa ya jeshi la Polisi mkoa wa Pwani:-​
TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA
Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.
Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.
Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.
Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.
Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.
Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.
Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.
Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:

  1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.
  2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.
  3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).
  4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.

Rip Mtikila Hujafa hujaumbika ,w engine tujiandae haijalishi uzima wetu mwenye mali akitaka roho yake aweza ichukua sekunde yoyote
 
Back
Top Bottom