Elections 2010 Mchakato majimboni TBC1 Jimbo la Kigoma Kaskazini

Elections 2010 Mchakato majimboni TBC1 Jimbo la Kigoma Kaskazini

Zito anashangiliwa sana inaonesha ana mashabiki wengi
 
Zito anawashushua ccm hapa kuhusu lami. Kajipanga kweli. Kasema iweje serikali isubiri zito awe mbunge ndipo wajenge lami. Walikuwa wapi tangu uhuru??!!
 
Inavyoonekana hamna tena haja ya mdahalo kigoma kaskazini. Zito kafunika. Hata slaa huko alipo anatabasamu
 
Zito anawashushua ccm hapa kuhusu lami. Kajipanga kweli. Kasema iweje serikali isubiri zito awe mbunge ndipo wajenge lami. Walikuwa wapi tangu uhuru??!!

zitto kavunja rekodi....na ni dalili nzuri ya kushinda kwani jamaa anakubalika
 
Mchakato ndio huo uko hewani, Zitto anafunika bovu, japo nahisi amewahamashisha mashabiki wake hivyo wamejaa kibao na kumshangilia kimpira mpira ile ya Ziitooo!..Ziitooo! Ziitooo! kelele kibao.
 
Katika kipindi cha TBC1 cha Mchakato Majimboni, mgombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametia fora na kuwapiku wagombea wenzake huku akishangiliwa na watu waliofurika kwenye ukumbi ambapo kipindi hicho kilirekodiwa na kurushwa hewani, kuanzia saa 3 usiku, Jumamosi, Oktoba 2, 2010.

Kabwe alijieleza vema kuliko kila mgombea na kudhihirisha kwamba CHADEMA bado inakubalika, na ina mipango dhahiri ya kuliendeleza jimbo hilo, mojawapo ya mipango hiyo ukiwa ni ule wa kuileta kampuni inayosimamia masuala ya reli nchini Ujerumani, kuja kusimamia uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania, kwa msaada, kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, kwa muda wa miaka miwili.

Zitto alisema: Sio kwamba tutafanya nini, ni kwamba, tunafanya nini. Tupendi nafasi tuweze kuendelea kutekeleza mipango yetu ambayo tayari imeonekana.

CCM na vyama vingine vitapaswa kufanya KAZI YA ZIADA kumwondoa Zitto kwenye jimbo hilo! Ama kweli, ni KAZI NZITO kumwondoa ZITTO kwenye jimbo hilo!

-> Mwana wa Haki
 
Huyu wa appt inaonekana kakurupushwa kuja kwenye mdahalo
 
amejibu swali la walemavu vizuri sana....

ila tatizo la zito ni time management!
 
Huyu jamaa mwingine wa appt sijui vp kwani ni mchemfu sana ......anakiaibisha sana chama chake!
 
kweli hayo mapandikizi ya ccm hayawezi kusoma alama za nyakati?ona yanavyopata aibu kwenye mdahalo
 
jamaa wa cuf alianza vizuri lakini sasa anaharibu, anawakataza watu kushangilia
 
Huyu wa cuf kaona jambo muhimu kwa walemavu ni choo tu. Dah!
 
Mchakato ndio huo uko hewani, Zitto anafunika bovu, japo nahisi amewahamashisha mashabiki wake hivyo wamejaa kibao na kumshangilia kimpira mpira ile ya Ziitooo!..Ziitooo! Ziitooo! kelele kibao.

Vipi amempigia kampeni Dr. Slaa?
 
Mkutano wa Kumi na Nne Kijiji cha Matyazo, Kata ya Kalinzi, Kigoma Kaskazini

1a1.jpg
1matyazo.jpg

212.jpg
49.jpg

57.jpg
69.jpg

77.jpg
87.jpg

96.jpg
106.jpg

125.jpg
 
Mkuu nina maswali mawili juu yako:-

1. Ni kweli unampango wa kugombea urais mwaka 2015?
2. Vipi mbona haufanyi kampeni za Mgombea urais wa Chadema Dr Slaa?
3. Ni kweli kuwa wewe na Dr Slaa hampikiki chungu kimoja (hamuivi)

Asante.

BNN
namsaidia kujibu
1.hana mpango wa kugombea urais 2015 kwa sababu atakuwa hajatimiza kigezo cha umri
2.anafanya kampeni za chadema, alikuwa kibaha, lindi, mtwara
3.si kweli
 
namsaidia kujibu
1.hana mpango wa kugombea urais 2015 kwa sababu atakuwa hajatimiza kigezo cha umri
2.anafanya kampeni za chadema, alikuwa kibaha, lindi, mtwara
3.si kweli

yatosha, kaka
 
CUF hawana kitu jimbo la kigoma kaskazini.......mgombea wao hawezi kabisa kujenga hoja!

Zitto jimbo ni lako mkuu!!!!!!
 
Back
Top Bottom