Mchakato wa ajira za ualimu mwaka 2025 si wa haki, umekaa upendeleo

Bodaboda hakosi elfu 30 Kwa siku Kwa mwezi laki 9
Na huyo boda yupo Dar anakunywa Pepsi ya baridi, mwalimu umepangiwa machakani Tandahimba unakunywa togwa
Wangekuwa wanapata kipato kizuri hivi wangebadili maisha yao.

Sikubaliani na maslahi ya walimu, lakini pia mtaa siyo rahisi kama unavyojaribu kukokotoa hivi.
Si ajabu wewe mwenyewe bado hujaanza kujitafutia fedha.
 
Kwa hiyo kada zingine wanaofanya mtihani? Hivi utawapaje ajira walimu 200 kati ya walimu 2000 bila usahili?
Kwa namba uliyoandika hapa, wala hakuna shida.
Tatizo ni kufanyisha usaili watu 25,000+ kwa ajili ya kupata watu 200.
Kuendesha zoezi hili nchi nzima ni kutumia kodi zetu vibaya.
Na, pia, kulitakiwa kuwe na mfumo unaochuja candidates ili kupata orodha fupi ambao ndiyo watafanyiwa usaili.
Kati ya watu 30,000 wanaotaka ajira nchi nzima ilhali wewe unahitaji watu 300, punguza hadi wafike 2,000.
Simple tu.
 
Mkuu embu shauri ni mbinu gani itumike kuchuja watu 30,000 wenye sifa sawa ili kupata watu 2,000 tofauti na hii wanayotumia PSRS.
 
Mkuu embu shauri ni mbinu gani itumike kuchuja watu 30,000 wenye sifa sawa ili kupata watu 2,000 tofauti na hii wanayotumia PSRS.
Huwa wanatumia mbinu gani kupata short lists za candidates wa kada nyingine?
 
Acheni kulalamika walimu, kada nyingine wanafanya hivyo tangu kitambo. Pambana na umasikini wako
 
Hawa jamaa ni miongoni mwa taasisi chache Tanzania ambazo zinaongozwa kwa weledi na utashi nawakubali sana
 
Utakuwa mmoja wapo wa wanufaika wa mfumo huu wa hivyo.
 
Saili ya geo maswali mengi yalikuwa ya kukariri na sio kuelewa tofauti na wale wa diploma wao ulikuwa unaeleweka, nadhani serikali haitaki watu walomaliza zamani tuangalie tu shughuli nyingine za kufanya, hapa nichome tu kadi zao za ccm niingie rasmi chadema niwe mpiga kampeni huko
 
Kabisa mkuu. Haya Ma CCM yanaroho mbaya balaa. Halafu yanaomba ridhaa ya kuongoza nchi Kwa mara nyingine. Nakwambia tofauti na wao wanufaika wa huu mfumo wa ulaghai na wa kidharimu, hakuna atakaempigia kura mgombea wa CCM.
 
Huwa wanatumia mbinu gani kupata short lists za candidates wa kada nyingine?
Kwahiyo unatoa ushauri wa kitu usichojua?

Mbinu wanayotumia jamaa ni kuwafanyisha usaili wa mchujo waombaji wote waliokidhi vigezo vya kazi husika wanaofaulu ndio wanaenda kwenye Usaili wa mahojiano kwa uwiano wa 3:1.

Sasa wenzentu mnaopinga mnaombwa mtoe mbinu mbadara ambayo itakuwa fair zaidi sio kuishia kukosoa bila kutoa solution.
 
Wewe, maHR na hiyo sektetarieti mnazijua mbinu hivyo mimi sina haja ya kuwapa ushauri.
Na hiki kinachoendelea ni siasa tu kuonesha kuwa mchakato ulikuwa jumuishi.

Nikuulize, unafahamu lengo la mwajiri kutaka vyeti vya candidates?
 
Bodaboda hakosi elfu 30 Kwa siku Kwa mwezi laki 9
Na huyo boda yupo Dar anakunywa Pepsi ya baridi, mwalimu umepangiwa machakani Tandahimba unakunywa togwa
Umekomaa sana kusema machakan Tandahimba,hvi ushawah kufika Tandahimba huko unakokuita machakani?
 
Kabisa mkuu. Haya Ma CCM yanaroho mbaya balaa. Halafu yanaomba ridhaa ya kuongoza nchi Kwa mara nyingine. Nakwambia tofauti na wao wanufaika wa huu mfumo wa ulaghai na wa kidharimu, hakuna atakaempigia kura mgombea wa CCM.
We nae ccm Ina Wanachama wengi sana usipo piga kula wewe mwingine ata piga ccm dude Moja kubwa sana mizizi yake ipo chini sana
 
Term hii ni nyumba Kwa nyumba. Utajua hujui
 
Waalimu endeleeni kuwa wavumilivu 😂

Your browser is not able to display this video.
 
sasa mkuu kama hujasoma guidance and counseling umekuwaje mwalimu?.
 
sasa mkuu hata weww ungepewa ufanye hilo zoezi ungefanyaje tofauti na kuwafanyia waombaji usaili.
kumbuka kila mtu ana sifa stahiki sasa utachukua vigezo gani kuwachuja bila kufanya usaili ili kuwapata walio bora zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…