Mchambue marafiki; kuna wa maendeleo na wa misiba na mazishi tu

Alikumbatia sanaa ukabila undugu na schoolmate, akatudharau sie watu baki alio tukuta mjini tukafanya kazi nae, ni mara ya kwanza tumeweza kujua kwake kama kikundi alikua hajawahi kutupeleka kabla ya kuugua.
 
Mtoa mada iko hivi. Maisha yana nyakati. Siku ukiwa na hela ama nafasi kubwa katika taasisi hata huhitaji kutafuta marafiki wa kukuchangia, wao ndio huwa wanajileta kukuchangia pesa nyingi nyingi tu. Na hii hua si kwa upendo bali kwa matarajio kuwa utawakumbuka siku wakija kwako na maombi binafsi. Wewe huyo huyo ukifulia ama kutumbuliwa hao hao uliodhani na marafiki waliokwisha wahi kukuchangia pesa nyingi hutawaona hata ukiwa na shida ya milioni moja ama ya kufa.
 
Yani wanaomjua wametoa vielf 30 sie tusiomjua ndo tutoe laki laki

Unaomba msaada kwa lugha ya dhihaka eti marafiki wengi mama ntilie, bora uwe nao 5 wa maana kawafate hao sasa, upumbavu tu
Mkuu unatoa kwa ajili ya Mungu wako sio mpaka mtu umjue kabisa, mimi ni mechiangia 2m ila sina vinasaba nae tumekutana tu kwenye hizi kazi mjini, toa mungu atakurudishia mwoyo wakutoa kama unao toa tu.
 
Alikumbatia sanaa ukabila undugu na schoolmate, akatudharau sie watu baki alio tukuta mjini tukafanya kazi nae, ni mara ya kwanza tumeweza kujua kwake kama kikundi alikua hajawahi kutupeleka kabla ya kuugua.
Kamsimange mgonjwa sio waliotoa vielf 30 vyao, adabu huna
 
Mkuu unatoa kwa ajili ya Mungu wako sio mpaka mtu umjue kabisa, mimi ni mechiangia 2m ila sina vinasaba nae tumekutana tu kwenye hizi kazi mjini, toa mungu atakurudishia mwoyo wakutoa kama unao toa tu.
Unamjua si ni mwanakikundi chenu, braza mbinu yako imekaa kimchongo, hamna watu wagumu kutoa hela km humu jf tena ukiongeza na uzi wako ulivyojaa jeuri na dhihaka ukipata hata laki njoo nikuongezee nyingine
 
Mkuu unatoa kwa ajili ya Mungu wako sio mpaka mtu umjue kabisa, mimi ni mechiangia 2m ila sina vinasaba nae tumekutana tu kwenye hizi kazi mjini, toa mungu atakurudishia mwoyo wakutoa kama unao toa tu.
Mkuu unadharau aise bandiko lako naamini nimekera kila aliyelisoma nami nikiwa mmoja wao
 
Mkuu unadharau aise bandiko lako naamini nimekera kila aliyelisoma nami nikiwa mmoja wao
Mkuu lengo sio kukera watu ni kujifunza kitu katika matukio mengine, lazima tujifunze, na mimi nilikereka sanaa baada ya kuona ndugu zake na marafiki hata 15m wameshindwa kufikisha.....
 
Mkuu lengo sio kukera watu ni kujifunza kitu katika matukio mengine, lazima tujifunze, na mimi nilikereka sanaa baada ya kuona ndugu zake na marafiki hata 15m wameshindwa kufikisha.....
Naweza kukubaliana nawe kuwa una hoja una jaribu kujenga lakini bado kutaja watu kwa makundi yaani unaposema polisi mamantilie manesi na walimu umezingua sana kiufupi umetudharau wengine ambao tupo kwenye makundi hayo SIJUI UNAELEWA TAJIRI?????
 
Nachelea kusema huna busara. Yaani unaonekana kuwa kwako na vihela unadharau sana wasio na kipato kama chako. Watu wanajaribu kukueleza lakini inaonekana umeshupaza shingo.

Ubaya Ubwela Undungu Umala
 
Naweza kukubaliana nawe kuwa una hoja una jaribu kujenga lakini bado kutaja watu kwa makundi yaani unaposema polisi mamantilie manesi na walimu umezingua sana kiufupi umetudharau wengine ambao tupo kwenye makundi hayo SIJUI UNAELEWA TAJIRI?????
Basi utanisamehe kwa hilo kama kuna kundi nime litaja na limekuumiza, ebu niende ku-edit nitowe huo makundi ya watu, ila na omba mnielewe hoja yangu ya watu kutojua watu muhimu wa kuwa saidia na kukumbatia ndugu na rafiki wasio kua na uwezo na roho ya kutoa.
 
Pole sana kwa jamaa. Ila usiwalaumu sana, Wengine tunaishi kwa kubahatisha sana leo hii nikipata hiyo changamoto sioni uwezekano wa kuipata hiyo 210m. Ni Mungu tu anatulinda na kutufichia aibu.
 
Wengine ndio wanategemewa wawavushe ndugu na jamaa kwenye majanga,Sasa wakiumwa ndo inakuwa hivyo....tofauti na familia za kiarabu au kihindi wao cycle Yao ni nzuri karibu wote wana mawe. Sisi huku unakuta ukoo mzima don ni mmoja tu...cha muhimu ni kwamba maisha yanahitaji nidhamu sana hasa namna ya kuishi maana mambo ya kusema Kila mmoja atakufa ni kujifariji.
 
Mkuu usidharau michango ya watu ata 10,000 ni hela pia,Kuna watu ni mabilionea lakini ata kutoa 100k hawezi.
Mimi mwaka juzi niliuguliwa na mwanangu alilazwa Bugando miezi 3 na mimi nilikua nimetumia pesa yote,nilimpigia Kaka yangu wa tumbo moja aniazime siyo anipe,na wakati huo alikuwa ametoka kuuza kiwanja 30 milioni!!
Lakini aliniambia hana,huyo ni ndugu kabisa sembuse mtu baki!
 
Daaa Mungu atusaidie
 
Kwa mchango gani ? Inategemea na wewe upo level gani kwa sababu kama kipato chako kikubwa utakuwa una'mingle na watu wa juu .

Sisi harusi tu hapa ofisini mchango unagonga mpaka 18 mil tena normal sana .
 
Pole sana kwa jamaa. Ila usiwalaumu sana, Wengine tunaishi kwa kubahatisha sana leo hii nikipata hiyo changamoto sioni uwezekano wa kuipata hiyo 210m. Ni Mungu tu anatulinda na kutufichia aibu.
Mkuu ahasante kwa kweli ukiwa na uhai na afya njema mshukuru sana Mola wako ndo utajiri wenyewe, sio wewe tu, hata mimi nikikubwa na tatizo kama hilo 210m nikiipata ila ntakosa makazi na gari ntauza kila kitu, manaake siwezi kukaa mjini tena loh, kweli "afya ni mali"
 
Kama alikuazima mshukuru sanaa Mungu.wengine ndugu ni mtihani, kutoa pesa sio rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…