Mchambuzi Edgar Kibwana wa CMG kama Kiingereza chako ni cha Kubabaisha kama Changu uwe unatumia Mbinu hii ili Usikikosee na Usishtukiwe kuwa hukijui

Mchambuzi Edgar Kibwana wa CMG kama Kiingereza chako ni cha Kubabaisha kama Changu uwe unatumia Mbinu hii ili Usikikosee na Usishtukiwe kuwa hukijui

Kuna mmoja nimemsikiliza sasa hivi baada ya mpira kumalizika kati ya KMC na AZAM nimekaa na mtoto wangu kasema huyu Mlimila hajui Kiingereza.

Kwenye sport wamejaa wajinga wengi sana Kitenge and Compay.
HAA Kitenge Group Wao Wanaunganisha Tu Hata Kama Haileti Maana
 
Ukikutana na Mgeni hasa Mzungu au Mmarekani Mweusi halafu ukataka kufanya nae Mahojiano basi hakikisha Maswali yako yanakuwa ni mafupi mafupi na ya moja kwa moja sawa?

Muda mfupi uliopita nimekusikia Sports Extra ya Clouds FM ukitumia dakika 5 nzima Kuzunguka Kuuliza Swali la Sekunde 10 au 15 tu huku Ukichapia mno hadi Redio yenu nayo ikazima ghafla.

Kama Wakufunzi wako wa Chuo Kikuu ulichosoma ( UDOM UNIVERSITY ) kama sijakosea kama nao Walikusikiliza nina uhakika watakuwa si tu Wameumia bali watakuwa Wamekasirika mno kwa Kiingereza chako kibovu, cha Kujitafuta na cha Kubabaika.

Na uliponiacha hoi ni pale na Wewe ulipojifanya unaongea Kiingereza cha Kimarekani kwa Kuwaiga Wageni waliokuwepo Studio wakati ukikiharibu kwa Broken yako.

Nilijua nisiyejua Kiingereza Tanzania nzima ni Mimi tu GENTAMYCINE kumbe nina Mwenzangu ( Pacha wangu ) Edgar Kibwana Mchambuzi wa Mpira wa Miguu Clouds FM na Clouds Tv.

Pongezi nyingi kwa Mtani wangu wa Kiha ( kutoka Mkoani Kigoma ) Mtangazaji Prisca Kishamba ambaye Yeye kwa kujua hakijui Kiingereza ( japo anakipenda sana ) aliamua kutokuwa muuliza Maswali ya Kiingereza kwa Wageni na kukaa Kimya na hata Maswali Mawili ya Kiingereza aliyojitutumua Kuyauliza mwishoni alionekana kuwa alitumia muda mrefu Kuyakariri ( Kuyameza ) na aliyauliza kwa haraka sana utadhani kuna Mtu alikuwa anamdai Fedha hivyo anaogopa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu kwa kuchomekea vineno vya kiingereza(kiswanglish) hawa watangazaji wa michezo unaweza kusema ung'eng'e umejaa sema tu anawatangazia wabongo wenzie kumbe hamna kitu.

Sema hata hivyo huku kuendelea kuchekana kwa kukosea kuongea kiingereza bora tungeacha tu maana inajulikana hii lugha ni changamoto kwetu uwe na elimu au usiwe na elimu, sasa kuendelea kuchekana haina maana yeyote.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna mmoja nimemsikiliza sasa hivi baada ya mpira kumalizika kati ya KMC na AZAM nimekaa na mtoto wangu kasema huyu Mlimila hajui Kiingereza.

Kwenye sport wamejaa wajinga wengi sana Kitenge and Compay.
Jamani usimwite mtu ni mjinga kwasababu tu hawezi kuongea kingereza kama cha Harry Kane!
 
kwamba amesoma UDOM UNIVERSITY..

Dah brother na wewe hapa umeliwa kichwa na mwalimu Antonnia kwenye module yake ya Communication Skills.
Wee Excel Module ndio nini kwanii??🤠
Mie chuo sijafika mwenzio!
Napasikia tu kwenye Tv na mitandao kama hivi!😁
 
MTU Kama kasoma dumu fagio inamuhitaji miaka 15 tangu amalize chuo kikuu kujua kiingereza Kwa ufasaha
Na bado inaweza isitoshe pia. Kuna wakati nilikuwa naenda kujifunza vitu fulani vya sanaa pale international school of tanganyika, nahisi kama ningefanya vile kwa miaka mitano mfululizo basi sasahivi ningekuwa natema yai kama mtu wa Birmingham 😂
 
U

Upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom