Mchambuzi gani wa soka unamkubali hapa Tanzania?

Mchambuzi ambaye kazi yake ni kusema mchezaji au kocha fulani ni rafiki yangu niliongea naye. Huyo ni maji taka.

Tunataka mchambuzi anayeongelea formations na sababu zake. Wapi makosa yametokea hadi goli kupatikana. Timu ipangwe vipi au kupata matokeo.
Aeleze aina ya sub na potential impact yake.
Sasa wengi wao wamegubikwa na unazi wa timu zao. Utasikia leo lazima tutoke.
 
Nimejaribu kuwafuatilia wachambuzi wengi waliokuja nyuma ya Dr leaky lakini bado sijaona wakumfikia. Dr leaky anakuchambulia mpira kwa lugha ya kiswahili na kila kitu unakielewa kuanzia formation,na vingine vyote.

Hawa wachambuzi wetu wakisasa wao kwakua wanajua yes na no basi kutwa nzima ni kuchanganya lugha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi sana,mie kashasha ni bora.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo uchambuzi ,utakua mchambuzi gani hujui history zaclub au timu zaTaifa zinachocheza.Dr huchambua mpira nakukatia historian siohawa waleo

Sent using Jamii Forums mobile app
Yule sio mchambuzi wa soka, ni mtoa historia ya matukio , vituko na vichekesho vya vinavyohusu soka, timu za soka na wanasoka..
Kwa hayo hana mpinzani toka enzi hizo hadi sasa.
 
Amri Kiemba anajua sana mambo ya kiufundi, kibiashara, na kisaikolojia ktk soka.
Nahisi akiwa kwenye timu nzuri ya ufundi akasikilizwa kama vile Klopp anavyo wasikiliza wasaidizi wake watajenga timu bora sana.
 
Mm niliacha kunisikiliza magic baada ya kununuliwa na CCM,nilikuwa sikosi kipindi Cha asubuhi morning magic
George namwelewa sana, sipatagi muda sana wa kusikiliza radio au kuangalia TVs, ila kwa kiasi ninachosikiliza, inatosha kujua kwamba jamaa yuko miles nyingi mbele ya wenzake.

Toka ameondoka Magic sijawahi tena kuisikiliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kazi ndo anaifanya baba g hapo wasafi msikilize kidogo siku moja utakuja kusema hapa
 
yupo wasafi huko naskia sasa hivi, kafuata malipo mazuri itakuwa

Yes, mara chache nimemsikia. Juzi kwenye buildup ya Liverpool vs Sheffield United nilimsikia na hata buildup ya Leicester vs Liverpool nilipata muda wa kumsikiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…