Umetumia lugha kali sana.
Hawa wachambuzi wa mpira hawajasomea popote, ni ufatiliaji tu, kuangalia wengine wanachofanya, kusoma tactics mbalimbali kwenye mitandao ya wenzetu, na pia kuwa na akili ya kufanya presentation. I mean kufikisha ujumbe kwenye hadhira na ujumbe ukaeleweka.
Ndiyo maana hawa wachambuzi unaweza kumkuta anakosoa mbinu za kocha, siku yeye akipewa timu anaboronga.
Mfano wa hivi karibuni ni Gary Neville, alipewa timu ya Valencia, angalia alifukuzwa baada ya games ngapi. Lakini ni pundit mzuri sana.
Thierry Henry, wote tunaukubali uwezo wake kama mchezaji, na amekuwa pundit anayeheshimika na kulipwa hela nzuri, lakini performance yake kama kocha wote tumeiona.
Kwa hiyo wachambuzi ni kama sisi tu, wasikutishe.