Mjukuu wa Nassor
New Member
- Mar 17, 2025
- 1
- 0
Dharau, kejeli na majina mabaya kwa timu ya Mchangamdogo Senta ni moja ya changamoto inayorejesha nyuma juhudi za maendeleo kwenye timu hiyo. Ameyasema hayo Kocha na Kepteni wa timu Bimkubwa Maulid Othman Wakati wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi na kuongeza kua, kutokana na kutoungwa mkono jamii imekua ikiwaita majina mabaya na baadhi yao kukosa ridhaa kutoka kwa wazazi na wenza wao hali inayopelekea kutotimiza ndoto zao.
“ sisi wanawake ambao tumejitoa kushiriki kwenye michezo tumekua tukitafsiriwa vibaya na jamii na kama mimi mume wangu mwanzo alikua mgumu na alinikatalia hasaa ila baada ya kupata mafunzo kutoka @TAMWA_ Zanzibar (Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania_Zanzibar ) muelewesha akakubali ndio naendelea lakini bado jamii inatuangalia vibaya”Nao wachezaji wa kati (C) Amina Kudra Ali na Zaina Rashid Said Wamesema, mbali na majina mabaya lakini kutokua na vifaa vya kutumia kwenye mchezo huo kama jezi na mipira bado ni vikwazo kwao hali inayopelekea wanawake wengine kua na mwamko mdogo wa kushiriki kwenye mchezo wa mpira wa pete.“ tunacheza kwa jezi za kuazima uwanja pia hauna viwango lakini kwa vile tunaupenda huu mchezo tunajitoa , hivyo tunaziomba taasisi husika pamoja na viongozi kutuona kwani kwetu tunaona michezo ni ajira pia ni fursa na tunahisi tunaweza kuongeza kujulikana na kipato kupitia mpira wa pete”.Idrisa Maulid Othman mwenyekiti wa CHANEZA Wilaya ya Wete amesema mbali na kadhia hizo ila ukosefu wa ligi za kushiriki kupitia mchezo huo bado ni kikwazo na kuamua kushiriki kwenye mabonanza hali inayopelekea kukosa umahiri na ufanisi.“ kwa huku Pemba sijawahi kusikia ligi za mpira wa pete hata kwenye mapinduzi hatujaona na kutiokana na hali ya uchumi ya chama chetu kama wilaya inakua ngumu kuanzisha hivyo tunaishia kwenye mabonanza hali inayopelekea kukosekana umahiri kwani wachezaji wanakua hawapati uwanja mpana wa kuongeza wigo kutoka kwa wenzaiwao, mana unaweza kukuta kila baada ya miaka 2 au 3 ndio mabonanza yanaandaliwa lakini kama kungekua na ligi za wanawake kama mpira wa miguu ingesaidia sana”.alisema mwenyekiti.Afisa program ya michezo kwa wote kutoka TAMWA Khairat Haji Ali amewaasa wachezaji hao ,mbali na changamoto wanazopitia lakini wanapaswa kuendeleza juhudi na kutumia mafunzo walioyapata ili kutimiza ndoto zao.“sisi tumewapa mafunzo ni wakati wa kuyatumia ili hao viongozi wanaowalalamikia waweze kuona juhudi zao na kuwafikia aidha wanapaswa wao wenyewe kua na ubunifu zaidi wa kuangalia kipi kitaweza kutufikisha kwenye mafankio kwani sisi hata baada ya mradi tutaendelea kuwashika mikono kwetu kumalizika kwa mradi sio sababu ya kuwaacha” alisema Khairat Tathmini iliyofanywa Zanzibar na S4DA Umoja wa maendeleo ya michezo Afrika mwaka 2023 imeonesha michezo ni sehemu ya kazi..