Razima tuambizane ukweri maana msema kweri ni mpenzi wa mungu....................hiiiiiiiiiiii.Au nasema uongo....?!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Razima tuambizane ukweri maana msema kweri ni mpenzi wa mungu....................hiiiiiiiiiiii.Au nasema uongo....?!!!
Na ukijipeleka kusema una wapagaji watano au mita tono zitaondolewa kwenye kulipia 1000 ila lazima ulipe kodi ya mapato kutoka katika pesa za wapangaji!!Nyumba yenye wapangaji 5 kila mmoja atalipa kodi ya jengo asilomiliki
Apo inatafutwa kodi ya mapato kutoka kwa wapangaji pesa mwenye nyumba anazo pokea kutoka kwa wapanaji!!hapa kuna kitu iko imejificha, mfano nina nyumba ina wapangaji 3, na luku zinajitegemea....hao wapangaji wakilipa luku zote zinasoma jina la mwenye nyumba......ina maana wapangaji ndio watalipia jengo,,sawa...je itasomeka nina nyumba 3?.......kama sijaelewa....kuna kitu hapa italeta mgongano mkubwa sana....tusubiri tuone....je majengo yote yapo registered???? ..kuna kivuli cha dhuluma nyingine kinakuja....WATANZANIA zetu kelele tuu...tena kwa muda mfupi sana.....then we move on.........
Tupo tayari lakini vipi kwa wale watu wa hali ya chini? Umeshawafikiria hata kidogo?ahsante sana.
najisikia fahari kuijenga nchi yangu.
watanzania tupo tayari, kazi na iendeleee.
bado ni pagumu sana, sidhani kama wamejipanga vema......hapa kuna watu wasio na nyumba watalipia pango bila kupenda...tusubirie tuone...hii na TOZO NA MIAMALA haina tofauti....kila kona tutatachapwa.........fikiria unaishi nyumba uliyopangishiwa na serikali, ya kwako umempangisha HAJI MANARA.....wewe huku kila kitu serikali inamaliza..habari sijui umeme umeisha hunayo....kule kwa mpangaji ndie anaenunua LUKU.....atakaelipa kodi ya jengo ni nani......kuna kitu ndani ya kitu.....subiri tuone...na tulivyo na vilaza wengiii....endelea kusikilizia mdundo kwanza....Wamesema mwenye nyumba apeleke Luku hizo ziingizwe kwenye luku moja. Hakafu wapangaji hamtakiwi kulipa hii ni ya mwenye nyumba. Akigoma nendeni TRA(ila mnaweza kufukuzwa kwenye hio nyumba ha ha ha ha)
Kodi wanatembea na 21%Ukinunua Umeme utalipia Kodi nne:
1. VAT - 18%
2. Ewura - 3%
3. REA - 1%
4. Kodi ya Jengo (Tsh 1000- Tsh 5000)
Awamu ya sita, tozo ziendelee!
Kodi ya majengo iliwepo toka kitambo, sema mmezoea kutolipa kodi mnataka watu wengine walipe huduma mpewe ninyi, now mmeona haikwepeki mmeanza vilio.Magu alifanya uhuni na kutuletea Bunge lililojaa wapuuzi wasiojali matakwa ya wananchi, na matokeo yake ndio haya. Haya sasa.
Maana ya kuupiga mwingi Ni Nini?Mama enu anaupiga mwingi kweri-kweri
kwani mkopo wa ma trillioni kutoka WB ni kwa ajili ya nini? au tunajiandaa kununua wapiga kura....mtu wa hali ya chini hana uwezo wa kumiliki nyumba.
ukiweza kumiliki nyumba na ukavuta umeme wewe unajiweza, na uanao uwezo wa kulipa Sh.elfu moja kwa mwezi.
tulipe kodi kwa maendeleo yetu, hakuna nchi inayo weza kuleta maendeleo bila kutoza kodi.
Wakati wa kampeni za uchaguzi au hati ktk ziara za Viongozi wa Serikali ktk maeneo mbalimbali utawasikia wananchi wanailaumu/wanalalamikia Serikali kwa kushindwa kuletea maji, hospitali, dawa, shule,vyoo, barabara, umeme n.k.
sasa unadhani huduma hizo zitatatuliwaje bila sisi wenyewe kulipa kodi.
kumbuka wananchi wakizikosa huduma hizo lazima pia watailaumu Serikali kwa kushindwa kutatua kero zao.
tuache kuibabaisha Serikali, tulipe kodi.
Huo ndio mtego!Na ukijipeleka kusema una wapagaji watano au mita tono zitaondolewa kwenye kulipia 1000 ila lazima ulipe kodi ya mapato kutoka katika pesa za wapangaji!!
Amang'ana ghenu!
Naomba niende kwenye maada moja kwa moja,
Wakuu naomba kuelimishwa/kufafanuliwa kuhusu hili Tangazo la TRA na TANESCO kupitia maswali ninayotaka kuuliza hapa kwa sababu kuna vitu Tangazo halijaweka wazi pengine ndo ikapelekea mimi kutokuliewa vilivyo na kuibua mswali kichwani mwangu,
Maswali yangu ni kama ifutavyo
1) Swala la wapangaji kuhusu hii kodi ya majengo likoje? Na wao ni wahusika wa kulipa hii elf1 kila mwezi kama sivyo TANESCO na TRA wanaliweka vipi?
2) Nyumba moja inazo Luku zaidi ya mbili, hili nalo likoje? Jengo moja litakuwa linalipiwa kodi zaidi ya elf2?
3) Je kuna maelekezo yoyote tukilipa hiyo wenye nyumba wawarudishie hicho kiasi walicholipa? Kama yapo kuna utaratibu gani umeweka kwa hizo hela kurudi kwa wapangaji!
Nb, Nimepita kwenye moja ya page zao kwenye mitandao hakuna majibu ya maswali yangu.
Hata kama sio wao watajibu naomba mwanaJF alieliewa Tangazo majibu yako tafadhali.
Tafadhali, Mimi sijaelewa. Ni kwamba kila anayenunua LUKU wana-asume ana jengo?Ndiyo. Kwa mujibu wa TRA ni kwamba mtu mwenye jengo la kawaida anapaswa lipa kodi ya jengo ya shilingi 12,000/= kwa mwaka, na wale wenye maghorofa watalipa 60,000/= kwa mwaka bila kujali idadi ya sakafu/floors iwapo jengo litakuwa kwenye miji midogo.
Sasa hii 1000/= kwa kila mwezi ndiyo italeta 12,000/= kwa mwaka na hii 5,000/= kwa mwezi ndiyo italeta 60,000/= kwa mwaka.
Au iitwe kodi ya watumia umeme kabisa😀😀Ndio maana watu wakapendekeza iitwe kodi ya luku/ umeme/ meter kwa sababu inatozwa kwa meter sio jengo.
Jengo lenye meter 2 litatozwa 2,000 kwa mwezi wakati kimsingi kodi ya jengo inatakiwa iwe 1,000/- kwa jengo.
Au iitwe kodi ya watumia umeme kabisa😀😀
Tatizo hizo hela zitatumika kwa maendeleo au kununua ma vx?ahsante sana.
najisikia fahari kuijenga nchi yangu.
watanzania tupo tayari, kazi na iendeleee.
Apa wasipokuwa makini hii kodi watalipa wapangaji tena wengine bila kujua,watanzania wengi hata wakungalia yale makato ni shida.bado ni pagumu sana, sidhani kama wamejipanga vema......hapa kuna watu wasio na nyumba watalipia pango bila kupenda...tusubirie tuone...hii na TOZO NA MIAMALA haina tofauti....kila kona tutatachapwa.........fikiria unaishi nyumba uliyopangishiwa na serikali, ya kwako umempangisha HAJI MANARA.....wewe huku kila kitu serikali inamaliza..habari sijui umeme umeisha hunayo....kule kwa mpangaji ndie anaenunua LUKU.....atakaelipa kodi ya jengo ni nani......kuna kitu ndani ya kitu.....subiri tuone...na tulivyo na vilaza wengiii....endelea kusikilizia mdundo kwanza....