Mchanganuo tozo za LUKU kuanzia August 20-2021

Apo inatafutwa kodi ya mapato kutoka kwa wapangaji pesa mwenye nyumba anazo pokea kutoka kwa wapanaji!!
siku sio nyingi wenye majengo wata pandisha kodi maana wata lazimikana Ama wata julikana
 
ahsante sana.
najisikia fahari kuijenga nchi yangu.
watanzania tupo tayari, kazi na iendeleee.
Tupo tayari lakini vipi kwa wale watu wa hali ya chini? Umeshawafikiria hata kidogo?
 
Wanawake mtaambia nini watu??

"Manawake wanaweza????"
 
mtu wa hali ya chini hana uwezo wa kumiliki nyumba.
ukiweza kumiliki nyumba na ukavuta umeme wewe unajiweza, na uanao uwezo wa kulipa Sh.elfu moja kwa mwezi.
tulipe kodi kwa maendeleo yetu, hakuna nchi inayo weza kuleta maendeleo bila kutoza kodi.

Wakati wa kampeni za uchaguzi au hati ktk ziara za Viongozi wa Serikali ktk maeneo mbalimbali utawasikia wananchi wanailaumu/wanalalamikia Serikali kwa kushindwa kuletea maji, hospitali, dawa, shule,vyoo, barabara, umeme n.k.
sasa unadhani huduma hizo zitatatuliwaje bila sisi wenyewe kulipa kodi.
kumbuka wananchi wakizikosa huduma hizo lazima pia watailaumu Serikali kwa kushindwa kutatua kero zao.
tuache kuibabaisha Serikali, tulipe kodi.
 
Wamesema mwenye nyumba apeleke Luku hizo ziingizwe kwenye luku moja. Hakafu wapangaji hamtakiwi kulipa hii ni ya mwenye nyumba. Akigoma nendeni TRA(ila mnaweza kufukuzwa kwenye hio nyumba ha ha ha ha)
bado ni pagumu sana, sidhani kama wamejipanga vema......hapa kuna watu wasio na nyumba watalipia pango bila kupenda...tusubirie tuone...hii na TOZO NA MIAMALA haina tofauti....kila kona tutatachapwa.........fikiria unaishi nyumba uliyopangishiwa na serikali, ya kwako umempangisha HAJI MANARA.....wewe huku kila kitu serikali inamaliza..habari sijui umeme umeisha hunayo....kule kwa mpangaji ndie anaenunua LUKU.....atakaelipa kodi ya jengo ni nani......kuna kitu ndani ya kitu.....subiri tuone...na tulivyo na vilaza wengiii....endelea kusikilizia mdundo kwanza....
 
Magu alifanya uhuni na kutuletea Bunge lililojaa wapuuzi wasiojali matakwa ya wananchi, na matokeo yake ndio haya. Haya sasa.
Kodi ya majengo iliwepo toka kitambo, sema mmezoea kutolipa kodi mnataka watu wengine walipe huduma mpewe ninyi, now mmeona haikwepeki mmeanza vilio.
 
kwani mkopo wa ma trillioni kutoka WB ni kwa ajili ya nini? au tunajiandaa kununua wapiga kura....
 

Mkuu Wgr30 salamu kwako.
Nashukuru kwa maswali mazuri. Kama sijakosea inaonekana kwamba TRA wame-Assume kila mtumiaji wa umeme atakuwa ananunua Umeme mara moja kila mwezi ambapo uhalisia unaweza usiwe huo. Kimkakati wa kukusanya kodi ya majengo hili zoezi litaiwezesha Serikali kupata mapato zaidi kutokana na majengo tofauti na ilivyokuwa awali. Najaribu kuwaza kama akitokea mtu akanunua Umeme mwingi (Mfano Unamnunulia Mzazi Kijijini) mara moja kwa mwaka utekelezaji wa haya makato utakuwaje.

Anyway, naipongeza Serikali kwa huu ubunifu
 
Tafadhali, Mimi sijaelewa. Ni kwamba kila anayenunua LUKU wana-asume ana jengo?
 
Ndio maana watu wakapendekeza iitwe kodi ya luku/ umeme/ meter kwa sababu inatozwa kwa meter sio jengo.

Jengo lenye meter 2 litatozwa 2,000 kwa mwezi wakati kimsingi kodi ya jengo inatakiwa iwe 1,000/- kwa jengo.
Au iitwe kodi ya watumia umeme kabisaπŸ˜€πŸ˜€
 
Au iitwe kodi ya watumia umeme kabisaπŸ˜€πŸ˜€

Kabisa, ni kosa kuiita kodi ya jengo wakati unawatoza wapangaji kila wanaponunua umeme na inatozwa kwa kila meter na sio kila jengo.
 
Hyo Kodi ni inakatwa mara Moja ndani ya mwezi sio Kila ukinunua
 
Apa wasipokuwa makini hii kodi watalipa wapangaji tena wengine bila kujua,watanzania wengi hata wakungalia yale makato ni shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…