Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba nami nitoe mchango wangu kwenye mada hii japo umepoint baadhi tu ya watu wawe washirika wakuu, mimi naomba niwe mshirika wa kawaida. Mtoa mada umezungumzia mchango wa wadada wanaoishi u.k na u.s.a na kujiona kwao masuperior. Mimi naona usuperior ni tabia ya wanawake/ wadada hasa anapokua amefanya jambo ambalo mwenzake hawezi kufanya au bado hajafanya. Chukulia mfano wa wadada wanaotokea mikoani wakaja DSM huwakoga sana wenzao ambao bado hawajafika dar tena wengine warudipo vijijini kwao hujifanya hata kilugha wamesahau na kuongea kiswahili tu tena kile cha mtaani na si fasaha.
Kwa mtazamo wangu wadada wanaoishi nje ya nchi wana mchango mkubwa sana nchini kwetu. Wengi wao wanasaidia sana ndugu zao na kwa bahati mbaya baadhi ya ndugu wanamissuse hiyo misaada. Kumbuka mwanamke huwa hasau kwao hata kama anashida kiasi gani lazima atasaidia wakwao.
Mimi hii naichukulia in a positive way ni kweli kuna baadhi ya wadada wanafanya kazi mbili mbili kama ambavyo huwa tunasikia lkn hii yote ni kwa sababu nyumbani kwao wanamtegemea karibu ukoo mzima na wengi tunaamini mtu akienda ulaya basi huyo atakua anapesa ie tunaamini wazungu wote anaosalimiana nao basi humkesh hii ni myth iliyozoeleka huku kwetu. Kuna wachangiaji wanasema pengine wengine kazi yao ni kuzoa kinyesi cha wazungu , mimi nadhani kazi ni shughuli yoyote halali inayomuwezesha mtu kuwa na kipato. Hii ni dharau tu, ambayo sijui tunaitoa wapi. Si wote wnazoa kinyesi wapo wengi wanafanya kazi nzuri tu.
Sasa ile hali ya kujikweza na nini ni tabia ya mtu . Mtu huyo hata angeishi China bado angejikweza tumewaona wagnapi wameenda china na wanajiona superior. Ile hali ya wadada wengi kusema watu wengine wanaenda ulaya kulala na mbwa hii ni kashfa hakuna kitu kama hicho jamani. Binafsi napenda kuwa positive in everything, wala kuishi ulaya sio mafanikio/kushindwa la hasha mafanikio popote japo ulaya kuna opportunities nyingi .
Nisiwachoshe naconlude kwamba madiaspora wanachangia pato la taifa kwani ukielimisha m/ke mmoja umeelimisha taifa. Niombe radhi kama utajisikia nimekukwaza mpendwa. Natoa rai jamani tutoke twende na nchi za wenzetu tuone wanishije ili tuepuke kuamini myth.
Wanajenga, wanawasomesha madogo, wanavuta ndugu/jamaa zao etc.
nilichomaanisha ni kuwa mkiendaga mandenyi mnafanya show ya bia kama kawa. nunulia kila mtu vitochi na nini. ila mkirudi daslamu mnaombwa ada na mliowapiga ofa. hawajui umesave na unaenda kula bataz na mzee wako awe proud, wanadhani unaishi maisha ya kula bataz kila siku. kumbe ukirudi daslamu ni bia za mawazo mtindo mmoja!:heh:
hivi kukaa nje ni kufanikiwa kweli,
sijawahi kuona aliyetoka nje na mafanikio
nimepata hasira kidogo niwataje kwa majina aliobobea nje lakini wako vile vile.
thats what we were waiting for..wataje tu!
nilichomaanisha ni kuwa mkiendaga mandenyi mnafanya show ya bia kama kawa. nunulia kila mtu vitochi na nini. ila mkirudi daslamu mnaombwa ada na mliowapiga ofa. hawajui umesave na unaenda kula bataz na mzee wako awe proud, wanadhani unaishi maisha ya kula bataz kila siku. kumbe ukirudi daslamu ni bia za mawazo mtindo mmoja!:heh:
aaah wapi..!! vibaka wapo sana, msitembelee miji mikubwa tu kuna miji mingine ukienda.... Jamani.. Jamani utasema bora hata ya mkaa mbagala mara elfu.
Msishangae kwanini walioko nchi za ulaya na kwingineko wanashindwa kuwasaidia ndugu zao?
Jamani wengine wanapokuwa huko wanapata hela ya kula tu ilimradi siku isogee wakirudi makwao mbwembwe nyingii..
haya ngoja tusubiri figganigga aje atufafanulie ili na mimi niweze kuchangia madaFP kivyangu siuoni pengine mzee wa mia anauona
au mke ya mzungu akija hapa atasema neno.
Source yangu ni the little book of financial numbers publicized by the world bank. but as I said nitacheki tena and revert.
Najua Mh. Zitto Kabwe nae aliandika on it. Leo jioni nikiwa home nacheki na naleta data. It could be more...
The money goes directly to individuals and most of them use it for education and health.
ha haaaaa, umenikumbusha kitu......saa zingine mtu anakuona superior na kwa sababu anajisikia inferior mwenyewe. ni attitude tu bwana. mie hata niwe tandahimba, im just me. siko superior wala inferior, i am me and i am occupying my space!
kuna mtu humu nilimuambia niko busy kidogo nna kazi naiandaa before dashing off kwa holiday, akanijibu ati naact boss lady. i was like huhhhh:suspicious:
FP kivyangu siuoni pengine mzee wa mia anauona
au mke ya mzungu akija hapa atasema neno.
Kambi popote ama?
Mimi nipo Kisiju huku nakwea minazi huu mwaka wa 12
na kweli ni dharau mbona tanzania waudumu wa afya tunazoa sana hayo mavi hamsemi,kwasababu yuko nje ya nchi akizoa mavi ndo si halali,kazi ni kazi ilimradi ukiuki maadili ya mwenyezi mungu