Mchango wa harusi sio deni. Usipange bajeti zako kwenye mifuko ya wenzako

Nimejianzia utamaduni wa kuulisa kumuuliza swali bwana harusi mtarajiwa kwenye kikao cha kwanza cha kupanga bajeti ya kwamba anataka kufanya harusi ya bajeti kiasi gani? Wengine hujibu laki nane, laki tatu, milioni moja, mbili, tatu na wengine bajeti zao ni ghali mno. Nimegundua suala la bajeji ya harusi hutegemea uwezo wa uchumi wa wanakamati, waliaalikwa wataburuzwa tu kwa mchango kiasi watakachopangiwa kutoa, watoe wasitoe harusi itafanywa na wanakamati. Na kamati ya harusi pia hutegema kariba ya bwana harusi au status ya wazazi wake wanazungukwa na watu wa aina gani na wana uwezo gani kiuchumi
 
Nimejianzishia utamaduni wa kuulisa kumuuliza swali bwana harusi mtarajiwa kwenye kikao cha kwanza cha kupanga bajeti ya kwamba anataka kufanya harusi ya bajeti kiasi gani? Wengine hujibu laki nane, laki tatu, milioni moja, mbili, tatu na wengine bajeti zao ni ghali mno. Nimegundua suala la bajeji ya harusi hutegemea uwezo wa uchumi wa wanakamati, waliaalikwa wataburuzwa tu kwa mchango kiasi watakachopangiwa kutoa, watoe wasitoe harusi itafanywa na wanakamati. Na kamati ya harusi pia hutegema kariba ya bwana harusi au status ya wazazi wake wanazungukwa na watu wa aina gani na wana uwezo gani kiuchumi
 
Habari waungwana wa humu.

Bila shaka hakuna aliye mgeni wa kadhia hii kwenye maisha yetu ya kila siku kwenye jamii zetu..

Kama kawaida ya watu duni umoja wetu ndio nguvu yetu ya kufanikisha yale yanayoonekana yako nje ya kimo chetu kiuchumi.

Mshikamano ni jambo la msingi sana lakini inakuwa kheri zaidi ukielekezewa kwenye mambo ya msingi kwenye jamii yetu kwa ujumla wake kama vile afya, elimu, misiba na majanga mengine ya kiasili.

Suala la ndoa au kufanya harusi ni suala binafsi..ambalo watu wa nje ya wale watu wako wa karibu inabakia kuwa ni khiyari kwao na sio kama shuruti

Kwenye jamii yetu kumezuka hali ya kudai na kulazimishana michango ya harusi utadhani ni deni mtu anakudai.

Wao wanakaa kwenye kamati zao na kuandaa bajeti zao ambazo wanajua kabisa haziendani na misuli yao kiuchumi.....alafu wanaamua kulingana na bajeti hii kila mtu atoe kiasi fulani cha fedha.

Ndugu zanguni hii si sawa...si vyema kupanga bajeti zenu za anasa kwenye mifuko ya watu wengine....Hali ya maisha ni ngumu.

Tunajua na kutambua kuwa ndoa ni jambo kheri lakini bado kwa asilimia kubwa linabakia kwenye uwezo wa muoaji kwanza na khiyari ya michango ya watu wengine

Kwanini usifanye jambo lako kwa wepesi kwa kadri ya uwezo wako kiuchumi....kwanini uhangaishe au kusumbua kwenye jambo ulilolipanga mwenyewe.....

Ukishampa mtu taarifa basi muache afanye khiyari mwenyewe na so kumfuatilia kama wale watu wa OYA..

MCHANGO WA HARUSI SIO DENI.......View attachment 3153423
Shida ni kwamba wengine hutafuta mitaji wakidhani kutakuwa na ziada walau.
 
Mtu hamjaongea miaka mitano Ila anakutafuta ghafla na ombi la mchango wa harusi na kakupangia kiwango wanachotoa familia na marafiki wa karibu. Usipotoa unaitwa fake friend kwenye urafiki ambao hata haukuwepo
Na ukitoa shughuli ikiisha mwendo ni ule ule, kuna dada nilisoma nae tulimchangia baada ya shughuli kupita yeye ndio wa kwanza kuleft group na hakuwahi kuchangia chochote kwenye grp la shule akijitetea yeye ni mke wa mtu.
 
Naanza kutoa Za kukwamisha sherehe AKA kataa Ndoa.

Tatizo pressure ya Jamii, watu wanataka kuoana kimyakimya utasikia wazazi "unatakiwa kutuheshimisha...." Mara "... Nimewachangia wenzangu sana ..nataka na Mimi wanitunze".

Nawakati mwingine Muoaji unaambiwa hii sherehe si yako, tuachie sisi. Pia Jamii hii imekuwa inapenda sana sherehe unakuta birthday ya mtoto wa Mwaka 1, sawa na send off, graduation ya kindergarten sawa harisi😁

Kwa nchi kadhaa nilizotembelea hii huwa Moja ya topic yangu muhimu nikiwa nabadikishana mawazo na wenyeji wangu. Sehemu nyingi nilizoenda kuoana ni swala la waoanaji kuandaa tafrija Kwa uwezo wao, wanaarika tu watu waje kuwapa company na zawadi. With exceptional na familia za kitajiri hao ndio ughalamia mchongo mzima.

Kwa hiyo hili swala linahitaji mjadala mpaka kuanza kubadiri akili za watu. Wakiambiwa tuchangie mtoto wa furani ada akasomee udaktari hakuna atakaye toa japo Iko wazi kabisa wanajua akifuzu anaweza watibu.
 
Habari waungwana wa humu.

Bila shaka hakuna aliye mgeni wa kadhia hii kwenye maisha yetu ya kila siku kwenye jamii zetu..

Kama kawaida ya watu duni umoja wetu ndio nguvu yetu ya kufanikisha yale yanayoonekana yako nje ya kimo chetu kiuchumi.

Mshikamano ni jambo la msingi sana lakini inakuwa kheri zaidi ukielekezewa kwenye mambo ya msingi kwenye jamii yetu kwa ujumla wake kama vile afya, elimu, misiba na majanga mengine ya kiasili.

Suala la ndoa au kufanya harusi ni suala binafsi..ambalo watu wa nje ya wale watu wako wa karibu inabakia kuwa ni khiyari kwao na sio kama shuruti

Kwenye jamii yetu kumezuka hali ya kudai na kulazimishana michango ya harusi utadhani ni deni mtu anakudai.

Wao wanakaa kwenye kamati zao na kuandaa bajeti zao ambazo wanajua kabisa haziendani na misuli yao kiuchumi.....alafu wanaamua kulingana na bajeti hii kila mtu atoe kiasi fulani cha fedha.

Ndugu zanguni hii si sawa...si vyema kupanga bajeti zenu za anasa kwenye mifuko ya watu wengine....Hali ya maisha ni ngumu.

Tunajua na kutambua kuwa ndoa ni jambo kheri lakini bado kwa asilimia kubwa linabakia kwenye uwezo wa muoaji kwanza na khiyari ya michango ya watu wengine

Kwanini usifanye jambo lako kwa wepesi kwa kadri ya uwezo wako kiuchumi....kwanini uhangaishe au kusumbua kwenye jambo ulilolipanga mwenyewe.....

Ukishampa mtu taarifa basi muache afanye khiyari mwenyewe na so kumfuatilia kama wale watu wa OYA..

MCHANGO WA HARUSI SIO DENI.......View attachment 3153423
Toa mchango huo kijana aoe ndio undugu huo
 
Mkuu tunapenda sana tusapoti watu wa karibu kwenye mambo yao ila wao wenyewe wanajifelisha, hebu fikiria shughuli ni early December alafu taarifa ya kuomba mchango mtu anakupa november na mambo yalivyo mengi.

Hapa nilipo nna michango minne yote shughuli ni december, kati ya hiyo ni mmoja tu alienipa taarifa october tena bado naona alichelewa sana, hawa wengine taarifa nmepewa juzi tu. Sms za kukumbushia kama mvua dadeki, uhalisia utaamua niliyoweka ahadi ni moja tu hiyo niliyopewa taarifa october, hizi nyingine uhalisia wa maisha utaamua.

Hivi kwanini watu wasifanye mambo kwa uwezo wao wenyewe? Kuna haja gani ya kufanya lisherehe likubwa wakati uwezo huo haupo?
 
Mimi kuna group nimeingizwa kwa ajili ya mchango wa birthday nimesikitika sana. Mimi meenyewe sijawahi kufanya birthday, si kutafutiana lawama huku! Kesho tutaonana kanisani najua mhusika atankumbusha.
Kuna watu wana upumbavu mwingi sana, wanatumia hizi events kujikusanyia fedha.
 
Naanza kutoa Za kukwamisha sherehe AKA kataa Ndoa.

Tatizo pressure ya Jamii, watu wanataka kuoana kimyakimya utasikia wazazi "unatakiwa kutuheshimisha...." Mara "... Nimewachangia wenzangu sana ..nataka na Mimi wanitunze".

Nawakati mwingine Muoaji unaambiwa hii sherehe si yako, tuachie sisi. Pia Jamii hii imekuwa inapenda sana sherehe unakuta birthday ya mtoto wa Mwaka 1, sawa na send off, graduation ya kindergarten sawa harisi😁

Kwa nchi kadhaa nilizotembelea hii huwa Moja ya topic yangu muhimu nikiwa nabadikishana mawazo na wenyeji wangu. Sehemu nyingi nilizoenda kuoana ni swala la waoanaji kuandaa tafrija Kwa uwezo wao, wanaarika tu watu waje kuwapa company na zawadi. With exceptional na familia za kitajiri hao ndio ughalamia mchongo mzima.

Kwa hiyo hili swala linahitaji mjadala mpaka kuanza kubadiri akili za watu. Wakiambiwa tuchangie mtoto wa furani ada akasomee udaktari hakuna atakaye toa japo Iko wazi kabisa wanajua akifuzu anaweza watibu.
Huko sahihi mkuu hapo kwenye kuchangia vitu kama ada au mtu anaumwa ni ngumu sana ila harusi ni chap tu inabidi tuchange hii mindset.
 
Back
Top Bottom