Mchango wa harusi sio deni. Usipange bajeti zako kwenye mifuko ya wenzako

Mchango wa harusi sio deni. Usipange bajeti zako kwenye mifuko ya wenzako

Ukiahidi ujue tayari ni deni. Kama hutaki kudaiwa usiahidi, ukiahidi na usipotoa huo ni utoto. Hekima na busara ni kutokuahidi.
Tatizo ni unashurutishwa utoe pledge, yaani kama vile dalali wa kuuza nguo anavyofanya kukulazimisha ununue mpaka unaingia line.

Unyama mimi nafanyaga mda mwingine, nakubali kuchanga kupunguza maneno mengi halafu ananiweka kwenye group na mimi napiga kimya mwanzo mwisho mpaka harusi inakuja kufanyika.

Sasa nakuwa najiuliza, mbona mimi sijachanga na harusi ameweza kufanya vizuri tu, kumbe nikaja kugundua mchango wangu haukua wa umuhimu
 
Wale huwa desperate na suala lao tu. Wakishafanikisha huwaoni tena
Na hii ndo sababu kubwa kwanini huwa sichangi. Mtu hamjawasiliana kwa miaka hata zaidi ya 6 anaibuka leo kuomba mchango, hiyo maana yako anataka kukutumia tu kama chombo na shida yake ikiisha anapotea.
 
Tatizo Watanzania tunaiga maisha. Wakati napata mke nilimueleza tutafunga ndoa miaka minne/mitano ijayo wakati tyr nauwezo wa kusimamia jambo mwenyewe. Lakini kipindi chote kabla na baada ya kuanza kuishi na mke nilikuwa nachangiaga watu vizuri tu. Ilipofuka miaka mitano nikaamua sasa ni muda wa kwenda kufunga ndoa. Nikapiga hesabu zangu nikaona nikiwa na milioni nane nafanya kitu kizuri huko kijijini kwetu. Kwakweli hiyo pesa nilikuwa nayo lakini nikakumbuka na Mimi nilichangiaga nikasema naomba mchango Kwa wale tu niliowachia. Nikawahesabu wakafikia 43 nikawacheki hewani kuomba mchango, aisee walikotoka walifika 17 tu. Nikaja gundua michango ya harusi ni ujinga tu unatusumbua
 
Ukifunga ndoa kanisan ukarudi zako nyumban kuendelea na majukumu yako ya kawaida
kina haribika nn tuache kusumbua watu kwa michango na ndipo chuki zinapo ibukia
Akiba uliyotaka kufanyia sherehe fanyia mambo ya maendeleo au
Fanya sherehe kwa pesa zako utajenga heshima
 
Na hii ndo sababu kubwa kwanini huwa sichangi. Mtu hamjawasiliana kwa miaka hata zaidi ya 6 anaibuka leo kuomba mchango, hiyo maana yako anataka kukutumia tu kama chombo na shida yake ikiisha anapotea.
On point mkuu, akishapata kampani na mchango mnarudi kwenye hali ile ile iliyokuwepo mwanzo
 
Tatizo ni unashurutishwa utoe pledge, yaani kama vile dalali wa kuuza nguo anavyofanya kukulazimisha ununue mpaka unaingia line.

Unyama mimi nafanyaga mda mwingine, nakubali kuchanga kupunguza maneno mengi halafu ananiweka kwenye group na mimi napiga kimya mwanzo mwisho mpaka harusi inakuja kufanyika.

Sasa nakuwa najiuliza, mbona mimi sijachanga na harusi ameweza kufanya vizuri tu, kumbe nikaja kugundua mchango wangu haukua wa umuhimu
Ongea na moyo wako. Achana na kuwaza watu watakuonaje, kama hujisikii kuchangia hiyo sherehe, tumepewa brain tuitimie, jifanye una tatizo kubwa limekukabili na linahitaji fedha nyingi na ndo unazichanga changa hadi ulimalize, kwahiyo huwezi kuahidi kwa sasa mpaka baadae, wapige chenga chenga mpaka likupite.
 
Shida kubwa ni maisha ya kuiga: Fulani kafanya hivi na mimi lazima nifanye kama yeye. Shida nyingine: Nilimchangia na yeye lazima anichangie hii inatengeneza ushindani usiyo na tija katika maisha.
Kwa ujumla michango ya harusi inaharibu mahusiano katika JAMII na ndoa changa kwani baada ya sherehe zilizo nyingi wanandoa wapya hubaki na madeni au kukosa nafasi ya kupanga maisha wataanzaje baada kufunga ndoa.
Turahisishe maisha Ili maisha yaende vizuri.
 
Back
Top Bottom