Ni kweli..
Usilazimishe kuchangiwa.
Angalia hii...
Ilikuwa kikao cha kwanza cha Harusi...ndugu, jamaa na marafiki kila mmoja aliulizwa kiasi ambacho anaweza kuchangia bila kulazimishwa kuna aliyetaja laki 1, 2, 3,4, 5, na wengine elfu 50, 30, 20 hadi elfu 10 ( Kwa hiari), na wengine walisema hawana uhakika ila Mungu akipenda tuko pamoja.
Kwasababu hujalizimishwa na mtu, ila ni kiherere chako cha kujifanya mwamba na kuahidi Tsh laki 5..endapo utashindwa kutoa kama ulivyo ahidi hilo ni Deni na inakulazimu ulipe.
Kwanini utoe ahadi ikiwa hauna uhakika na bajeti zako na hujalazimishwa..?
Michango ya kijinga ni ile ya kulazimisha kwa kumpangia mtu kiasi cha kuchangia kwenye furaha yako.