Shida ni kwamba wengine hutafuta mitaji wakidhani kutakuwa na ziada walau.Habari waungwana wa humu.
Bila shaka hakuna aliye mgeni wa kadhia hii kwenye maisha yetu ya kila siku kwenye jamii zetu..
Kama kawaida ya watu duni umoja wetu ndio nguvu yetu ya kufanikisha yale yanayoonekana yako nje ya kimo chetu kiuchumi.
Mshikamano ni jambo la msingi sana lakini inakuwa kheri zaidi ukielekezewa kwenye mambo ya msingi kwenye jamii yetu kwa ujumla wake kama vile afya, elimu, misiba na majanga mengine ya kiasili.
Suala la ndoa au kufanya harusi ni suala binafsi..ambalo watu wa nje ya wale watu wako wa karibu inabakia kuwa ni khiyari kwao na sio kama shuruti
Kwenye jamii yetu kumezuka hali ya kudai na kulazimishana michango ya harusi utadhani ni deni mtu anakudai.
Wao wanakaa kwenye kamati zao na kuandaa bajeti zao ambazo wanajua kabisa haziendani na misuli yao kiuchumi.....alafu wanaamua kulingana na bajeti hii kila mtu atoe kiasi fulani cha fedha.
Ndugu zanguni hii si sawa...si vyema kupanga bajeti zenu za anasa kwenye mifuko ya watu wengine....Hali ya maisha ni ngumu.
Tunajua na kutambua kuwa ndoa ni jambo kheri lakini bado kwa asilimia kubwa linabakia kwenye uwezo wa muoaji kwanza na khiyari ya michango ya watu wengine
Kwanini usifanye jambo lako kwa wepesi kwa kadri ya uwezo wako kiuchumi....kwanini uhangaishe au kusumbua kwenye jambo ulilolipanga mwenyewe.....
Ukishampa mtu taarifa basi muache afanye khiyari mwenyewe na so kumfuatilia kama wale watu wa OYA..
MCHANGO WA HARUSI SIO DENI.......View attachment 3153423
Duh!!Shida ni kwamba wengine hutafuta mitaji wakidhani kutakuwa na ziada walau.
Unaweza ukatoa ahadi lakini yakaenda kombo kinyume na matarajio.......hiyo haimfungi mtu kushurutishwa kama deni....Ukiahidi ujue tayari ni deni. Kama hutaki kudaiwa usiahidi, ukiahidi na usipotoa huo ni utoto. Hekima na busara ni kutokuahidi.
Na ukitoa shughuli ikiisha mwendo ni ule ule, kuna dada nilisoma nae tulimchangia baada ya shughuli kupita yeye ndio wa kwanza kuleft group na hakuwahi kuchangia chochote kwenye grp la shule akijitetea yeye ni mke wa mtu.Mtu hamjaongea miaka mitano Ila anakutafuta ghafla na ombi la mchango wa harusi na kakupangia kiwango wanachotoa familia na marafiki wa karibu. Usipotoa unaitwa fake friend kwenye urafiki ambao hata haukuwepo
Toa mchango huo kijana aoe ndio undugu huoHabari waungwana wa humu.
Bila shaka hakuna aliye mgeni wa kadhia hii kwenye maisha yetu ya kila siku kwenye jamii zetu..
Kama kawaida ya watu duni umoja wetu ndio nguvu yetu ya kufanikisha yale yanayoonekana yako nje ya kimo chetu kiuchumi.
Mshikamano ni jambo la msingi sana lakini inakuwa kheri zaidi ukielekezewa kwenye mambo ya msingi kwenye jamii yetu kwa ujumla wake kama vile afya, elimu, misiba na majanga mengine ya kiasili.
Suala la ndoa au kufanya harusi ni suala binafsi..ambalo watu wa nje ya wale watu wako wa karibu inabakia kuwa ni khiyari kwao na sio kama shuruti
Kwenye jamii yetu kumezuka hali ya kudai na kulazimishana michango ya harusi utadhani ni deni mtu anakudai.
Wao wanakaa kwenye kamati zao na kuandaa bajeti zao ambazo wanajua kabisa haziendani na misuli yao kiuchumi.....alafu wanaamua kulingana na bajeti hii kila mtu atoe kiasi fulani cha fedha.
Ndugu zanguni hii si sawa...si vyema kupanga bajeti zenu za anasa kwenye mifuko ya watu wengine....Hali ya maisha ni ngumu.
Tunajua na kutambua kuwa ndoa ni jambo kheri lakini bado kwa asilimia kubwa linabakia kwenye uwezo wa muoaji kwanza na khiyari ya michango ya watu wengine
Kwanini usifanye jambo lako kwa wepesi kwa kadri ya uwezo wako kiuchumi....kwanini uhangaishe au kusumbua kwenye jambo ulilolipanga mwenyewe.....
Ukishampa mtu taarifa basi muache afanye khiyari mwenyewe na so kumfuatilia kama wale watu wa OYA..
MCHANGO WA HARUSI SIO DENI.......View attachment 3153423
Mimi kuna group nimeingizwa kwa ajili ya mchango wa birthday nimesikitika sana. Mimi meenyewe sijawahi kufanya birthday, si kutafutiana lawama huku! Kesho tutaonana kanisani najua mhusika atankumbusha.Hilo ni jangq, mara nyingine unajikuta ushaingizwa grupuni na humo humjui muowaji wala muolewaji.
Glass ni silaha za kupopoana kipindi cha mgogoro au ugomvi kwa wanandoa sema tu watu hawajui.Aisee halafu sijui kwanini zawadi nyingi kwenye harusi ni glass.
Mh!Kuchangishana harusi ni umasikini tu.
Kuna watu wana upumbavu mwingi sana, wanatumia hizi events kujikusanyia fedha.Mimi kuna group nimeingizwa kwa ajili ya mchango wa birthday nimesikitika sana. Mimi meenyewe sijawahi kufanya birthday, si kutafutiana lawama huku! Kesho tutaonana kanisani najua mhusika atankumbusha.
KAMA BILA MCHANGO KUTOKA HUWEZI KUOA AU KUOLEWA BASI NA IWE HIVYO.Bila kuwafatilia amtoi.
Hata mimi nimehisi hivyo, imagine unapangiwa kiwango kabisa. Nimepiga hesabu hicho kwango ni mshahara wangu wa siku moja, hesabu zimekataa kabisa kama atakasirika poa tu.Kuna watu wana upumbavu mwingi sana, wanatumia hizi events kujikusanyia fedha.
Huko sahihi mkuu hapo kwenye kuchangia vitu kama ada au mtu anaumwa ni ngumu sana ila harusi ni chap tu inabidi tuchange hii mindset.Naanza kutoa Za kukwamisha sherehe AKA kataa Ndoa.
Tatizo pressure ya Jamii, watu wanataka kuoana kimyakimya utasikia wazazi "unatakiwa kutuheshimisha...." Mara "... Nimewachangia wenzangu sana ..nataka na Mimi wanitunze".
Nawakati mwingine Muoaji unaambiwa hii sherehe si yako, tuachie sisi. Pia Jamii hii imekuwa inapenda sana sherehe unakuta birthday ya mtoto wa Mwaka 1, sawa na send off, graduation ya kindergarten sawa harisi😁
Kwa nchi kadhaa nilizotembelea hii huwa Moja ya topic yangu muhimu nikiwa nabadikishana mawazo na wenyeji wangu. Sehemu nyingi nilizoenda kuoana ni swala la waoanaji kuandaa tafrija Kwa uwezo wao, wanaarika tu watu waje kuwapa company na zawadi. With exceptional na familia za kitajiri hao ndio ughalamia mchongo mzima.
Kwa hiyo hili swala linahitaji mjadala mpaka kuanza kubadiri akili za watu. Wakiambiwa tuchangie mtoto wa furani ada akasomee udaktari hakuna atakaye toa japo Iko wazi kabisa wanajua akifuzu anaweza watibu.