Mchango wa harusi sio deni. Usipange bajeti zako kwenye mifuko ya wenzako

Huo ni ubinafsi wa kiwango cha lami.
Mkuu binadamu wengi ni wabinafsi haswa kwa umri wetu maana Kila mtu anakusogelea anapoona utampa wepesi kwenye jambo flani. Akifanikisha anaondoka

Kwa hiyo ni kiasi tu cha kujiwekea mipaka ili ujue wapi pa kuweka nguvu zako tu. Ukiwa na extra unatoa, ukiwa huna unaacha kwa lugha nzuri. Muelewa ataelewa, asiyeelewa hawezi kuelewa, Simple tu
 
Kuna watu sio waelewa kabisa ila maisha lazima yaendelee hata asipokubaliana na uhalisia.
Kabisa mkuu, mwisho wa siku mwenye kutaka ku_judge hata umpe 50k or 100k bado atalalamika hujatoa wa kutosha. Mtu anaona kama ni yake kupata pesa kubwa hata kama hamna bond
 
Kweli kabisa aseh, Kuna jamaa yangu nae alikuwa kwenye kikao Kama hicho, Kwa kupenda sifa ndo akawa wa kwanza kunyoosha mkono na kutaja kiwango kikubwa zaidi kuliko wenzie,basi unadhani alitekeleza!!,wafuatiliaji aliwa block kabisa.
 
Bila kuwafatilia amtoi.
Kwani lazima? Acheni kusumbua watu. Jiandae mwenyewe kwa kadiri ya nguvu yako; michango ya ndugu, jamaa na marafiki iwe nyongeza tu. Mbona mimi nilijuandaa kwa kidogo nilichokuwa nacho, nikapanga sherehe kwa bajeti ndogo niliyokuwa nayo. Waliopewa kadi hawakufutiliwa kama vile wanadaiwa madeni.

Mtu akishapewa kadi, kama amekusudia kuchanga kutokana na umuhimu wako kwake, atachangia tu bila hata kulazimika kukumbushwa.

NB: Kwa wale wanaoahidi hao ni lazima walipe. Kwa kuwa ahadi ni deni. Usijifanye mwamba kwa kutoa ahadi nono, wakati uwezo wa kulipa hiyo ahadi huna.
 
Heri wanaume mnapewa ya harusi tu.
jamani wadada kitchenparty, bridalshower, babyshower kajifungua kuna kibeseni ...akiolewa ana mimba basi mnachanga mpakaaa..... na Usipotoa mtu anakununia kheeee🙌🤣
Kiuhalisia hiyo michango yenu yote inalipwa na mwanaume indirect.
 
Mi nadhani ianze kwa mwenye sherehe, beba sherehe yako mwenyewe kama una milioni inatosha kufanya sherehe.baada ya hapo hutajiona una deni kuwachangia wengine.wengi wanachanga kwa sababu na wao walichangiwa.Wengi wanachanga kwa kujifariji na yeye atachangiwa.
 
Sasa kwenye ufunguzi wa kamati ulipikiwa chakula Cha gharama ukala na kunywa, uliposhiba ukainuka na Kutoa ahadi,

Leo hii hutaki kukumbushwa ahadi uliyoitoa.

Kumbuka hata wazazi wako walisaidiwa walipooana.

Wacha kibri, this is Africa.
 
Sasa kwenye ufunguzi wa kamati ulipikiwa chakula Cha gharama ukala na kunywa, uliposhiba ukainuka na Kutoa ahadi,

Leo hii hutaki kukumbushwa ahadi uliyoitoa.

Kumbuka hata wazazi wako walisaidiwa walipooana.

Wacha kibri, this is Africa.
KInachoshangaza Mjomba akiumwa hachangiwi hata laki moja ya matibabu hadi anakufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…