Mchango wa mawazo kutoka kwa wadau nataka kufunga ndoa

Mwambie unayo ruhusa ya kuoa hadi wanne,lakini umeanza na moja itategemea na atakavyojiweka na kuitunza nafasi yake pweke.

Mwambie, kitaani kuna wazuri wengi wananyemelea kuichukua nafasi yake ,asijibwagaze na kuibeza nafasi hiyo.

Mwambie Ndoa sio ndoano bali ni maelewano na MARIDHIANO.

Mwambie lengo la ndoa si kupata Mali za Urithi wala Ngono, bali kupata waoto na kujenga Familia itakayomridhisha Muumba na kuleta tija kwa jamii na Taifa kwa Ujumla.

Umasikini na Utajirini Majaaliwa yake Mungu, hoja tujitahidi kushirikiana kujenga maisha

Mwambie Ushirikina ni Adui wa Kwanza kuliko yote katika Ndoa,Ukimbaini anakupa Liimbwata au Mizizi ndio mwisho wa Ndoa yenu bila msamaha.
 
Asanteeeee kwa ujumbe mzuri.
 

Bwana harusi una busara/akili sana....hope hii busara utaitumia katika kupambana na matatizo/migogoro yako katika ndoa

Bibi harusi ana bahati sana kupata mtu kama wewe....kila la heri
 
Ushauri wangu, oa. Ikiwezekana hata jana. La msingi mkeo asiwe spana mkononi, asiwe mtu ambaye kupitisha wiki mbili bila kuumwa serious kwake ni ajabu. Hilo ni la msingi kuliko yote, niamini mimi
kwahiyo kiongozi unamshauri jamaa kabla ya kuweka ndani mzigo ufanyiwe overhaul kwanza sio⚙🛠🔨🔧
 
Mshirikiane katika mambo yenu yote kusiwe na usiri baina yenu
Upendo wa kweli ikiwemo kumwmbia kuwa unampenda
Kuvumilia mapungufu yanayovumilika
Kusamehe pindi anapokukosea na wewe kuomba msamaha pindi unapokosa
Kumjali na kuhudumia familia yako mtakapopata watoto. Jua kuwa wewe ndio kila kitu katika familia ndio mtoaji na mwangalizi mkuu
Usifuatilie au kukipigia hesabu kipato cha mkeo
Msali au kuswali na kumtumikia Mungu kama familia
 
Bwana harusi una busara/akili sana....hope hii busara utaitumia katika kupambana na matatizo/migogoro yako katika ndoa

Bibi harusi ana bahati sana kupata mtu kama wewe....kila la heri
Asante mkuu.
 
Amiin Mwenyezimungu atatuongoza.
 

Mtangulize Mwenyezi Mungu.. kama namba moja kwenye ndoa yenu.. mawasiliano na wako mujenge mapema.. kuzoea kuongea mengi.. muwe marafiki.. ni mengi haya pia tosha..
Kamwe usimpige mkeo.. na musitukanane kutiana machungu.. machungu huwa hayaondoki kirahisi.. mupendane huku munarekebishana..

Vitu vidogo sana.. ndio uvunja ndoa au mahusiano..

Kila ya kheri
 
Akizingua kwa uhuni kiburi na kukupanda kichwani na kukosa kukusikiliza mpe za UCHEBE atanyooka.
 
Hongera sana Jah awe mlinzi, faraja, na mpatanishi wa ndoa yenu, muishi kwa amani na mfurahie muungano wenu, mjaliwe watoto wazuriiiii na mzeeke pamoja. Ameeeeeeen
 
Hongera sana Jah awe mlinzi, faraja, na mpatanishi wa ndoa yenu, muishi kwa amani na mfurahie muungano wenu, mjaliwe watoto wazuriiiii na mzeeke pamoja. Ameeeeeeen
Ameeeeen,Dua makbur Mashallah....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…