Mchango wa sherehe ya kumaliza Masters itakayofanyika ukumbini. Nini maoni yako kuhusu uchangishaji wa sherehe za namna hii?

Ukichangia huo ujinga utakuwa huna tofauti na Lucas Mwashambwa
 
hamna hoja hapo
kwan kp kbaya klichoongelewa
mtazamo has kabsa yan wew n bureee
 
Kama huoni haja ya kuchangia unakaa tu kimya. Kuna mtu kaniadd kwenye grupu la mchango wa harusi bila ridhaa yangu nimeamua tu kukaa kimya grupuni bila kuchangia chochote.. sichangii mawazo wala hela. Nimeona kwa influence niliyo nayo nikileft italeta taharuki kwa wengine wanaochanga
 
Kumdhalilisha kivipi wakati hatumjui mleta mada kwa jina halisi wala huyo anayechangiwa? Stori kama hii inaweza kuwa kweli au isiwe kweli.
 
Sherehe yoyote inatakiwa ighalamiwe na mwenye sherehe. Mwenye shangwe awaalike rafiki zake wajumuike kwenye sherehe yake bila malipo. Wao waamue kuja na zawadi kulingana na uwezo.

Changa kuondoa ugomvi na mwamba maana anatafuta njia ya kukosana.
 
Sherehe yoyote inatakiwa ighalamiwe na mwenye sherehe. Mwenye shangwe awaalike rafiki zake wajumuike kwenye sherehe yake bila malipo. Wao waamue kuja na zawadi kulingana na uwezo.

Changa kuondoa ugomvi na mwamba maana anatafuta njia ya kukosana.
Sasa hapo mwenye sherehe anawaburudisha waalikwa au yeye?

Sherehe ni ndugu na marafiki kumburudisha na kumsherehesha mwenye sherehe yake sio vinginevyo

Hilo la kwako haliko sahihi ujinga mtupu
Watu wakichanga ni kumsherehesha mwenye sherehe sio yeye kuwasherehesha wao

Una mawazo ya kimaskini sana
 
Msihalalishe upumbavu kisa et ujamaa!
Michango ya kipuuzi haina maana yoyote..
Tukianza na Birthday/Graduation/send off/kitchen party na Harusi zenyewe..
Yani sherehe yako unanipangia hela ya kukupa na nguo ya kuvaa....
Huu upuuzi tunaufanya basi tu ila unanikera sana hapa yenyewe nipo kwenye Graduation nmetolea mchango kisa sijui ujirani mwema! Inachosha hasa kwa sisi ambao hatuna mpango wa kufanya sherehe yoyote maishani!
 
Pumbavu... hawa ndio wasomi wetu, yanashangilia kumaliza elimu yao lkn kichwani hamna kitu, na hata lamaana labda lenye mchango kwa taifa hakuna.

Tunasafari ndefu sana waTz kwa kuendekeza upuuzi usio na maana, huyo mpumbavu mwambie hizo pesa angewekeza ktk gunduzi na tafiti za kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali, na sio kuendekeza starehe ya dakika chache isiyo na faida.

Bado wahitimu na wasomi wetu haijulikani huko masomoni wanajifunza vitu gani, maana akili zao haziko tofauti na wasio soma.

Narudia tena, huyo mpumbavu au hata kama ni wewe hizo pesa za kufanyia ujinga wa sherehe elekeza nguvu hizo na pesa hizo kutatua mambo ya msingi na sio sherehe.

Hawa ndio wasomi wetu
 
Shida yako ni kuzaliwa kwenye koo maskini na wasio na mshikamano

Matukio kama hayo ndio hukutanisha ndugu na marafiki kumpongeza mwanaukoo au rafiki au mtoto wa ndugu au rafiki kwa kwenda hatua nyingine ya maisha

Wana celebrate success

Ila kama umezaliwa familia au ukoo wa malofa wasio na mshikamano kama ndugu au ukoo hutaelewa hayo mambo utaona ni nonsense
 
Ulofa unakusumbua yaani mchango wa elfu 50 unaandika maneno yote hayo hadi sauti inakauka ungeambiwa mchango milioni si ungejinyonga

Kemea Pepo la umaskini likutoke kwa Jina la

Ulofa unakusumbua yaani mchango wa elfu 50 unaandika maneno yote hayo hadi sauti inakauka ungeambiwa mchango milioni si ungejinyonga

Kemea Pepo la umaskini likutoke kwa Jina la Yesu
Kama pesa sio shida wasingelialia kuchangiwa wangejipanga wao.

Wasomi wetu vilaza hawajui matumizi sahihi ya akili
 
Kama pesa sio shida wasingelialia kuchangiwa wangejipanga wao.

Wasomi wetu vilaza hawajui matumizi sahihi ya akili
Sherehe hushikwa na kamati kama hujui sio mhusika

Mfano mtoto anaoa au kuolewa sio jukumu. Lake wazazi na ndugu na marafiki ndio husambaza kadi kwa ndugu na marafiki wachangie hata kama huyo anayeoa au kuolewa ni bilionea

Kiafrika ndugu na marafiki ndio huoza mtu hajiozi yeye kama ilivyo kwa maruhuni wazungu huko kwao

Ndio maana yeye hata kwenye kamati huwa tu kama mtu wa kawaida tu kuchanga chochote alichonacho kidogo tu sehemu kubwa hubebwa na hao ndugu na marafiki ambao wana mshikamano wanaomwozesha sio yeye

Narudia kwa wale mliozaliwa familia na koo za kimaskini na zisizo na mshikamano kama familia na koo za wazungu wasio na mshikamano hii mada kwenu ngumu mno kuielewa na kupata logic ngumu mno kwenu
 
Kwenye taifa ambalo watu kupata milo mitatu ni Anasa, Taifa ambalo watu maiti zinawekwa rehani sababu marehemu hajamalizia Pesa ya Matibabu..., Taifa la hivyo hata nikiwa na pesa za kumwaga kushiriki kwenda kufuja / kutumbua Pesa kwa siku Moja sijui Bajeti ya Mamilioni ya Pesa wakati hata hao tunaowachangia Hata Nyumba hawana na wanakwenda kuanza maisha ya Kupanga, kwa kuwaongezea madeni ya kurudisha fadhila (walichangiwa lazima nao wachange) Nadhani ni kuwa na Vipaumbele vya Kilimbukeni....

Kama unazo zako tumia hata trilioni, au kama hio ndio ndoto yako basi jichange kabla ya wakati ili wakati ukifika usiweke viingilio
 
Bado kidogo tutaanza kuchangiana za kulipa Gest House.! Sina maana hiyo unayofikiri wewe!
 
Sasa nyinyi ndo mmezaliwa kwenye umasikini
Kuchangisha ni ishara kuu ya umasikini maana yake mwenye tafrija ameshindwa kujimudu anaomba mchango!
Ukoo wetu haunaga umasikini ni inaandaliwa sherehe nmnaalikwa tu mka celebrate na zawadi zenu.
 
Mm kuna mdada mtoto wake amemaliza std 7 anamfanyia sherehe mwezi ujao anataka nimchangie...yan nimecheka kimoyomoyo nimeshindwa hata kumjibu
 
Sasa nyinyi ndo mmezaliwa kwenye umasikini
Kuchangisha ni ishara kuu ya umasikini
Hujui kitu mabilionea wote duniani huwa na mifuko ya kuchangisha inaitwa Foundation kusaidia watu

Kuna Billy Gates Foundation, Mo Dewji Foundation, Benjamin Mkapa Foundation nk yote hiyo huchangiwa na watu mbalimbali duniani hata maskini wa kuchangia dola moja

Mchango ni njia mojawapo ya kusema tuko pamoja kwenye hilo jambo lako kwa tendo la kuchangia sio tuko kwa maneno

Donald Trump ni bilionea lakini pesa za kampeni kachangiwa hadi na watu wa chini ni njia yao ya kusema tuko pamoja na wewe

Concept yako ya kusema kuchangisha kuwa mchangishaji maskini haiko sawa

Narudia shida umezaliwa koo na familia malofa na wasio na mshikamano

Hii mada iko juu ya uwezo wa kichwa chako kitalipuka moto bure ngumu kwako kuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…