Nimejaribu kumsikiliza professor Tibaijuka ambaye anafanya constructive criticism juu ya mambo mbalimbali nchini pia kufuatia hali ya nchi sasa ilivyo nimekuja na mtazamo wangu binafsi.
1.Nchi yetu sasa hivi imeparanganyika .Hakuna ukaribu kati ya wananchi hasa tabaka la chini na watu wa tabaka la juu kwa hiyo watu wamejaa chuki ,hasira na kuombeana mabaya tu ,ndani ya serikali wapo watu hawashangilii yanayoendelea na hawaongei kitu lakini sio kwamba wanafurahi.
2.Nahic kuna namna tunashauriwa vibaya mfano kesi ya Lissu haina maslahi yeyote kwa Taifa ,Masuala ya utekaji na watu kupotea yamefanya nchi yetu iendleee kupoteza mvuto na heshima yake kama mwanzo.
3.Kuna haja ya Mh Raisi kuangalia namba ya kufanya uteuzi wa wakuu wa wilaya ,mikoa na wakurugenzi ili kureplace uzembe unaoripotiwa katika halmashauri mbalimbali nchini.
4.Chama cha mapinduzi sasa hivi hakina mtu mwenye mvuto ambaye unconditional anaweza kupata public attention kama zamani ilivyokua kwa upande wangu kwa sasa simuoni mtu mwenye ushwawishi.
5.Watu wengi hasa watawala na wananchi hawana elimu ya kutosha ya mambo mfano uchumi,teknolojia matumizi ya akili mnemba nk.
6.Deni la Taifa sio himilivu maana 18percent ndio limit kwa IMF sisi tuko 31 kwa hyo tupunguze kasi ya kukopa halafu tusipende kuweka uongo uongo sehemu ya utamaduni wetu.
7.Kila wizara ije na mkakati wa kuboresha maisha ya watu wake na idadi ya watu wake yenye takwimu sahihi mfano ajira graduates wangapi wameajiliwa? Wangapi jobless? Nk.
8.Tunahitaji maridhiano ya kweli yanayoambatana na haki na uwajibikaji kisha katiba mpya.
9.chochoko za Muungano zinaendelea kuharibu nchi yetu
10.Tusikubali tena kushiriki maandano yanayoambatana na vurugu sisi ni nchi masikini tukiharibu miundombinu ni kazi kuirejesha .