Mcharo kawa mtamuuu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Matangazo ya kibongo shida tupu, inakuwaje mwanaume asifiwe kawa mtamu?

Mtamu anajulikana ni mtu wa namna gani! Kwa kawaida chakula na wanawake ndio husifiwa kwa utamu, haya ni mazoea ya kiasili sasa inakuwaje leo mwanaume asifiwe kawa mtamu??

Kwa wenye tangazo wanaona kama wamefanikiwa sana lakini kiuhalisia ni matusi kwa jinsia ya kiumeni! Na matangazo ya namna hii yapo mengi sana bongo
 
duh...mara ya kwanza kusikia hili tangazo nikawa najiuliza walikuwa na maana gani? nikapotezea tu nikujua ni lugha ya kibiashara...kumbe tupo wengi!! Nilidhani nilielewa vibaya mimi tu..
 
duh...mara ya kwanza kusikia hili tangazo nikawa najiuliza walikuwa na maana gani? nikapotezea tu nikujua ni lugha ya kibiashara...kumbe tupo wengi!! Nilidhani nilielewa vibaya mimi tu..
Aisee hata mimi..!
 
Ni kweli mshana jr matangazo yanayoleta ukakasi wa masikio yako mengi bongo. Lingine linaloniudhi ni lile linalotaja condom kwa kufananisha na helmet.
Linasema:
"Sa sikiliza mpenzi wangu, mi leo sivai helmet bwana. Naona inaniletea joto tu yaani. Mi naona safari yangu sitafika kisawasawa yaani............"
Wamejitahidi kutumia lugha ya staha lakini huhitaji akili kubwa kujua watu wale wako kwenye "faragha". Tangazo lile ukilisikiliza ukiwa na mtu unayemstahi (kwa mila za kitanzania) unatafuta pa kuangalia. Wapo walio kinyume au tofauti na mimi lakini kama nilivyotanguliza kusema - ni mimi, ni mtazamo wangu.
 
Last edited by a moderator:
Hayo matangazo kwa kweli ni n.oma
 
Kwa kweli ni tangazo la kijinga na lisilo eleweka, walioliweka inabidi wtueleze Mcharo kawa mtamu kivipi?
 
Linawavunjia kina mharo heshima. Nani hajaelimika a hayo mambo.

Mengi acha kupiga pesa kinyume n maadili
 
Tatizo watu wanaojihusisha na hayo mambo hujifanya wajuaji sana... iko wapi Radio Tanzania
 
Mkuu wala siyo wewe tu! Hata mimi huwa linaniudhi sana, henu fikria mko sebuleni na watoto wamewazunguka halafu ndo linatoka tangazo kama hilo inakuwaje mkuu? Yaani hii nchi sisi kila kitu ni mazuzu tu, yule mama si anataka kupigwa kitu yule? Maana hata wanavyozungumza kwa kupepesa midomo yaani ni full maloviiiiii. Hivi hayana mtu ya kudhibiti hii kitu? Eti mwisho mama anamalizia "naona baby hiki chumba uje uhame bodaboda zinakuchanganya mpaka kondom unaita helmet?" Ukiwa na hivi vitoto vya dotcom havijakupiga swali tu? Jamani hebu hizi aibu watuondolee aiseee!! Mpaka tunashindwa kukaa kwa uhuru na watoto wetu maana hapo ni full remote mkononi, maana yake nini?
 
hahahaha hili kosa nililisikia muda sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…