Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Matangazo ya kibongo shida tupu, inakuwaje mwanaume asifiwe kawa mtamu?
Mtamu anajulikana ni mtu wa namna gani! Kwa kawaida chakula na wanawake ndio husifiwa kwa utamu, haya ni mazoea ya kiasili sasa inakuwaje leo mwanaume asifiwe kawa mtamu??
Kwa wenye tangazo wanaona kama wamefanikiwa sana lakini kiuhalisia ni matusi kwa jinsia ya kiumeni! Na matangazo ya namna hii yapo mengi sana bongo
musami usitetee ujinga hata mimi naishi mtaani na lugha zetu kama mtu kafanikiwa ni mambo safi, katoka, yuko njema, kibopa nk...! Neno utamu halipo labda kama ni msamiati mpya ambao hata hivyo hauashirii memaNi kutokana na uliyoyajaza mawazoni mwako ndio maana umetafsiri hivyo.Lakini kuwa mtamu ni neno la mtaani likiwa na maana ya kufanikiwa kimaisha
Mshana Jr.......
Ni kweli mshana jr matangazo yanayoleta ukakasi wa masikio yako mengi bongo. Lingine linaloniudhi ni lile linalotaja condom kwa kufananisha na helmet.
Linasema:
"Sa sikiliza mpenzi wangu, mi leo sivai helmet bwana. Naona inaniletea joto tu yaani. Mi naona safari yangu sitafika kisawasawa yaani............"
Wamejitahidi kutumia lugha ya staha lakini huhitaji akili kubwa kujua watu wale wako kwenye "faragha". Tangazo lile ukilisikiliza ukiwa na mtu unayemstahi (kwa mila za kitanzania) unatafuta pa kuangalia. Wapo walio kinyume au tofauti na mimi lakini kama nilivyotanguliza kusema - ni mimi, ni mtazamo wangu.
Mkuu wala siyo wewe tu! Hata mimi huwa linaniudhi sana, henu fikria mko sebuleni na watoto wamewazunguka halafu ndo linatoka tangazo kama hilo inakuwaje mkuu? Yaani hii nchi sisi kila kitu ni mazuzu tu, yule mama si anataka kupigwa kitu yule? Maana hata wanavyozungumza kwa kupepesa midomo yaani ni full maloviiiiii. Hivi hayana mtu ya kudhibiti hii kitu? Eti mwisho mama anamalizia "naona baby hiki chumba uje uhame bodaboda zinakuchanganya mpaka kondom unaita helmet?" Ukiwa na hivi vitoto vya dotcom havijakupiga swali tu? Jamani hebu hizi aibu watuondolee aiseee!! Mpaka tunashindwa kukaa kwa uhuru na watoto wetu maana hapo ni full remote mkononi, maana yake nini?