Mchawi kazi yake ni kuroga urudi nyuma, jilinde

Mchawi kazi yake ni kuroga urudi nyuma, jilinde

Sio kidogo Kaka..
Unaweza kuona kijana ameenda chuo na tabia nzuri na Imani za kimungu!
Lakini baada ya muda kadhaa anaanza kujihusisha na makundi, ulevi na umalaya..

Wengi huwa tunaita ni sababu ya Toxic Friend cycle Ila huo sio ukweli..

Hao watu huwa na tabia ya kumpelekesha mtu bila kujua anayofanya after Long-term anakuja kujilaumu.

Nina ushahidi wa dogo mmoja alikuwa anapata division oNe kuanzia form Hadi six.

Baada ya kufaulu chuo tu! Siku anapanda treni kuja Udsm..... Alikimbia bila kuaga mtu yoyote na mpaka naongea na wewe muda huu uyu dogo Ni Teja......

Baaada ya muda mrefu mama yake alitembea kwa wataalamu na kubaini Ni ndugu zake ndio wamemfanyia hivyo kwasababu Ilikuwa ya yeye kuja kufanikiwa hapo baaadae
Kwa hiyo taifa Zima limelogwa na mana hamna ajira au
 
Mwaka 2014 nilipitia changamoto za kiroho ( uchawi) nikajikuta naenda kwa mganga. Nilianza kuota ndoto mbaya mbaya sana, moja ya ndoto niliyowahi kuota ni ile ambayo niliota tumemkamata mchawi na aliku ni mtu ambaye simfahamu tumemuweka mtu kati na kumuuliza alikuja kufanya nini akaninyoshea kidole kwamba alikuja kunichukua nikatolewe kafara na mjomba wangu( mume wa shangazi) tena akimtaja jina . Baadae akaomba nimsamehe na akaomba nauli kwani alikuwa ni mtu wa nyumbani na baada ya kumpa nauli tu nikashtuka usingizini na ilikuwa saa Tisa usiku. Huyu shangazi ni mdogo wa baba wa mwisho wa tumbo moja . Huyu shangazi huwa haipendi familia yetu kabisa nakumbuka mwaka juzi walikuja kwenye harusi ya mtoto wake( binamu) na hawakunijulisha Wala kunialika na binamu yangu anaishi mkoa mmoja na mimi lakini kimya. Uchawi upo, mimi mama yangu anatokea mkoa x wa huko Kanda ya ziwa Kuna mdogo wake yaani mama mdogo alikuja kuishi na sisi kumbe alikuja kuifunga na kuisambaratisha familia na imegundulika majuzi tu hapa . Yako mengi sana lakini mjue uchawi upo. Mchawi mbaya ni yule anayetoka katika familia huyu ni rahisi hata kuchimbia madawa katika nyumba
 
Mwaka 2014 nilipitia changamoto za kiroho ( uchawi) nikajikuta naenda kwa mganga. Nilianza kuota ndoto mbaya mbaya sana, moja ya ndoto niliyowahi kuota ni ile ambayo niliota tumemkamata mchawi na aliku ni mtu ambaye simfahamu tumemuweka mtu kati na kumuuliza alikuja kufanya nini akaninyoshea kidole kwamba alikuja kunichukua nikatolewe kafara na mjomba wangu( mume wa shangazi) tena akimtaja jina . Baadae akaomba nimsamehe na akaomba nauli kwani alikuwa ni mtu wa nyumbani na baada ya kumpa nauli tu nikashtuka usingizini na ilikuwa saa Tisa usiku. Huyu shangazi ni mdogo wa baba wa mwisho wa tumbo moja . Huyu shangazi huwa haipendi familia yetu kabisa nakumbuka mwaka juzi walikuja kwenye harusi ya mtoto wake( binamu) na hawakunijulisha Wala kunialika na binamu yangu anaishi mkoa mmoja na mimi lakini kimya. Uchawi upo, mimi mama yangu anatokea mkoa x wa huko Kanda ya ziwa Kuna mdogo wake yaani mama mdogo alikuja kuishi na sisi kumbe alikuja kuifunga na kuisambaratisha familia na imegundulika majuzintu hapa . Yako mengi sana lakini mjue uchawi upo. Mchawi mbaya ni yule anayetoka katika familia huyu ni rahisi hata kuchumbia madawa katika nyumba
Tobaaaaaa! Msukule tena???

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pole sana..

Sijui nisemeje, ila kama umeamua kukaa kwenye hayo maombi mwenyewe , basi shikilia hapo hapo, lakin inabidi utafakari sana hio vita, na approach unayochukua, mwanamke huyo na wanaomsaidia wanaachwaje huku wameua baba wakubwa na wazee wa ukoo wanakufa tu, naona kama mission yake ni kuwamaliza wote upande wako na mama yenu

Kuna mdau humu alikuja kuelezea stori yake jinsi walivyommaliza mzee wake, nadhan ni kama wewe tu, ila yeye aliamua kuchukua kisasi kwa wote waliohusika, aliwajua, na alifanikiwa lengo lake la kuwamaliza

Shangaz yangu yeye alikuaga anatumua approach ya maombi, lakin kuna dada wa mume wake ndio alikua na chuki na kaka yake na familia yake, aliona sijui anafaidi sana, mana mjomba alikua ofisi ya rais, na walikua wanaishi maisha mazuri, ( oneni watu walivyo na roho mbaya na roho za kwanini), chuki hio ilipelekea akaanza kuiangamiza familia, alianza na watoto, mtoto wa kwanza ( dada yangu) , aliugua na anachoumwa hakijulikani, na siku anakata roho alimtaja huyo mama..haitoshi, akaja mama ( shangaz yangu) , kifo chake kilikua kibaya nashindwa kusema, akafata mtoto mwingine, naye akaondoka, akaja baba , naye akaondoka, akaja mtoto mwingine yeye akapata uchizi, akaja mtoto mwingine maisha yake yakarudi nyuma sana na kua magumu sana, aliyesalimika ni mmoja tu ambaye ndio kidogo anajiweza,..ngoja niishie hapa.
duuuh! hii dunia inatisha😢😞
 
Mfano baada ya kuweka au kulaza gari lako car parking kwa Malipo Kuna dawa ya mti Shamba unaweka kwenye gari. Au pikipiki

Mwizi akija wewe una amua afe baada ya siku moja .. au akute jiwe kubwa.....

Huoni Nina reduce cost ya kulaza gari kwa kununua mti Shamba????
😂😂😂
 
Unawaongelea vipi kina mwendazake waliokua wanaombewa na wachungaji, machifu, waganga , wachawi n.k
Kwenye mikutano yao?
Kabla Mungu hajashuka mlima Sinai alimtuma Musa awambie wana wa Isreali wajitakase ili kuondoa uovu miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kutubu dhambi zao na kuondoa miungu ya kigeni, hirizi, masanamu na makandokando mengine. Pamoja na kufanya kama Musa alivyowaagiza, siku ile Mungu anashuka mlima Sinai huo mtiti wake hawakutamani tena ashuke siku nyingine, walimwambia Musa awe anaenda yeye kuongea na Mungu halafu anawaletea taarifa. Unajua ni kwa sababu gani walipata shida kuhimili utukufu wa Mungu ulioshuka pale mlimani pamoja na kwamba walikuwa wamejitakasa? unajua ni kwa nini Mungu anaitwa ni moto ulao (a consuming fire). Mungu ni mtakatifu sana kwa hiyo nguvu zake zinaposhuka mahali kitu chochote ambacho ni kichafu, mfano, wachawi, walozi, ushirikina, uganga, umebeba hirizi sijui mitishamba na makandokando kama hayo ni kuteketeza kila kitu. Kwa hiyo nawashangaa watu wanaosema unaweza kumtegemea Mungu huku umefunga hirizi kiunoni, sijui unaenda kwa mganga, mara umeoga madawa ya kuondoa nuksi na mikosi. Huyo labda siyo huyu Mungu Mkuu ambaye pia anajulikana kama Mungu wa Israeli, atakuwa ni mungu mwingine tu.....
 
Kabla Mungu hajashuka mlima Sinai alimtuma Musa awambie wana wa Isreali wajitakase ili kuondoa uovu miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kutubu dhambi zao na kuondoa miungu ya kigeni, hirizi, masanamu na makandokando mengine. Pamoja na kufanya kama Musa alivyowaagiza, siku ile Mungu anashuka mlima Sinai huo mtiti wake hawakutamani tena ashuke siku nyingine, walimwambia Musa awe anaenda yeye kuongea na Mungu halafu anawaletea taarifa. Unajua ni kwa sababu gani walipata shida kuhimili utukufu wa Mungu ulioshuka pale mlimani pamoja na kwamba walikuwa wamejitakasa? unajua ni kwa nini Mungu anaitwa ni moto ulao (a consuming fire). Mungu ni mtakatifu sana kwa hiyo nguvu zake zinaposhuka mahali kitu chochote ambacho ni kichafu, mfano, wachawi, walozi, ushirikina, uganga, umebeba hirizi sijui mitishamba na makandokando kama hayo ni kuteketeza kila kitu. Kwa hiyo nawashangaa watu wanaosema unaweza kumtegemea Mungu huku umefunga hirizi kiunoni, sijui unaenda kwa mganga, mara umeoga madawa ya kuondoa nuksi na mikosi. Huyo labda siyo huyu Mungu Mkuu ambaye pia anajulikana kama Mungu wa Israeli, atakuwa ni mungu mwingine tu.....
vipi khs mitishamba
 
vipi khs mitishamba
Mitishamba kama mitishamba haina shida, ila kuna watu wanaitumia kiganga au kichawi na unakuta wengine wameoteshwa eti na mizimu. Kuna manabii wa Mungu ambao waliweza kutakasa maji kwa kurusha kipande cha mti ndani yake, pia kuna nabii ambaye alirusha kipande cha mti ndani ya maji, shoka iliyokuwa imezama ikaelea. Kwa hiyo itategemea miujiza au uponyaji unahusisha nguvu zipi........nguvu za Mungu au ulozi?
 
Mitishamba kama mitishamba haina shida, ila kuna watu wanaitumia kiganga au kichawi na unakuta wengine wameoteshwa eti na mizimu. Kuna manabii wa Mungu ambao waliweza kutakasa maji kwa kurusha kipande cha mti ndani yake, pia kuna nabii ambaye alirusha kipande cha mti ndani ya maji, shoka iliyokuwa imezama ikaelea. Kwa hiyo itategemea miujiza au uponyaji unahusisha nguvu zipi........nguvu za Mungu au ulozi?
mganga na mchawi ni kitu kimoja?
 
Mwanamke Ni mtu hatari sana, Mimi ni mfano Hai wa Matendo ya ukatili wa Mwanamke:

Hii naongea kutoka Moyoni mwangu wanao Bisha tabia za wanawake hawazijui.

Sikia hii story ya kweli katika Familia yangu,

Mama mkubwa mke wa Baba yangu walio oana na Baba yangu bonge la Harusi ujanani wali Dumu katika ndoa yao kwa miaka 5tu na wakazaa watoto wa3. Ila ugomvi ulikuwa daily tatizo mwanamke Alikuwa hafanyi majukumu yake ya nyumbani bali alipenda sana starehe na waganga kumchezea mume, Mume akapewa taarifa na majirani akafuatilia aka kuta kweli mkewe na vitu vya ajabu kwenye kabati la nguo na kitandani kwenye mto wa Baba na uvunguni kaweka dawa za mitishamba..

Mume kufuatilia vizuri aka gundua Mwanamke pia alikuwa anaiba hela ndani na kujenge kwao.. Wakaachana ndai ya miaka mi5 ya ndoa.

Mzee akachiwa watoto wa3 wadogo sana, akaishi bila mke kwa miaka4 , wazazi wake wakamshauri Aowe mke mwingine baada ya taarifa za yule mke wake kusambaa kuwa anaishi na mawanaume Mwingine Arusha na nimja mzito, wakati kamuachia watoto tena kwenye Nyumba ya kupanga uja nani akiwa na hali ya kawaida sana kimaisha kwa maana ya kipato cha kawaida.

Mzee kweli akajiongeza aka chukua mke mwingin ambaye ndio mama Yangu, tukazaliwa sisi, baada ya miaka kama 25 kupita tukiwa tusha zaliwa watoto6, Baba alisha pandishwa cheo na kusoma zaidi maisha yakawa makubwa na akawa msaidizi wa mkurugenzi wa Bank kuu ya tanzania na baadaye mkuu wa Azina, akawa kesha wekeza sana kila kona ya jiji la Dar na kwao Mkoani..

Ghafl mauza uza ya ugomvi ndani yakaibuka mzee kawa kama anachanganyikiwa haishi kumpiga mama kila mara yaani akawa kama siyo yeye tena.. Mara afukuze watoto mara hili mara lile, Baadaye Mama yangu akaugua ugonjwa wa ajabu sana akabaki mifupa tupu mm nikiwa ndio nimezaliwa nina mwaka 1 , mzee akawa hajali huduma wala hataki kuangali watoto,

Mama akaja kuchukuliwa apelekwe matibabuni, walizunguka mahospitali yote tanzania na ukumbuke hadi kenya na South africa alipelekwa lakini haponi wala ugonjwa hauonekani, Mwishoe akawa anakaribia kukata roho kabaki mifupa tu waka mrudisha Kijijini kwao asubirie kufa tu. Lakini kule kijijini wazee wa upande wa Mama wakajiongeza wakampeleka kwa mtaalamu wa Jadi aka aguliwa na ukweli ukajulikana alitupiwa jini na mke mkubwa na mambo mengine mengi tu.. bahati nzuri akatibiwa akapona akarudi kwenye hali yake baadaye Wakati anarudishwa nyumbani kwa wazazi wake maana alitokea kwa Matibabu ya jadi.. aka kuta watoto wote wame teletwa na kutelekezwa kwa wazazi wote. . wamekonda nusu ya kufa yule mkubwa kuliko wote aliye kuwa ana mika15 ndio kachangnyikiwa wengine wote wameacha shule na hawataki kabisa kusikia shule wala hawajielewi. Wazee wakoo waka jiongeza kuwapokea na kuwalea.

Mama alipo fuatilia aka ambiwa alivyo ondoka tu kwenda matibabuni, Week ile ile Mke mkubwa aliyekuwa ame achana na baba kwa miaka 25 alirudi na kugina ndani kwenye nyumba aliyejenga Mama yetu na Baba, na wakati huo Mzee hajitambui tena kawa kama mjinga wala hakumbuki watoto ana itwa ustawi wa jamii anaulizwa matumizi ya watoto ana sema mbona yeye hana watoto zaidi ya watatu aliyo nao nyumbani,?? watu wakadhani ni utani, kuja kumbana sana wakaagundua kweli hana kumbukumbu .. ila kesi ikaenda mahakamani ika amuliwa ahudumie watoto na aangaliwe kama akili ziko sawa. baadaye Ikaisha kienyeji Majaji wakapewa hongo na yule mke kubwa maana sasa yeye ndio alishikilia account zote za baba na mzee alifukuzwa kazi maana alikuwa haeleweki tena..

Baada ya Muda Baba kaja kufa kiajabu ajabu tu.. tuka mzika, mama mkubwa kaendelea kuishi ndani na wanawe, Ukoo ukasema kuwa kila kitu kwenye nyumba aliyokimbilia kuishi Mke mkubwa nicha watoto wa mke mdogo kwa kuwa Marehemu alisha Andika na kuwambia Wazazi wake kuwa Nyumba ya ujanani aliyo jenga kabla ya mama yangu kuishi naye na kuzaa naye ni ya watoto wake watatu aliye zaa n mke wake wandoa, ila hii mpya aliyojenga akiwa na mke mdogo yaan maa yang ni ya watoto 6 aliyo zaa na mama yangu.. Una ambiwa kile kikao cha ukoo kilivurugika kwa ugomvi mke mkubwa akawa moto na yule aliye kuwa kiongozi wa ukoo alikufa ndani ya week iliyofuata, Kukawa na viongozi wengine wanao chaguliwa Kushika nafasi ya Ukoo ila wakigusia haki za watoto wa mama yangu tu wanakufa, mpaka sasa Ninavyo ongea Baba wakubwa wa5 wote wamekufa kimaajabu. . na haki yetu hatuja ipata .. ndugu zangu karibia wote ni vichaa . nime baki mm tu ndio angalao nina jitambua..ingawa vita ya maisha yangu ni kubwa kama siyo kujificha katika maombi wangesha ni maliza..

Lakin kikubwa kinacho ni shangaza ni kuwa Baba anaonekana kule kijijin watu kazaa wana muona akiwa mchafu na manywele ila waki msogelea anapotea, mwanzoni tulidhani ni utani tukasema labda watu wanongea tu kwa kuwa yaliyotokea kweye familia yangu yameumiza watu wengi hadi majirani wa kule kijiji hivyo wanazusha tu kwa hasira walizo nazo juu ya mateso wanayo yaona kwa ndugu zangu.. Lakin sasa Hivi ni navyo ongea juzi tu mwezi wa kumi na moja mwaka huu uliyoisha. Kaka yangu mkubwa akiwa ndani kwake Katokewa na baba, kaamka zake aka kojoe ghafla akamuona mzee kakaa kwenye kochi ila haongei kitu alipo piga kelele mzee kapotea.


Jamani Uchawi Upo.. Ila naku hakikishia siku nikiingia kwenye Uchawi.. Nita angamizaa kizazi cha huyu Mwanamke mpaka kitukuu cha mwisho.. Naupima tu Uvumilivu wangu katika maombi.. Mungu aniongoze maana naijua nafsi yangu ilivyochoka na siku nikihamia kwa Shetani nitakuwa Shetani Halisi wala sita Igiza kabisa.
Pole mkuu. Yani mpaka chozi limenitoka... Nami pia nimepitia mazito mengi kama wewe japo yako ni makubwa haswa. Mwanamke akiamua kuw ibilisi anakuwa ibilisi kamili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio Elimu tu, mpaka uhusiano na ndugu jamaa na marafiki zako!
Mchawi mtu mbaya Sana!
Unaweza kuwa umesoma sana, au unasoma Sana but you haverst Nothing jua tayari Kuna mkono wa mtu...

Wanajua kabisa ukifanikiwa wewe Basi ukoo wako umefanikiwa...

Yani mtangulize Mungu pia usishau kutembea Mana hata waganga wa jadi hutumia miti ambayo imeubwa na Mungu .
Yani upo sahihi kabisa , mwaka Jana ndo nimekuja kujua kuwa wanga wananichezea , ikabidi niende kwa witch doctor kucomfirm, nimeenda kwa watu wawili tofauti wamenipa jibu moja kwamba wameniroga , nisipige hatua yoyote , saiz nipo kwenye harakati ya kuwafahamu ili nijue namna ya kuwazuia. Uchawi hupo.
 
Asante. Nmeuliza hivi makusudi kabisa, ili wale watalam na wabobezi wa maisha motiveshen speakers na maprofesa wa makanisa na manabii waone, hasa hasa wa makanisa.
Halafu mtu kama huyu unamuambia maisha sio pesa, ni amani na furaha, imagine unateseka kwa miaka 25.
@Whyme iv ule uzi wako kwann waliufunga? Ujue kuna member sisi ambao hatuwez kubishana na wafia din tunasomaga kimya kimya..... ningepend kufaham ulifikia wap?
 
Unamaanisha nguvu za Mungu ni limited hadi uzi boost na dawa za kienyeji za kuondoa mikosi na nuksi........kwamba nguvu za Mungu zinakuwa limited na vifungo vya kichawi!? mkuu unahitaji kujielimisha zaidi kwenye kujua nguvu na mamlaka ya Mungu Mwenyezi.........
Wafia dini mnasumbua..anzisheni uzi wenu huu tuachieni wazee wa mitishamba..brainwashed creatures ninyi...mmedharau na kukana asili yenu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Uchawi uchawi uchawi aaagh ptuu inachosha sasa..kila sehemu watu wanalia na madhara yatokayo na uchawi.
Mm nashindwa hata kuandika,nimeamua kumuachia Mungu tu kama ataamua kuniacha niendelee kuteswa,kunyanyaswa na kuonja joto ya jiwe na wachawi sawa tu si ameamua iwe hivyo bhana Ila mm nimechoka na sina msaada wowote kutoka popote zaidi yake.

Nimechoka kuona wenzangu wakisonga mbele mm nikiwa nyuma na wamwisho kila siku, nimechoka kudharaulika sababu sina maendeleo kama wenzangu,nimechoka pesa zangu kuishia kwenye matibabu,nimechoka na kuugua maradhi yasiyoisha mwilini mwangu.

Nimechoka kutibia wazazi,nimechoka kutibia wadogo zangu,nimechoka kutibia familia,nimechoka kuishi kwa huzuni na mateso.

Nimechoka kujaza namba za simu za madaktari na manesi,nimechoka kitembelea maduka yamadawa,nimechoka kunywa dawa,nimechoka kugeuza dawa mbadala wa Chakula.

Nimechoka dharau,kebehi,masengenyo na vijembe juu ya uduni wangu unaosababishwa na wao wenyewe,nimechoka nimechoka nimechoka.

Eeh Mungu Mwenyezi,Mfalme wa falme,Mmiliki wa mbingu na dunia na ukazisimamisha pasipo nguzo,Mfalme wa siku ya Malipo,Mwingi wa Rehma mwnye kurehemu.

Ulieniumba mm ukamuumba baba na mama yangu,ukawaumba bibi na babu zangu, ukaumba wanangu,ukaumba ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake,Nakuomba eeh Rabbi uninusuru mm pamoja na kizazi changu chote dhidi ya udhalimu wa shetani na hila Zake zote.

Ewe Mola wangu mtukufu,usieshindwa na chochote mana vyote ni Mali yako,hakuna kilichopo nje matakwa yako,hakuna linalowezekana ila kwa idhini yako..nakuomba uniponywe mm,waponye wazazi wangu, iponyewe familia yangu,iponye jamii yangu liponye taifa langu dhidi ya uchawi, ulozi,ushirikina,na hila zote ovu za shetani.

Ninakuomba utufungulie milango ya rizki zetu ziwe za halali,za wepesi na uzikinge dhidi ya mabaya yoyote.sisi bila ww hatuwezi kitu Mungu wangu.

Tupe afya tuondolee maradhi,tupe Neema tuondolee ufakiri na umaskini,tupe mioyo safi tuondolee chuki na husda,tupe upendo tuondolee huzuni fitna na majungu.

Eeh mola wetu mlezi,mwenye huruma,mwenye upendo na msikivu, tunaomba usikie Dua yetu,tunakuomba usikie kilio chetu.sisi ni wakosefu tu si wakamilifu,ukamilifu unao ww Mungu wetu mtukufu.

Ninaomba yote haya kwa imani yangu kwangu,na kwa imani za wenzangu ila naamini sisi sote tunakutukuza ww kwa njia tofauti.
Amiiin
Amiiin
Amiiin
Unamlilia mungu yupi..wa wayahudi..wawazungu..wawaarabu..wawahindi..wawachina au wawaafrika?

Anyway kua na imani katika yote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom