Shukuru Mungu baba yako hakuoa mshirikina akamleta kwenye familia yenu! Hilo ndio jambo pekee naweza kukwambia kwa sasa.
Mkuu Extrovert sikatai hayo mambo kuwepo na huenda na mimi yameniathiri, ninachosema ni kwamba unatakiwa kumtegemea Mungu kwa hali yoyote ile. Kinyume cha hapo unakuwa unachanganya au kutegemea nguvu nyingine tofauti. Hakuna binadamu aliyetumika kwa viwango vya juu katika utumishi wa Mungu kama Mtume Paulo, lakini alikuwa na ugonjwa sugu mwilini mwake hadi kumwomba Mungu amponye lakini hakupona, alipozidi kuomba, Yesu akamwambia neema yangu yakutosha. Ndo maana katika maneno yake ameandika hivi "Nitajivunia udhaifu wangu ili uweza wa kristo ukae juu yangu, maana ninapokuwa dhaifu ndipo nilivyo na nguvu" ingekuwa sasa ungesema aende kutafuta mitishamba au waganga wa kienyeji......nilipotafakari kuhusu haya maneno ya Mtume Paulo alimaanisha kwamba pamoja na kwamba anaishi katika hali ya udhaifu wa mwili, lakini imani yake katika Mungu au nguvu zake za kiroho zinaongezeka siku baada ya siku. Ndo maana mahala pengine kaandika hivi "Japokuwa utu wangu wa nje unachakaa, bali utu wangu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku" haya ni maneno kutoka kwa mtu mwenye imani iliyovuka viwango vya kawaida vya kiimani.......