Uchawi uchawi uchawi aaagh ptuu inachosha sasa..kila sehemu watu wanalia na madhara yatokayo na uchawi.
Mm nashindwa hata kuandika,nimeamua kumuachia Mungu tu kama ataamua kuniacha niendelee kuteswa,kunyanyaswa na kuonja joto ya jiwe na wachawi sawa tu si ameamua iwe hivyo bhana Ila mm nimechoka na sina msaada wowote kutoka popote zaidi yake.
Nimechoka kuona wenzangu wakisonga mbele mm nikiwa nyuma na wamwisho kila siku, nimechoka kudharaulika sababu sina maendeleo kama wenzangu,nimechoka pesa zangu kuishia kwenye matibabu,nimechoka na kuugua maradhi yasiyoisha mwilini mwangu.
Nimechoka kutibia wazazi,nimechoka kutibia wadogo zangu,nimechoka kutibia familia,nimechoka kuishi kwa huzuni na mateso.
Nimechoka kujaza namba za simu za madaktari na manesi,nimechoka kitembelea maduka yamadawa,nimechoka kunywa dawa,nimechoka kugeuza dawa mbadala wa Chakula.
Nimechoka dharau,kebehi,masengenyo na vijembe juu ya uduni wangu unaosababishwa na wao wenyewe,nimechoka nimechoka nimechoka.
Eeh Mungu Mwenyezi,Mfalme wa falme,Mmiliki wa mbingu na dunia na ukazisimamisha pasipo nguzo,Mfalme wa siku ya Malipo,Mwingi wa Rehma mwnye kurehemu.
Ulieniumba mm ukamuumba baba na mama yangu,ukawaumba bibi na babu zangu, ukaumba wanangu,ukaumba ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake,Nakuomba eeh Rabbi uninusuru mm pamoja na kizazi changu chote dhidi ya udhalimu wa shetani na hila Zake zote.
Ewe Mola wangu mtukufu,usieshindwa na chochote mana vyote ni Mali yako,hakuna kilichopo nje matakwa yako,hakuna linalowezekana ila kwa idhini yako..nakuomba uniponywe mm,waponye wazazi wangu, iponyewe familia yangu,iponye jamii yangu liponye taifa langu dhidi ya uchawi, ulozi,ushirikina,na hila zote ovu za shetani.
Ninakuomba utufungulie milango ya rizki zetu ziwe za halali,za wepesi na uzikinge dhidi ya mabaya yoyote.sisi bila ww hatuwezi kitu Mungu wangu.
Tupe afya tuondolee maradhi,tupe Neema tuondolee ufakiri na umaskini,tupe mioyo safi tuondolee chuki na husda,tupe upendo tuondolee huzuni fitna na majungu.
Eeh mola wetu mlezi,mwenye huruma,mwenye upendo na msikivu, tunaomba usikie Dua yetu,tunakuomba usikie kilio chetu.sisi ni wakosefu tu si wakamilifu,ukamilifu unao ww Mungu wetu mtukufu.
Ninaomba yote haya kwa imani yangu kwangu,na kwa imani za wenzangu ila naamini sisi sote tunakutukuza ww kwa njia tofauti.
Amiiin
Amiiin
Amiiin