Mchawi kazi yake ni kuroga urudi nyuma, jilinde

Kwa hiyo taifa Zima limelogwa na mana hamna ajira au
 
Mwaka 2014 nilipitia changamoto za kiroho ( uchawi) nikajikuta naenda kwa mganga. Nilianza kuota ndoto mbaya mbaya sana, moja ya ndoto niliyowahi kuota ni ile ambayo niliota tumemkamata mchawi na aliku ni mtu ambaye simfahamu tumemuweka mtu kati na kumuuliza alikuja kufanya nini akaninyoshea kidole kwamba alikuja kunichukua nikatolewe kafara na mjomba wangu( mume wa shangazi) tena akimtaja jina . Baadae akaomba nimsamehe na akaomba nauli kwani alikuwa ni mtu wa nyumbani na baada ya kumpa nauli tu nikashtuka usingizini na ilikuwa saa Tisa usiku. Huyu shangazi ni mdogo wa baba wa mwisho wa tumbo moja . Huyu shangazi huwa haipendi familia yetu kabisa nakumbuka mwaka juzi walikuja kwenye harusi ya mtoto wake( binamu) na hawakunijulisha Wala kunialika na binamu yangu anaishi mkoa mmoja na mimi lakini kimya. Uchawi upo, mimi mama yangu anatokea mkoa x wa huko Kanda ya ziwa Kuna mdogo wake yaani mama mdogo alikuja kuishi na sisi kumbe alikuja kuifunga na kuisambaratisha familia na imegundulika majuzi tu hapa . Yako mengi sana lakini mjue uchawi upo. Mchawi mbaya ni yule anayetoka katika familia huyu ni rahisi hata kuchimbia madawa katika nyumba
 
Tobaaaaaa! Msukule tena???

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
duuuh! hii dunia inatisha😢😞
 
😂😂😂
 
Unawaongelea vipi kina mwendazake waliokua wanaombewa na wachungaji, machifu, waganga , wachawi n.k
Kwenye mikutano yao?
Kabla Mungu hajashuka mlima Sinai alimtuma Musa awambie wana wa Isreali wajitakase ili kuondoa uovu miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kutubu dhambi zao na kuondoa miungu ya kigeni, hirizi, masanamu na makandokando mengine. Pamoja na kufanya kama Musa alivyowaagiza, siku ile Mungu anashuka mlima Sinai huo mtiti wake hawakutamani tena ashuke siku nyingine, walimwambia Musa awe anaenda yeye kuongea na Mungu halafu anawaletea taarifa. Unajua ni kwa sababu gani walipata shida kuhimili utukufu wa Mungu ulioshuka pale mlimani pamoja na kwamba walikuwa wamejitakasa? unajua ni kwa nini Mungu anaitwa ni moto ulao (a consuming fire). Mungu ni mtakatifu sana kwa hiyo nguvu zake zinaposhuka mahali kitu chochote ambacho ni kichafu, mfano, wachawi, walozi, ushirikina, uganga, umebeba hirizi sijui mitishamba na makandokando kama hayo ni kuteketeza kila kitu. Kwa hiyo nawashangaa watu wanaosema unaweza kumtegemea Mungu huku umefunga hirizi kiunoni, sijui unaenda kwa mganga, mara umeoga madawa ya kuondoa nuksi na mikosi. Huyo labda siyo huyu Mungu Mkuu ambaye pia anajulikana kama Mungu wa Israeli, atakuwa ni mungu mwingine tu.....
 
vipi khs mitishamba
 
vipi khs mitishamba
Mitishamba kama mitishamba haina shida, ila kuna watu wanaitumia kiganga au kichawi na unakuta wengine wameoteshwa eti na mizimu. Kuna manabii wa Mungu ambao waliweza kutakasa maji kwa kurusha kipande cha mti ndani yake, pia kuna nabii ambaye alirusha kipande cha mti ndani ya maji, shoka iliyokuwa imezama ikaelea. Kwa hiyo itategemea miujiza au uponyaji unahusisha nguvu zipi........nguvu za Mungu au ulozi?
 
mganga na mchawi ni kitu kimoja?
 
Pole mkuu. Yani mpaka chozi limenitoka... Nami pia nimepitia mazito mengi kama wewe japo yako ni makubwa haswa. Mwanamke akiamua kuw ibilisi anakuwa ibilisi kamili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani upo sahihi kabisa , mwaka Jana ndo nimekuja kujua kuwa wanga wananichezea , ikabidi niende kwa witch doctor kucomfirm, nimeenda kwa watu wawili tofauti wamenipa jibu moja kwamba wameniroga , nisipige hatua yoyote , saiz nipo kwenye harakati ya kuwafahamu ili nijue namna ya kuwazuia. Uchawi hupo.
 
@Whyme iv ule uzi wako kwann waliufunga? Ujue kuna member sisi ambao hatuwez kubishana na wafia din tunasomaga kimya kimya..... ningepend kufaham ulifikia wap?
 
Wafia dini mnasumbua..anzisheni uzi wenu huu tuachieni wazee wa mitishamba..brainwashed creatures ninyi...mmedharau na kukana asili yenu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Unamlilia mungu yupi..wa wayahudi..wawazungu..wawaarabu..wawahindi..wawachina au wawaafrika?

Anyway kua na imani katika yote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…