Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Ndugu zangu,
Nimefanya utafiti nikagundua CHADEMA wako vema kwenye eneo la propaganda mitandaoni na kulimbikiza madaraka makao makuu ya ufipa.
Mchawi Mkuu wa Chadema ni Kukosekana kwa taasisi, oganaizesheni na ugatuzi wa madaraka Mikoani na Wilayani. Basil Lema ambaye ni katibu wa CHADEMA Kilimanjaro alisikika akisema "tumeshindwa kuweka mawakala vituoni kusimamia zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ukosefu wa pesa" ni dhahiri kuwa hawapati msaada wa rasilimali pesa kutoka makao makuu.Kama leo CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro unakosa hamasa ambapo ndio ngome unategemea nini kwa mikoa ya Mtwara,Lindi,Tabora,Mwanza nk? Hapa ndipo atakumbukwa Chacha Wangwe (RIP) kwani alikuwa na ndoto ya kuipeleka CHADEMA kila kona ya nchi.
Zaidi ya hili,baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ofisi nyingi za mikoa,wilaya,vijiji zilitelekezwa hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu hivyo kwa sasa hakuna oganaizesheni ambayo kimsingi ingesimamia nidhamu,usahihi ujazaji wa fomu na uratibu wa mambo mbalimbali.Hapa ndipo Dr.Slaa alifanikiwa kwani aliweza kupata taarifa ya kila eneo kwa urahisi.
Ukweli hupanda ngapi.
Nawasilisha.