kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mwanamke anataka jamii imtambue kama mtu dhaifu anaehitaji kulishwa, kutunzwa na kutunduliwa na mwanaume, anaona ni sawa lazima atolewe mahari na kuhurumiwa sana na kupewa upendeleo na wanaume.
Mwenyezimungu amewaumba viumbe wake wote sawa bila upendeleo wowote ila tofauti unazoziona baina ya viumbe ni kwasababu ya kazi zao kwenye uso wa dunia na kuepusha kugombania vyakula na makazi. Ndio maana ndege anaruka na binadamu anatembea, mchwa anaozesha vitu viwe mbolea majani yamee binadamu hawezi.
Lakini pamoja na tofauti hizi zote viumbe vuote vinapumua, vinazaa, vinajisaidia haja kubwa na ndogo, vinahisi, vinakula, vinasogea. Mke na mume wako sawa kwa viumbe vyite isipokuwa mifumo yao ya uzazi tu basi.
Majike yoote ya viumbe vingine yanajilisha, yanajitunza na kujitafutia na kupambana isipokuwa majike ya binadamu tu ambayo yanataka huruma za kusaidiwa vitu vyote la sivyo unapelekwa mahakamani kwanini humpi chakula. Majike ya simba, mbuzi, fisi, kuku, mbweha, nguchilo na mengine yote yanazaa, kutuza watoto wao na kujilisha, majike ya binadamu yanatafuta huruma za wanaume kwenye mambo yao? HII itawachelewesha sana. Jike la simba halisubiri dume likamate nyumbu ili yeye na watoto wake wale, kuku hivyohivyo, nyoka hivyohivyo.
Wanawake msisubiri huruma za wanaume fanyeni yote kama wanaume isipokuwa kwenye taratibu za kuzaa tu na uzazi baaaaasi. Jikomeesheni wenyewe vitu vyote vya kuwafanya muwe tegemezi kwa:
1. Kuamua bila kujali mwanaume atasema nini
2 fanya kazi zote sawa na wanaume isipokuwa kwwnye uzazi tu
3 Nendeni shuleni kama wanaume
4. Gombeeni kama wanaume
5. Pigeni vita sheria na kanuni za kupendelewa nanaume, zinazidi kuwadidimiza.
6. Pingeni kuolewa kwa mahari, kunakowageuza kuwa bidhaa. Hata utumie kugha gani mahari ni bei ya kununua mwanamke kutoka kwa wazazi wake.