Mchawi wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe, tuache kulaumu wanaume

Mchawi wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe, tuache kulaumu wanaume

Nadhani kuna vitabu vya dini vibadilishwe some verses kufikia huko. All in all kwenye family yafaa kila mtu afit kwenye nafasi yake, binafsi ntaruhusu aendelee kuhubiri feminism huko majukwaani kwao ila akifika mlangoni aingie kama partner, mama, mke na mlezi😊😊
 
Hii mada ya hovyo sana,
Mtu,jamii ya watu waliteswa na mifumo,siku zote na wao watatesa wengine,ukisema mchawi wa mwanamke ni mwanamke,basi hata mchawi wa Mtu mweusi ni mweusi mwenzie!
Haivi umeishawahi kuona watu wanapoishi uswahili wanavyochukiana Richa ya kwamba wote ni mafukara?!!
Mchawi wa mwanamke ni mfumo uliomfsnya hivyo,maana hata mwanamke mwenzie ni muhanga wa mfumo,
Kibaka akiiba kuku,anapigwa mpaka afe,fisadi akiiba bilioni 5!hakuna maskini wa kwenda hata masaki arushe jiwe kwenye nyumba yake,
Wanawake ni victim wa mfumo,
Hata shida za waafrika zinasababishwa na Waafrika wenyewe. Mara ngapi tunaona viongozi wa Afrika wakiimba hela na kuzificha kwa wazungu, wanaingia mikataba feki, wanauza Twiga wazimawazima, wanauza kigamboni yote, Wana sera za honyo, nk.

Hata biashara ya utumwa ni machifu wetu waliowauza wasiowataka kwa tiptip
 
Kwahiyo unataka kusema kupitia uzi wako wanaume tunatakiwa kujaza mimba na kupita na hamsini zetu kama dume la simba
Madume ya binadamu tumejaaliwa akili kuliko madume ya Simba na wanyama wengine.
Kwa akili tulizojaaliwa, twaona umuhimu wa kutekeleza majukumu ya kulea familia yaani mke na watoto , tofauti na madume ya Simba maana huko majike ndo yameonekana Yana akili za kulea familia.
Sisi wanadamu madume, hatubebi haya majukumu kwa sababu wanawake hawayawezi, la hasha, Bali twafanya hayo kwa sababu ya nguvu ya upendo, iliyotuvuta na kutusukuma kuwafuata wanawake kuomba ridhaa ya kushirikiana nao katika ujenzi wa familia( hii Tena ni tofauti na madume ya Simba ambayo huyabaka tu majike kuyasababishia uja uzito, toka lini mbakaji hata awe binadamu huwa anatunza familia).
Ndiyo maana wanawake ambao hawakubahatika kupata wanaume wenye akili zaidi ya madume ya Simba Bado wanna uwezo wa kujipambania kwa ajili ya matunzo yao na watoto wait.
Hata hivyo wake zetu sisi wanaume wenye akili zaidi ya madume ya Simba, wana hiari ya kuendeleza mapambano ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ila tu bado wanaweza kutunzwa hata wasipofanya hivyo na wakati wakiendelea na mapambano.
 
Critical thinking haimaanishi ufikirie sawa na wengine bro. Wanawake wanadai uhuru kutoka kwa watu wasiostahili, Mungu wao tayari ameshawapa uhuru siku moja pamoja na viumbe wengine. Hawahitaji huruma, msaada wala ruhusa za wanaume ili wawe wanachotaka kuwa kama vile wanaume wasivyohitaji ruhusa za wanawake ili wawe wanavyotaka kuwa. Makutano muhimu ya pekee ya mume n mke ni wakati wa kutafuta mimba baaasi. Mwanamke anaweza kuwa bondia, askari, rubani, msukuma mkokoteni, mwashi, mwindaji. nk kama mwanaume, ni yeye tu. Mim nikiwasikia wanalala majukwaani wanadai pedi za kike nacheka sana, viti maalumu, madawati ya kijisia, ukeketaji. Nk
Ongeza SAUTI KIDOGO.
 
Wenzako wanashukuru siku hizi wakiolewa maana Hali mbaya wanataka hata waolewe wakiwa kumi
 
Wenzako wanashukuru siku hizi wakiolewa maana Hali mbaya wanataka hata waolewe wakiwa kumi
Kila kitu wanalia na wanaume, mara hawatupi matunzo, mara hawatupi Pedi, mara wametupa mimba, mara waache kutembea na makahaba ili wakose soko, mara tupeni viti maalum, nk nk nk. Kama uhuru wao ni lazima wapewe na wanaume basi hawataupata milele.
 
Back
Top Bottom