TANZIA Mchekeshaji Jumanne Alela maarufu kama "Mzee Matata" wa Mizengwe afariki dunia

TANZIA Mchekeshaji Jumanne Alela maarufu kama "Mzee Matata" wa Mizengwe afariki dunia

Taarifa zinaeleza kwamba amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa tangu tarehe 13 June

========


MWIGIZAJI wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela almaarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, 2021..

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, @madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa.

“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” taarifa kutoka kwa @madebelidai.

Chanzo: Global Publishers
Kwani huko chamazi hakuna makaburi?!
 
Kwani huko chamazi hakuna makaburi?!
Yuko ndugu yangu kwake ni huko buza kwa mama kibonge , lakini alipofariki alizikwa makaburi ya Mburahati , kwa maelezo kwamba mama yake mzazi alizikwa kwenye makaburi hayo enzi hizo , kwahiyo kunakuwa na vijisababu fulani hivi visivyo na mashiko yoyote yale .
 
Mwigizaji wa vichekesho wa kikundi la Mizengwe, Jumanne Alela maarufu Mzee Matata amefariki dunia.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo Jumatano Juni 16, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Juni 13, 2021.

1623829079436.png
 
Mwenyezi Mungu amsamehe mapungufu yake na aiweke roho yake mahali peponi
 
Katika komedi nanayoipenda ni hii.mizengwe waigizajinwake ni comedian by nature huyu mzee alikuwa mahiri kwa kila idara R.I.P mzee wa sarakasi
 
Back
Top Bottom