Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam uanze mara moja ili kurataibu maendeleo yote yanayofanyika kwenye halmashauri za mkoa wa Dar es salaam.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam leo tarehe 24.10. 2024 kwenyz viwanja vya Mwengeyanga Manispaa ya Temeke.
Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi yetu na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo mkoa huu unatakiwa na chombo kinachoratibu maendeleo ya mji huu na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika hapa inakua na muunganiko ili kulete ile sura tunayoitegemea.
Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi, miradi mikubwa kama hii ikiachwa kwenye halmashauri inaweza isiweze kujiendesha hivyo kuwe na chombo cha kusimamia miradi mikubwa kama hii na kuhakikisha inaungana na jitihada zingine za maendeleo zinazofanywa katika halmashauri za mkoa huu.
Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa.
Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalumu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimaraifa.
TAMISEMI